Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kijana anatumia njia nyingi kumtetea Putin na wakati sisi tunamjua huyo putin na Russia yake zaidi ya amjuavyo yeye.Lete clip Putin akisema hayo. Ninachojua ni kwamba Putin alisema yeyote atakayeisaidia Ukraine kwa namna yoyote ile basi atashambuliwa papo hapo.
Wewe upo buza unajifanya unamjua Putin?marekani akijaribu kuivunja Russia itakuwa mwisho wake yaani wataingia kwenye vita ya moja Kwa moja na Russia kitu ambacho kila siku huyo marekani wenu anasema hataki.yaani Kwa mawazo yako haya unajiita Akilihuru?Bora ungejiita akili ovyo.Kijana anatumia njia nyingi kumtetea Putin na wakati sisi tunamjua huyo putin na Russia yake zaidi ya amjuavyo yeye.
Kaisha jichukulia majimbo yake manne. Awe na papara za nini ?Daaah, ila Putin sio kwa mikwara ile ambayo alikuwa anafoka.
Sahv Kawa kama Kabudi tu🤣🤣
we jemaa, silaha anazopewa ukraine na marekani sio silaha ndogo ni silaha nzito sana ndugu:hizo ndio polojo tuliokuwa tukiaminishwa toka tukiwa shule ya msingi, kuwa URUSI ni jitu kubwa na hatari sana kwenye medani za kivita, na dunia kuliamini kinachoonekana sasa hivi ni tofauti kabisa na uongo ule!! eti USA,ana muogopa sana URUSI,?! kama vi ji siraha hivyo vidogo tu kwa USA, ni kama manati tu ambavyo ana mpatia UKRAINE, tayari mbambe wa mchogo yupo hoi! Sasa akianza kutumia japo gobole itakuwaje?!
leo hii hata maeneo ambayo ameyatangaza kuwa sasa ni mali ya Urusi yameanza kuchukuliwa na UKRAINE. URUSI wakati vita inaanza alisema ole wake atakaye msaidia Ukraine naye atajumuishwa humo humo, nini kimemkuta USA?
Silaha Gani Russia Hana?we jemaa, silaha anazopewa ukraine na marekani sio silaha ndogo ni silaha nzito sana ndugu:
ukraine wamepewa M777 howitzer hii ni mitambo ya mabomu ya kipekee kabisa karne hii ya 21. Bomu lake moja gharama zake ni US$140,000!!!
wamepewa mitambo ya kutungulia ndege iitwayo MANPADS hii cost ya mtambo mmoja ni U.S.$38,000!!
hii ni mifano tu asee na gharama zake
Marekani imetumia gharama za trilion 3 za silaha kwa ukraine
na sio marekani pekee bali washirika wake wote
usibeze kabisa aina silaha anazopewa ukraine. Nyingine hata Mrusi mwenyewe hana.
PITIA HAPA UTAJIFUNZA KITU
![]()
What weapons has Ukraine received from the US and allies?
Since the Russian invasion, Ukraine has received billions of dollars’ worth of weapons from dozens of countries.www.aljazeera.com
Acha tu mkuu, Putin katuvunja moyo mno.Kumbe tupo wengi, dah Putin katuangusha sana katika vita hii.
Aivunje mara ngapi? Ebu uliza kwanza ni nchi ngapi ambazo zilikuwa zinaunda umoja wa soviet, na leo zimebaki ngapi, pia ilikuaje zikagawinya na kujitoa?Wewe upo buza unajifanya unamjua Putin?marekani akijaribu kuivunja Russia itakuwa mwisho wake yaani wataingia kwenye vita ya moja Kwa moja na Russia kitu ambacho kila siku huyo marekani wenu anasema hataki.yaani Kwa mawazo yako haya unajiita Akilihuru?Bora ungejiita akili ovyo.
Russia hakuna kitu pale. Kweli Russia ina nguvu lkn kwa baadhi ya nchi kama vile Belarus nk ila hana uwezo wa kupambana na nchi zenye uwezo mkubwa wa kijeshi kama USA au China.Yaani nyie wote mnaosema Russia itavunjika nawasiwasi na uwezo wenu wa kufikiria.wengine mmeenda mbali mnasema Putin atauawa.Dah Elimu yetu sometime inazalisha watu ovyo sana.au hamuijui Russia nini?
Marekani hajashindwa kuiangusha NK, bali ameona pale hamna kitu ambacho anaweza kuchukua mfano dhahabu, almasi, petrol, gesi nk.Marekani ameshindwa kuangusha utawala wa NK anaweza Kwa warusi? ifike mahali watanzania tufikirie Kwa mapana Zaidi.kwa michango ya baadhi ya watu humu kuanzia Kwa mtoa mada nimeona tatizo la kufikiria Kwa mapana ni kubwa Sana.
Hiyo walivunja Warusi wenyewe tena na raisAivunje mara ngapi? Ebu uliza kwanza ni nchi ngapi ambazo zilikuwa zinaunda umoja wa soviet, na leo zimebaki ngapi, pia ilikuaje zikagawinya na kujitoa?
Basi hujui chochote NK anarasilimali za kutosha.Marekani hajashindwa kuiangusha NK, bali ameona pale hamna kitu ambacho anaweza kuchukua mfano dhahabu, almasi, petrol, gesi nk.
North Korea inashindwa hata kujilisha yenyewe, sasa Mmarekan atapata kitu gan cha maana kutoka kwao.
Basi hujui chochoteRussia hakuna kitu pale. Kweli Russia ina nguvu lkn kwa baadhi ya nchi kama vile Belarus nk ila hana uwezo wa kupambana na nchi zenye uwezo mkubwa wa kijeshi kama USA au China.
Marekani hana muda wa kugfanya mabo ya kijinga hayo ambayo hata balozi wa Kenya anayaona kuwa ni ya kifala; yaani kuvamia ardhi ya nchi nyingine kuwa ni yao. Hayo mambo ya conquest yalifanywa na watu wa zamani akina Alexander the Great kwa kutumia mikuki na farasi, siyo ya dunia ya leo.Za asubuhi ndugu zangu, kwema?
Kwa wale wanajamii forums wenzangu wafuatiliaji wa siasa za kibabe na za kimikakati za nchi za magharibi hasa Marekani. Bila shaka mtakubaliana na mimi kwamba sasa Russia (itake isitake) inakwenda kugawana baadhi ya majimbo yake ya mpakani na Marekani kupitia mgongo wa vita yake (Russia) na Ukraine.
Ni nani asiejua kwamba toka miaka mingi iliyopita, lengo kuu la Marekani na washirika wake lilikuwa ni kuigawanya Urusi vipande vipande ili iwe na eneo dogo, jeshi dogo na uchumi wa kawaida kwa ajili ya masilahi mapana ya kijeshi, kiuchumi na kiubabe kwa Marekani na washirika wake!
Hata kugawanyika kwa umoja wa nchi za Soviet pia kulikuwa na mkono wa Marekani na washirika wake, ambao wanataka kuiona Russia inakua nchi yenye kaeneo ka kawaida, jeshi la kawaida na uchumi wa kawaida kama ilivyo Iran, North Korea, Venezuela nk.
Sasa basi, kwa vile mkakati wa kuigawanya Urusi kwa njia ya kawaida ulishindikana, ndo ukatengenezwa mkakati wa kuanzisha zengwe katika mipaka ya Russia kwa kuitumia nchi ya Ukraine huku Marekani akiamini kwamba zengwe hilo lingeweza kuzaa matunda kwa kuishawishi Russia (bila kujua) iingie katika vita na Ukraine, na hatimae baadae Urusi itapoanza kuwa weak (kuelemewa) kutokana na vita hivyo.
Marekani na washirika wake waitumie nafasi hiyo kuitwanga Russia (kupitia jeshi la Ukraine) na hatimae kuingia mpaka Russia kama vile Russia ilivyoingia Ukraine. Ukraine itapoingia Russia, Marekani ataendelea kutuma silaha nzito nzito mno za kijeshi ili kuwapa nguvu zaidi wanajeshi wa Ukraine kuteka baadhi ya majimbo ya Russia yaliopo katika mpaka na Ukraine.
Ikumbukwe kwamba Marekani na washirika wake hawajaingia kwenye hii vita kijeshi, lkn wamekuwa wakituma silaha mbali mbali kwa jeshi la Ukraine ili kutimiza mipango yao, na kwa kiasi kikubwa zimeleta mafanikio makubwa kwa jeshi la Ukraine.
Mmarekani chini ya CIA yake sio mjinga wa kutuma tu mamilioni ya dola na silaha nzito nzito kwa Ukraine bila kujua hizo hela atazirudisha vipi. Bila shaka anajua anachokifanya, na huu ni mkakati wa muda mrefu ambao Putin bila kujua ameingia kichwa kichwa vitani asijue madhara yake ya baadae.
Vita hii ni kama mpira wa miguu ambapo timu iliyoanza kushambulia, sasa inashambuliwa huku wachezaji wake hadi wa akiba wakiwa hoi bint tabaani wasijue nini kifanyike ili kuzuia kufungwa.
Vita ilianza kwa Russia kuishambulia Ukraine na kuleta furaha kubwa huko Moscow hali iliyokuwa inapelekea Putin kuongea kibabe na kwa kejeli kubwa dhidi ya Ukraine na washirika wake (Marekani, UK)
Lakini sasa vita imegeuka, Russia sasa ndio inashambuliwa, furaha ya Moscow imegeuka majonzi, mpaka wanajeshi wa akiba wamepelekwa Ukraine, lkn kichapo ni kilekile.
Putin anataman ipatikane suluhu hata kesho ili Marekani asipate nafasi ya kukamilisha mission zake, ila ni kama vile amechelewa,,, na yeye kutafuta suluhu kupitia yeye mwenyewe hawezi, maana itaonekana ameshindwa vita alivyoanzisha, hivyo itakuwa aibu kwake, kwa jeshi lake na nchi yake.
Marekani anapokuwa na lengo la kuvamia nchi fulan kwa ajili ya masilahi yake fulan, basi huwa na njia nyingi tofauti tofauti za kukamilisha lengo hilo bila kujali itamchukua muda gani, na atapata kwanza hasara kiasi gani.
Tuliona alivyotumia mgongo wa Osama kuivamia Afghanistan, tuliona alivyotumia mgongo wa silaha sijui za sumu kuivamia Iraq chini ya Sadam Hussein, tuliona alivyotumia mgongo wa waandamanaji kuivamia Libya, na sasa anatumia mgongo wa jeshi la Ukraine kuivamia Russia.
Japo si kwa nchi yote, lkn kuna baadhi ya maeneo tutakuja kusikia yalivamiwa, kutekwa na kushikiliwa na jeshi la Ukraine (kumbe nyuma ya pazia) maeneo hayo yatakayotekwa yatakuwa chini ya usimamizi wa Marekani.
Hivi sasa Ukraine ishaanza kurudisha maeneo yao yaliotekwa, na kuyarudisha nyuma tena kwa kasi majeshi ya Russia. Ni swala la muda tu mtakuja kuona haya niliyoandika hapa yanatokea, na Putin hatothubutu kurusha bom la nyuklia hata 1, maana kwa vile Mmarekani atakuwa katika baadhi ya maeneo ya ardhi yake, basi akijaribu kurusha atajikuta anajiangamiza yeye mwenyew na watu wake.
Miezi kadha iliyopita China ilitaka kufanya kosa lile lile alilofanya Mrusi, eti alitaka kuivamia Taiwan aifunze adabu. Mimi kwa kutambua hatari iliyopo mbele ya China endapo angeivamia Taiwan, nilikuja fasta fasta kutoa ushauri wangu kwa ndugu zetu wa China ili kuiepusha na mtego uliokuwa umetegwa na wakubwa pale China angethubutu tu kuivamia Taiwan.
Sina haja ya kuweka link ili kuwachosha wasomaji, kwahiyo naweka tu kipande cha picha ya onyo langu hapo chini. Ila atakaetaka kuusoma uzi wenyewe niliowaandikia wa China atautafuta mwenyew ausome kwa kutulia.
Karibuni kwa uchangiaji zaidi, hasa kwa wale wenye uelewa mpana kuhusu malengo na mikakati ya vita hii.
Moderators najua kuna jukwaa la international, lkn nimeuleta uzi huu uku kwa sababu zangu 🙏
Nawatakieni siku njema.
Rais wa wakati huo wa urusi ndo alisababisha yote Yale ndo maana hata juzi alipozikwa hakupewa hiyo heshima.unaniaibisha Sana Kwa fikra hizo .Aivunje mara ngapi? Ebu uliza kwanza ni nchi ngapi ambazo zilikuwa zinaunda umoja wa soviet, na leo zimebaki ngapi, pia ilikuaje zikagawinya na kujitoa?