JF ina tatizo naandika napost comment inafutika. Narudia kwa ufupi.
China haina demokrasia utawala wake ni chama kimoja, haijawahi kuwa na free general election hata moja, katiba yake haijatengamaa mwaka huu Xi kajibadilisha na kuchaguliwa tena kwa 100% hivi, wakati huo kamfunga Waziri wa Sheria aliyekuwa anapinga kuongezewa muda (kuna wanaJF walidhani ni uwajibikaji wa serikali). Central Bank yao sio independent kuna muda inaamuliwa ifanye devaluation ya RMB wakati $ inakuwa valued na soko. Nchi yao inaongozwa na chama CCP, jeshi na serikali vikiwa kitu kimoja wakati nchi zinazoaminika zinaongozwa na serikali, bunge, mahakama vikiwa independent.
Nchi kama hiyo ni risk kuhifadhi hela kwa sarafu yake. Ushawahi ona oligarchy wa Urusi katunza hela kwenye RMB au benki za China? Si wanatunza Switzerland na kwingine.
China itafanikiwa kufanyia biashara sarafu yake kwa kiasi fulani ila sio sarafu yake kuwa reserve ya nchi nyingine. Kwanza China inakwepa sarafu yake kupatikana sana duniani (kuna athari zinaambatana na fedha yako kuwa widely available).
Huwezi waambia Brazil wadundulize hela waweke akiba kwa sarafu ya China, kesho China wakiibuka wanaona biashara inawapiga chenga wanapunguza thamani ya sarafu, umeweka bilioni 500 zinakuwa bilioni 400 bila sababu za msingi. Au Brazil inatukana China ghafla Xi Jingpin akisema wafungie hawa, hakuna kenge pale CCP anagoma. Bora uko Marekani bunge huru linapitia au benki inaweza goma ikafungua kesi kwenye mahakama huru.
Kuna EU inafanya biashara sana na China, kuna Japan, India na South Korea ni maasimu wa asili wa China na wapo top 10 ya uchumi duniani, bado kuna Marekani yenyewe. Hizi hutoziona zinaitumia RMB, hapo tushaondoa nchi 4 za uhakika kati ya 10 ambazo 6 nyingine karibia ziko EU kina France, UK, Germany, etc. Hapo China anabaki na uhakika wa Russia ambayo ni ya 8 kwa transactions za kibiashara, wakati Marekani ndio ya kwanza kwake.
Na bado Biden mayaimayai yupo, hakai term nyingine huyu. Akija Rais aggressive kama walivyokuwa kina Reagan mtakuja gundua Marekani ina nguvu sana kiuchumi ikiamua. China bado bado tupo na status quo ileile