Radar yenyewe hii hapa 48Y6-K1 Podlet radar,imeharibiwa na HIMARS. Ina range ya 200-600km hivyo ina uwezo wa kucover mpaka Kiev mji Mkuu wa Ukraine.
Ni Radar ya kisasa na imeanza kufanya kazi 2015,ndo Radar inayotumiwa na hata S400 kuangalia targets.
View attachment 2298098
Radar yenyewe hii hapa 48Y6-K1 Podlet radar,imeharibiwa na HIMARS. Ina range ya 200-600km hivyo ina uwezo wa kucover mpaka Kiev mji Mkuu wa Ukraine.
Ni Radar ya kisasa na imeanza kufanya kazi 2015,ndo Radar inayotumiwa na hata S400 kuangalia targets.
View attachment 2298098
Taarifa nyingi za jeshi la Ukraine zinawekwa chumvi wana shirikiana na waunda silaha wa magharibi kutangaza indirectly biashara ya silaha - ndio maana wanakimbilia kutangaza kwamba eti wameteketeza silaha za kisasa za Urusi na kuzitaja kwa majina,lengo ni kuwaribia biashara za silaha Warusi kwamba silaha zao ni za low quality hivyo hazifahi - ndio walivyo roho mbaya na ubinafsi uliyo kubuhu!!
Ninacho kisema hapa ni kweli tupu na wala siweki chumvi - chukulia mfano wa Urusi kutangaza kwamba wamefanikiwa kushambulia na kuharibu baadhi ya makombora ya HIMARS na hifadhi ya roketi zake - loh, Warusi walipo tangaza hilo,basi Waamerika wakaja juu kama nini, wakikanusha ukweli huo, yaani mpaka wizara ya ulinzi,wizara ya mambo ya nje na Serikali ya Zelensky wote wakakanusha vikali madai ya Urusi, just imagine, mpaka Ikulu inafikia hatua ya kukanusha taarifa za jeshi la Urusi, what does that tell you?? Halafu, kitu chenyewe ni HIMARS stuff not a big deal at all lakini Waamerika wanakanusha mpaka mishipa inawatoka, mnajua kwa nini?? Hawataki biashara ya HIMARS itiwe dosari kwamba silaha yao inaweza kushambuliwa na kuharibiwa kirahisi, lakini linapokuja suala la kuhusu uwezo wa silaha za Urusi au Uchina mara zote vyombo vya habari vya magharibi ukejeli na kubeza beza uwezo wa silaha za Warusi na Wachina kwamba ni takataka - yaani kampein zao chafu zinakuwa driven na uchoyo na roho zao za kutu, hawataki kabisa ushindani wa kibiashara au kuzidiwa kete na Urusi au Uchina wanatumia media zao, hongo na vitisho kuwalaghai potential buyers wa silaha zao - kumbukeni vitisho Turkey ilipotaka kununua S-400 kutoka Urusi, India vile ilitishiwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wakinunua S-400 kutoka Urusi, kama nakumbuka vizuri hata China iliwahi kukemewa au kutishiwa kuwekewa vikwazo iwapo wangenunua S-400 kutoka Urusi, mwaka juzi nchini Singapore au Malaysia mkataba wa kununua fighters 20 type SU-30 kutoka Urusi ulifutwa kutokana na shinikizo la Merikani kwamba wakizinunua basi Taifa lao litawekewa vikwazo kunyimwa mikopo.
Hujuma za kibiashara linapokuja suala la ushindani wa kuuza silaha ni mkubwa sana, ebu tuchukulie mfano wa Podlet rada type 48Y6-K1 inayo undwa Urusi kwa nini vyombo vya habari vya magharibi na vyombo vyao vya ulinzi linaizungumzia sana,kunani? Jibu ni rahisi: Rada hiyo inatumiwa sana vile vile kwenye a formidable Russian Integrated Air defense type S-400 ambayo Amerika inavalia njuga silaha hii hisinunuliwe popote Duniani, wanao kahidi wanawekewa vikwazo vya kiuchumi na kunyimwa misaada na mikopo, sasa hii habari ya kusema eti HIMARS imefanikiwa kuharibu rada ya kisasa ya Urusi inayo tumiwa kwenye S-400 air defense systems, lengo la habari hizo potofu ni kutaka kuipunguzia sifa air defense system inayo sifiwa sana Duniani na kuogopewa na majeshi ya NATO ndio maana USA inapiga vita usambazwaji wa Russian air defense Duniani - wanatoa impression kwamba yeyote ataye nunua S-400 atakula hasara kwa kuwa inaweza kushambuliwa na HIMARS na kuteketezwa kabisa - ulaghai mtupu of couse.