Ndiyo.
Lengo linaweza kuwa ni kuokoa taarifa(data) au nyaraka muhimu toka kwenye hiyo laptop.
Watu wa service wenyewe wanakuwa makampuni makubwa au freelancer ambao ni very expert kwenye hizo kazi.
Siyo kama jamaa zetu wa uchochoroni kariakoo.
Unfortunately jamaa alisahau hakuna kitu inapotea jumla kwenye mambo ya ICT. Once ukitengeneza data na kuitunza kwenye kifaa cha kielectroniki ujue bado kipo sehemu, ipo siku kinaweza kuibuka tena mikononi mwa adui zako.
Tuwe makini sana na maandishi(emails, chats, sms), mapicha, sauti, video za faragha au za matukio ya siri kubwa au faragha.
Ile permanent deletion ni illusion tu kwenye macho yetu huwa bado zina baki trails au foootprints kwenye device zetu watu wana recover au reconstruct upya hizo data.
Vipande vilivyopotea kabisa wanajazia na teknolojia za kisasa.
Kwani hizi data si zipo ktk mfumo wa nishati(energy) ya sumaku au umeme? Ukikumbuka Energy can neither created nor destroyed utaziogopa sana data.