Urusi, China, Iran na Saudi Arabia zaanza maandalizi ya kuachana na matumizi ya Dola ya Marekani

Ndio maana kwenye comment yangu ndefu nimesema leo wala kesho hutomuona Brazil anadunduliza hela yake ya dharura ikahifadhiwa kwenye Yuan. Nikasema China atafanikiwa kufanyia transaction kwenye Yuan baadhi ya nchi na baadhi ya bidhaa ila sio hela yake kuwa foreign reserve currency ya nchi.


Yuan itatumika kwenye international payments kwa bidhaa za Kichina au mauzo ya kwenda China. Nani akanunue microchips Taiwan kwa Yuan? Nani akanunue automobiles Japan kwa Yuan? Na hayo malipo hayatakuwa na balance kwa nchi zote, unakuta huku China inanunua malighafi za RMB 50 billion na inauza bidhaa za RMB 180 billion. Na hiyo currency haitumiki pote. Sisi bongo tunaweza nunua mafuta Iraq kwa $ na hatuwauzii hata kiberiti lakini hamna kesi si tutabalance dola kwa mauzo mengine nchi yoyote duniani.

Hutasikia Kenya imeweka hakiba, hazina, dharura kwenye Yuan. Hata hao Saudi Arabia bado sana watakuwa na reserve ya $. Kuliko kutumia Yuan kama reserve central banks zao si bora watumie gold kama Russia inavyofanya.
 
Huo usahihi upo wapi sasa hapo ?
Hili neno CCP ni neno la propaganda chafu dhidi ya China. Kifupi sahihi cha chama cha kikomunisti cha China katika lugha ya kimombo ni CPC duniani kote na wala sio CCP.
CCP ni name na CPC ni official name, yote ni sahihi. Mbona hujataka Japan tuiite Nippon kama wao wanavyojiita. Na Turkey iliyobadilisha jina kuwa Turkiye tutaiita Turkey hivyo. Sisi sio diplomats wala sio official forum.

Ukitaka kukazana na majina utatumia nguvu sana tukiijadili Soviet Union
 
Hamna kitu hapo, sasa China biashara zake na nchi za magharibi ambayo ndio kubwa zaidi atafanyaje.

Hata hivyo kumezuka tena wimbi la makampuni ya Marekani kuanza kuondoka tena China, yanafanya "Disinvestment from the communist state."
Unakimbiaje soko la over 10% ya wanadamu wote duniani na zaidi ya 800mil middle class?

Mfanyabiashara makini hatishwi na porojo. USA alikuwa anatrade na NAZI Germany hadi alipoamua kuingia vitani upande allies. Usimwamini mfanyabiashara anayetafuta faida
 
Nimeuliza ulichoa andika. Japan na Turkey hazipo kwenye maandishi yako.

Official name ndicho kiwakilichi kikuu na wala sio maneno ya kuokoteza yasiyo leta maana yoyote ile ya kueleweka.
Japan ipo kwenye maandishi yangu.

Official name ipo kwenye Kichina hizi nyingine ni translations, ili ukaze kichwa basi andika Kichina ili uwe official. Na ukitaka kuwa official kwenye majina kwanini unaiita China tu, si inaitwa People's Republic of China?
Ukisema China what if ninajua unamaanisha Republic of China (ROK) ile Taiwan?
 
Nikasema China atafanikiwa kufanyia transaction kwenye Yuan baadhi ya nchi na baadhi ya bidhaa ila sio hela yake kuwa foreign reserve currency ya nchi.
Israel's central banks adds Chinese yuan to its reserve currency holdings.

Ikiwa Israel kwenye foreign currency reserve ameweka Yuan ndio washindwe washirika wake kama Brazil waliokubaliana kwa mikataba kabisa
 
Urusi yuko na rubble anatumia tayari baada ya kupigwa pini.
Mchina mwongo huyo
Iran hamna kitu hata azire.
Rial Saudi siku nyingi na ina thamani ila akitoka hapo kwake hamna kitu
 
Kwani mrusi alipokatangaza kuanza kuuza Gas na mafuta yake kwa ruble ilikuwaje? Mbona biashara ilifanyika kama kawaida na ruble ikapanda thaman dhidi ya Dolla?
 
Urusi yuko na rubble anatumia tayari baada ya kupigwa pini.
Mchina mwongo huyo
Iran hamna kitu hata azire.
Rial Saudi siku nyingi na ina thamani ila akitoka hapo kwake hamna kitu
Kilichopo now wanaanza na local currency zao! Ila BRICS hipo katika maandalizi ya kutengeneza currency yao ya pamoj
 
Who cares? Mbona China wana viwanda vyao watauza bidhaa zao tu
Wewe kinachokusumbua ni ushabiki wa kijiweni, hujui kwamba watu huko China wameshaanza kupoteza ajira kufuatia kuanza kuondoka kwa hayo makampuni.

China hana teknolojia yeye kama yeye na anategemea kuipata kutoka nje hasa Marekani sasa kwa hii hali China anakuwa kwenye wakati mgumu sana.
 
Ao hawajaanza kutoka leo! Anzia Trump Rais akaweka na vikwazo kibao vya kibiashara
 
Wataka kunambia Yuan na Rubu ndio ziwe hela za matajiri ulimwenguni? emu fikiria mara mbili mbili how is it possible, tajiri aliyezoea Dola na Euro sasa akashike Real ya Saudia Arabia
 
Wataka kunambia Yuan na Rubu ndio ziwe hela za matajiri ulimwenguni? emu fikiria mara mbili mbili how is it possible, tajiri aliyezoea Dola na Euro sasa akashike Real ya Saudia Arabia
Matajiri walitoka wapi si kwa biashara tu za kila siku ogopa sana nguvu ya soko
 
Yaani unapiteza muda kumjibu huyo jamaa?

Foxconn ilikuwa imeajiri watu 100,000 Kiwanda kinahama
 
Yaani unapiteza muda kumjibu huyo jamaa?

Foxconn ilikuwa imeajiri watu 100,000 Kiwanda kinahama
Suala la kupoteza ajira hilo haliepukiki nilishasema.

Ila kumwambia mwenzako anapoteza muda inaonyesha kuwa mijadala huiwezi tunaenda kwa hoja kama ulivyosema Foxconn ikahamishwa kuna watu watapoteza ajira ni hoja nzuri.

Jitahidi uwe greater thinker punguza mihemko
 
Huko China wameshaanza kupoteza ajira kufuatia kuanza kuondoka kwa hayo makampuni.
Hayo makampuni yanaondoka kwa sababu za kisiasa kwa sababu wanahofia kuinuka kwa China kiuchumi na kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu na ushawishi duniani.

Wanasiasa wa nchi za Magharibi wanawashawishi wamiliki wahamishe viwanda vyao wakidhani watairudisha China nyuma

Ila kiuchumi, miundombinu, logistic, kiusalama, stable currency, nishati ya uhakika na soko la uhakika China bado ndo sehemu bora zaidi kwa uwekezaji pale Asia na duniani kuliko hayo mataifa ambayo wanahamishia makampuni yao kama Vietnam, India, Malaysia, Singapore n.k

Pia baadhi ya makampuni yanahama kwa sababu wanakabili ushindani mkali kutoka kwa makampuni na viwanda vya ndani

Jiulize kwa nini serikali ya Marekani imeshindwa kumsawishi Elon Musk akiondoe kiwanda chake cha magari ya Tesla pale Shanghai? Anajua changamoto yake akihama China
 
China hana teknolojia yeye kama yeye na anategemea kuipata kutoka nje hasa Marekani
Ulishawahi kutembelea Shenzhen Silicon Valley uone jinsi serikali ya China inasupport kwa kumwaga mpunga wa kutosha katika invention, innovation na R&D kwa watu wenye idea na makampuni.

Kila aina ya teknolojia katika semiconductor, automotive, aerospace, robotics, computing systems iko hapo

Ni vile tu China sio muuzaji wa teknolojia ila Mchina sio wa kumchukulia poa

Miaka ya copycat ilishapita saivi kuna baadhi ya teknolojia China yuko juu zaidi ya Marekani

Na bado wana hizo Silicon Valleys na zinakua kwa kasi kwenye majiji ya Shanghai, Beijing, Hangzhou, Suzhou, Chongqin na Zhengzhou
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…