Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Mtazamo mfupi huo uliojaa mawazo ya ugombea uhuru wa miaka sitini; Uingereza, Ufaransa na Israel wamevamia nchi gani. Mgawanyo wa ardhi baina ya Israel na Palestina ulifanywa na Umoja wa mataifa mwaka 1947 kufuatia mapendekezo ya United Nations Special Commission on Palestine. Waarabu wengine hawataki kuwapo kwa Tiafa la Israel, na ndiyo maana ya mgogoro huo. Wangetambua tu mipaka hiyo iliyowekwa na umoja wa mataifa kama Tanganyika ilivyotambua mipaka baina yake na nchi za Rwanda na Burundi ambayo iliweka na umoja wa mataifa baada ya vita ya kwanza, kusingekuwapo mgogoro.
Acha kuruka Falkland pale pamekuaje na uk na kule guantanamo na us pamekuaje kuaje
Venezuela avamie tu sababu ni mambo yakawaida hatakama hayapendezi
 
Mifano yako mingi ni propaganda tu za wapigania uhuru. Dunia tunayoshi leo siyo ile ya zamani, huwezi kusema kuwa kwa vile mambo fulani yalifanyika mwaka 1884 basi nawe uyafanye leo. Kama mwaka 1884 walikuwa wanaandika barua kwa mikono leo tunaandika kwa computer.

Hawaii ni jimbo halali la Marekani kama ilivyo Texas na Alaska; inawakilishwwa na Congressman mmoja na Maseneta wawili kwenye bunge la marekani, na pia hupiga kura kumchagua rais wa Marekani.

Israel na Palestina waliganywa aradhi na Umaja wa Mataifa, hakukuwa na Taifa la Israel lililovamia Taifa jingine la Palestina kwani wakati huo eneo hilo lilikuwa ni koloni la Uingereza. Ni mwaka huo 1948 ndipo mataifa ya Isarel na Paletsina yalipoundwa.

Mayote lilikuwa koloni la Ufaransa tangua miaka 1884 na wala wananchi wenyewe hawajawahi kudai uhuru; hawakuvamiwa leo.

Visiwa vya Falklands vilikuwa tupu kabisa wakati Uingereza inavichukua mwaka 1765. Argentina ilividai kwa vile tu vikoi jirani yake lakini visiwa hivyo havikuwa kukaliwa na watu wa aina yoyote ispokuwa waingereza tundio walianzisha maskani pale. Ujirani hauhalalishi kujichukulia.

Angola pamoja na jimbo lake la Cabinda lilikuwa koloni la wareno kwa kufuata mipaka ya mwaka 1884; walipopata Uhuru walipata kama nchi moja.

China na Tibet ni tatizo kama hilo la Urusi; Tibet lilikuwa Taifa lenye serikali yake China ikaivamaia, na mpaka leo hawelewani pale Tibet.
Kwahio kama jambo limetokea miaka ya 80s ndio liachwe lisiongelewe
Kama hvyo hata Crimea inapiga kura kumchagua rais wa Russia na pia ina wawakilishi wote na inatumia nyenzo zote kotekea Moscow hvyo basi napo paishakua pakwao
Venezuela avamie tuuu
 
Acha kuruka Falkland pale pamekuaje na uk na kule guantanamo na us pamekuaje kuaje
Venezuela avamie tu sababu ni mambo yakawaida hatakama hayapendezi
Maswali yako yote yanaonyesha ufinyu wako kwani hujui kuwa Falklands ni kisiwa ambacho hakikuwa kinakaliwa na mtu yoyote miaka hiyo ya 1700 kabla ya Uingereza kuanza kuweka makazi yake pale, na Guantamano siyo ardhi ya US ila imekodiwa na US kama ambavo Hong Kong ilivyokuwa imekodiwa na Uingereza. Baada ya Mkataba wa ukodishaji Guantanamo itarudi Cuba
 
No.
Kuheshimu mipaka ni jambo la muhimu sana kwa karne hii na zama hizi za sasa. Aidha, Sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya kimataifa inafaa sana kuheshimiwa ili kulinda amani na pia kulinda usalama na maisha ya watu. Ubabe wa kuvamia nchi za watu wengine au kujimegea ardhi kwa nguvu kutoka kwa mataifa ya jirani siyo kitu kizuri hata kidogo kwa dunia ya sasa iliyostaarabika.
Sasa hamujiulizi kama haya yanayotokea sasa nimatokeo mabaya ya kufumbia macho yalokua yanatokea zamani
Mkitaka haya majambo yaishe lazma huo ulimwengu mnaodai umestaarabika ukae chini urekebishe makosa ya zamani halaf ugeukia na haya makosa mapya
Yaani kuikalia kimya marekani inayoikalia guantanamo bay kinguvu nimoja kwamoja kua unahalalisha anachokifanya Russia pale Ukraine na analotaka kulifanya Venezuela
 
Kwahio kama jambo limetokea miaka ya 80s ndio liachwe lisiongelewe
Kama hvyo hata Crimea inapiga kura kumchagua rais wa Russia na pia ina wawakilishi wote na inatumia nyenzo zote kotekea Moscow hvyo basi napo paishakua pakwao
Venezuela avamie tuuu
80s ni baada ya UN kuweka taratibu za Mpaika. Watu hapa wanakopi mambo yaliyotokea kabla ya UN kuwapo, na huo ndio ujinga wenyewe.
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Umesahau Tanganyika na Zanzibar,
 
Maswali yako yote yanaonyesha ufinyu wako kwani hujui kuwa Falklands ni kisiwa ambacho hakikuwa kinakaliwa na mtu yoyote miaka hiyo ya 1700 kabla ya Uingereza kuanza kuweka makazi yake pale, na Guantamano siyo ardhi ya US ila imekodiwa na US kama ambavo Hong Kong ilivyokuwa imekodiwa na Uingereza. Baada ya Mkataba wa ukodishaji Guantanamo itarudi Cuba
Acha kupotosha watu
Guantanamo ilipiga kura ama walikubaliana cuba na us kuungana baadae Cuba wakavunja makubaliano na us wa kataka ardhi yao us wakagoma
Hakuna sehem cuba wameikodisha us guantanamo uache kuona watu wajinga kijana
Unajua mgogoro ulipo baina ya Havana na Washington dc kisa nini
Venezuela na wengine wakijisikia kuvamia wavamie tu kama wanauwezo hakuna cha UN wala nini hao ndio wanasababisha yote haya kutokea
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Tanganyika kuikalia Zanzibar
Morocco kwa Sahara
Hahahahahaha
 
80s ni baada ya UN kuweka taratibu za Mpaika. Watu hapa wanakopi mambo yaliyotokea kabla ya UN kuwapo, na huo ndio ujinga wenyewe.
Sawa golan heights na israhell pale Syria mwaka 1960s
Au UN haikua imezaliwa bado
 
Safi sana Venezuela [emoji1263] kama muna haja yakufanya hivyo nauwezo munao nikiwa kama mpenda amani nawaunga mkono
Nanyie kama mnaweza vamieni tu baadae msije mkaanza kulialia maisha yamekua magumu
Akil zko fupi
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Hayo maswali unataka ajibu km nan ? Kwan usiandike km nyongeza badala ya kuifanya km attack , je ww ni raia wa urusi kubehave hivyo?
 
kwa urusi inataka kurudisha nchi zake zote zilizokuwa jamhuri, USSR, labda kama atataka kumega zile nchi ambozo hazikuwa shirikisho lake.
Ussr sio nchi ya urusi ila umoja wa mataifa mbali mbali ikiwemo Urusi
 
Huo mfano mbaya kwanini iwe Urusi na Venezuela,na sio Uingereza, Ufaransa, Israel, Marekani,ambao wote wapo kwenye ardhi za nchi nyingine kinyume cha sheria?
Kiufup ww sio mrusi unapaswa kujiuliza je ni sahihi kuvamia nchi nyingine?
 
Back
Top Bottom