The Knowledge Seeker
JF-Expert Member
- Apr 13, 2019
- 3,418
- 5,028
Pascal Mayalla hakika CCM mna chakujivuniaJana Jumamosi nilikuwa Kigsmboni ambako kulikuwa na tamasha la Kigambono Tamu tamasha ambalo lilirushwa hewani na Wasafi Tv tangu asubuhi mpaka jioni.
Nilichojionea kwenye tamasha hilo ni uwepo wa mamia ya vijana wasichana kwa wavulana kumlinda mama Samia, kuna kikundi cha Ukimvaa Samia nasi tutakuvaa! Kikundi cha uhamasishaji cha Samia na vingine vingi, vikundi vyote hivi viwepewa sare ambazo zinamajina ya kikundi na vikundi hivi hulipwa baada ya shughuri.
Kati ya mambo wanayoyafanya ni kusaidiana na jeshi la polisi kulinda mikutano ya viongozi wa serikali! Hili linahitaji ufafanuzi tujue kama jeshi la polisi halina uwezo wa kulinda.
Hawa vijana huletewa muziki ambapo hata kama shughuri ni ya dakika chache basi itachukua saa nyingi kumalizika kwani muda wote ni vijana kucheza, ni uhuni mtupu ukizingatia ujana wao.
Kwa hili linaloendea CCM inatengeneza jeshi la vichaa jeshi ambalo litakuja kuwa vigumu kulidhibiti kwani kuna wengine watajitoa na kuingia mitaani kufanya uhalifu.
Just imagine mbegu kama hii ccm wanaipanda kila mkoa.
Alafu baadae wanadai mashehe ni magaidi, mara chadema wana vurugu