Urusi imeingia kwenye 18 ya Marekani, dunia ijiandae kuona majimbo mapya ya Marekani katika ardhi ya Urusi

Huyu putin kaingia cha kike. Kapanikishwa kaingia mzima mzima. Hapo ndio wengi wanapokosea. Bora angebaki na kuwa mbabe wa kuchongwa. Angestafu kwa heshima na angebaki kwenye historia nzuri ya kuogofya. Hivi sasa atastafu kama mwanamke mrembo tu
 
Mmeshindwa kuelewa metaphor.
Tembo ana mwili mkubwa na mwenye nguvu lakini siku zote wanajaribu kukaa mbali na simba sababu ya tabia zao.
Simba ukimbana na akachoka atafanya chochote kile ili akumalize na haijalishi kama atakufa.



Simba kumshusha Nyati dume mkubwa inabidi wawe wengi, sembuse Tembo.
 
Ila tukiacha utani wakuu USA ana vichwa vinavyosuka sana mipango aiseee
Yan USA si ajabu akatumia miaka 10 kukusaka uingie kwenye king yake na ukikaa hapo anashikalia hadi mwisho ko haitakuwa ajabu Putin akitolewa madarakan miaka inagokuja

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 

Tuwe wakweli, Mrusi ana hali mbaya.
Ukraine anawaua sama Warusi.
Kuna makala nilifuatilia Warusi wamekimbia na kuacha mitambo na wengi wameuawa na mizoga inaokotwa sana na kuwekwe kwenye mifuko miusi.
Na papo hapo wanashusha bendera zao na kupandisha za Ukraine.

Sasa unapigwa na Ukraine bado unamtunishia kifua mamba mla watu US?

Tuache utani
 
Huu ukweli mchungu mno.
Mimi toka ile imeanza nilijua week tu tumemaliza mambo.
Pale Kieve panakuwa kwetu siye Pro Russia.
Sasa mwaka unakatika kazi kusikia tu ooh amesaini ..oh ataangusha Nuklia..

Putin ameniangusha sana..sana..ila bado nasikilizia vya mwishoni mwishoni.
 
Sikiliza rafiki. Mimi na wewe hatujui the real strategy za Urusi au USA zingine siri. Anachotamka kila mmoja sio kile anamaanisha.
Fikiri alikuwa anatangaza SMO lkn lengo kutwaa eneo fulani.
Au ukute USA analengo la kuangasha uchumi wa Ulaya ili yeye ndio ategemewe
 
Mimi ni team Putin, na hapo kabla ya kuivamia Ukraine nilikuwa naamini kwamba Russia chini ya Putin ina uwezo wa kuiangamiza nchi yeyote hapa duniani. Lkn sasa nimebadilisha imani yangu kwa Urusi, yan kusema ukweli hii vita imetuvua nguo vibaya sana. Kwa kupigwa na kanchi ambako hakafikii hata robo ya mkoa mmoja wa Russia.

Dah hii ni fedheha kubwa, Putin anatupa wakati mgumu kumtetea yeye na nchi yake huku mitaani.
 
Kumbe tupo wengi, dah Putin katuangusha sana katika vita hii.
 
Huyu putin kaingia cha kike. Kapanikishwa kaingia mzima mzima. Hapo ndio wengi wanapokosea. Bora angebaki na kuwa mbabe wa kuchongwa. Angestafu kwa heshima na angebaki kwenye historia nzuri ya kuogofya. Hivi sasa atastafu kama mwanamke mrembo tu
Sasa hivi Putin anaishi kwa stress maana anajua wakati wowote anaweza kusikia dude limetua juu ya nyumba yake na ikawa ndio mwisho wa maisha yake. Vigumu sana kushindana na Marekani maana wao (usa) wameshika kwenye mpini, afu Putin (russia) wameshika kwenye makali.
 
Hiyo ndio sababu ya kuanzisha CIA, lengo kubwa la kuanzisha kwake ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda masilahi ya nchi nje ya mipaka yake, kusaka fursa za nchi nje ya mipaka yake na kusuka mbinu mbali mbali ambazo zitakuwa na tija pamoja na faida kwa taifa. So CIA wanalipwa vizuri kwa sababu ya kazi nzuri wanayoifanya kwa nchi yao. Hicho kitengo hakina kilaza hata mmoja.
 
Tusiende mbali mkuu, soma kwanza hicho kipande hapo pichani. Putin atakufa kama Ghadafi akiwa kajificha mtaroni au pangoni. We ngoja utaona.
 

Attachments

  • Screenshot_20221006-151130.jpg
    61.1 KB · Views: 4
Pole sana kwa kuingizwa chaka na warusi mkuu. Sisi wenye uelewa tulijua tu kama ile mikwara ya urusi ilikuwa ni nguvu ya soda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…