Urusi imeingia kwenye 18 ya Marekani, dunia ijiandae kuona majimbo mapya ya Marekani katika ardhi ya Urusi

Urusi imeingia kwenye 18 ya Marekani, dunia ijiandae kuona majimbo mapya ya Marekani katika ardhi ya Urusi

Kuna wakati najiskia kucheka, wizara ya ulinzi Russia inasema tumeondoka maeneo Yale na Yale kwa sababu Ukraine katumia silaha za West...
Kwa nin Russians wasijibu kwa silaha za kirusi?
 
Wamarekani mwitu hamuishiwi ndoto
Screenshot_20200805-145513_1.jpg
 
Mkuu watu waliliona hili wakajaribu kumshauri Putin asiingie vitani, yeye akapuuza.
Sasa acha avune alichopanda, bahati mbaya alipanda mizabibu afu yeye anavuna miba.
Haoni mwenzake mchina alivyochezwa na machale ya kuivamia Taiwan. Mimi nilikuwa mmoja wa walioishauri China isiivamie Taiwan na kweli walielewa.
Wewe ukiwa hapo hapo Buza na kuishauri china?????
 
Angemuogopa asingetuma silaha kwa uwazi.
Mmarekani anaepusha madhara ya vita kwa dunia kwani vita sio mchezo wa rede
Mkuu hakika wewe unaona mbali sana. Asante kwa ufafanuzi ulionyooka.
 
Kabla ya Russia kuivamia Ukrean nakuunga mkono sana kwa sababu US alikuwa hajui mrussi ana nini., Lakini baade kidogo kwenye hii vita ama operation US akagundua kumbe jamaa ni mweupe sana, Putini alifungasha vifaru vya tokea Soviet na USSR msururu toka gongo la mboto hadi kariakoo, Amerika wakawa wanacheka sana kwamba kumbe jamaa silaha hizi ndio alijiandaa nazo kuvamia ukrean??

Jibu likawa rahisi US akatoa ile Javeline na Stinger ambayo unaweka begani unapiga kwa 16km, biashara ya vifaru kwa russia ikafa, akashindwa Kyiv na maeneo mengine sasa karudi Donbas anachezea HIMARS yaani US wanampiga russia kama mtoto mchanga, usishangae Zelensky akatawazwa kuwa rais wa Russia hapo baadae kidogo
Huu ndio ukweli ambao vijana wa Putin wengi hawataki kuusikia.
 
Mimi Mrussia wa huku Madongo kuinuka,niliambiwa vita ile Ukraine ingeisha ndani ya week tu.
Nilipona week imepita nikafa moyo juu ya ushindi.
Kusema kweli tunabisha tu ila yule Comedian asingeweza kujiamini vile kubaki Ukraine kwa ile Mikwara aisee.
Jamaa anakuja kuwa Man of the Match kama vile Suarez alichotufanya na Ghana ile 2010 WC.
Habari za kushupaza mishipa juu ya Russia zimenifanya nione aibu sasa kwa Jirani zangu Ukraine.

Putin the KGB aliniaminisha kuwa anaikaanga Ukraine kwa sekunde tu..anyway ngoja tusubiri silaha zilizobakia.
Mkuu Mmarekani kupitia CIA yake, kamwe huwa hawaingii kwenye vita au kufadhili vita bila kufanya research yoyote ili kujiridhisha kwanza na kile watachokifanya.
Kwahiyo toka mwanzo wa vita au kabla ya vita, tayari Mmarekani alikuwa ashajua kwamba ni lazima Russia itakuja tu kushindwa vita (haijalishi ni lini) afu ndipo hapo watakapokamilisha mipango yao.
 
hujamsikia mpambe wake yule kiongozi wa chechinia,amemshauri atumie tu nyuklia,ili mambo yasiwe mengi
Yule kiongozi wa chech hajui ni hatari gani itakuwa mbele yao endapo Putin atathubutu kutumia nuk.
Bahati nzuri Putin na maofisa wake wameshaiona hatari iliyopo mbele, kwahiyo wamesitisha uwezekano wa kutumia nuk ktk vita hii.
 
Mimi sio shabiki wa Rusia wala wa Ukrain.
Ila nacho kumbuka Rusia alitangaza Oparation Ukrain ndani sijui ya week mbili sijui na kuaidi ataichukua miji ya Ukrain pamoja na Mji mkuu wa Kiev.

Ila sasa naona miezi sita sasa imekata na sijaona Mji wa Kiev ukichukuliwa.

Na bado mtu anakuwa Bishi kama Ng'onda
Putin alipiga mkwara kwamba kama wanajeshi wa Ukraine hawatojisalimisha wao na silaha zao au kumpindua raisi wao. Basi wajue kwamba siku 5 zilizopo mbele yao ndio utakuwa mwisho wao.

Sasa jeshi halikujisalimisha na badala yake linatoa kichapo kitakatifu kwa genge la Putin mpaka mwenyew anahisi kuchanganyikiwa.
 
"Fikiri kwanza is the most important thing" hayo ni maneno niliyo kuwa naambiwa na Mwalimu wangu wa Kihindi wa Physics nikiwa O-Level.

Kitu ambacho umesahau ni kwamba mpaka sasa Urusi hainjatangaza vita kamili inacho fanya ni specially operation sio vita kamili - Putin akitangaza vita kamili dhidi ya Ukraine Zelensky na jeshi lake halitachukua round kumbukeni vita vya jeshi la Urusi na:Chechenyena,Georgia na Syria nk, je kulitokea nini eventually tukiwekea maanani kwamba mataifa hayo yalikuwa yana saidiwa kijeshi na silaha nzito kutoka Merikani, sasa swali,je,walifakiwa kushinda jeshi la Urusi, jibu ni hapana - sasa ni kitu gani kinawapa imani kwamba mapigano ya Ukraine yatakuwa tofauti kidogo, FYI, kipigo kipo pale pale Putin bado afanya mahesabu makali ya kuwakata ngebe - Putin atawashangaza wengi.

Hapa naona umekazania kuisema Urusi kwamba si lolote si chochote kwenye medani za kivita kisa, Ukraine,yaani mnajifanya kusahau jinsi taifa kubwa lenye uwezo mkubwa kijeshi/silaha lilivyo vurumishwa na kudhalilishwa na kushindwa na wakulima wa mpunga wavaa sandals za kakata mbuga hilo hamlisemi, miaka miwili iliyo pita mambo kama hayo hayo ya VietNam yalijirudia tena huko Afghanistan Dunia nzima iliona kwenye luninga jinsi wanajeshi wa Kimerikani na Majenerali wao walivyo kuwa wanatimua mbio kwenda kupanda ndege za mizigo za jeshi la Merikani wakiogopa kipigo cha wanamgambo wa kitelabani walio kuwa wanasogerea airbase ya Kabul. Swali hapa ni: ilikuwaje tena taifa la Kimungu Mungu kuvurumishwa na kushindwa na wanamgambo wa KivietCong na baadae wajukuu wa Mulla Omari huko Afghanistani!!!
Ni uhuru wako kufikiri hicho unachofikiri mkuu. Ila uendelee kutega sikio kuhusu vita hivi vinavyoendelea huko Ukraine, nina imani siku zijazo hautoonekana tena humu kuandika hiki ulichoandika.
 
Back
Top Bottom