Urusi kukutana na makundi yote ya kipalestina kwa mashauriano. Ni mchakato wa kuundwa taifa huru la Palestina

Urusi kukutana na makundi yote ya kipalestina kwa mashauriano. Ni mchakato wa kuundwa taifa huru la Palestina

Urusi...? Ndio kitu gani hicho?

Parestine atachelewa sana akuwekeza nguvu zake kwa Urus, hawa jamaaa wangeliamua tu wawe nchi mpja ya Israel basi

Waungane tu ili wakae kwa amani
 
unaitizama Israel kama Burundi si ndio? waisrael wamekulia hofu ya kifo mpk leo wameizoea so usifikirie wanahofia kifo
Hata hao Hamas wao kifo sio issue kwahiyo wamekutana watu wasioogopa kifo hapohakuna mshindi abadani.
 
Hiyo ardhi ilipogawanywa na UN Israel walipewa 55% na Wapalestina wakapewa 45% wakakataa wakitaka 100% yote. Wapalestina mpaka leo kuna makundi yanataka maeneo ambayo Israel haiwezi yatoa nayo yawe sehemu ya Palestina. Au wengine wanataka kabisa Israel ifutike waende sijui wapi na ardhi nzima iwe Palestina.

Kama unadhani Israel inatishika na mikutano wewe jidanganye tu, hiyo ni mikwara mbuzi kwao. Hakuna taifa la Palestina litaanzishwa kwa maeneo yaleyale wanayodai Wapalestina. Na hakuna taifa lolote litailazimisha Israel ikubali taifa la Palestina kinyume na msimamo wao wa do or die.

Pale suluhu ilikuwa ni mataifa mawili jambo ambalo wote hawataki. Huwezi wafukuza Wapalestina sababu walipolowea hapo baada ya Waisraeli kupigwa na Babylonian empire, utawala wa Byzantine, Roman empire na Muslim crusaders walizaliana hivyo ni kwao. Waisraeli walikimbia eneo lao sababu ya kuteswa na kunyanyaswa na kila jirani na kila state, hawakuikana au kuisahau ardhi yao (rejea wimbo wao wa taifa - Hatikva). Walikuwa goigoi, leo hii huwatoi hapo bora uwaue.

Huwezi waondoa Waisraeli sababu zaidi ya miaka 1400 nyuma ile ni ardhi yao, wana historia nayo na ushahidi kama magofu ya temple ya Suleiman upo.

Kwa akili ya kawaida tu, jiulize Wayahudi kwao wapi? Walijikusanya kutoka Uingereza, Ufaransa, Marekani, Canada, Misri, Uturuki, Urusi na kote uko walikuwa na tamaduni zilezile, lugha ileile na dini ileile. Kwahiyo Myahudi wa Marekani ilitokea zari tu akafanana kilakitu na Myahudi wa Uturuki maelfu ya kilometers mbalimbali? Jibu ni lazima kuna chimbuko lao, ndio hapo Israel sasa.

Ukitaka kuunda Palestina kwa masharti ya Wapalestina hawa basi waue Waisraeli wote. Nao wamejipanga kukusubiri, wakiwa na machungu na hasira za kuzunguka dunia nzima wakinyanyaswa kisa wamekimbia kwao. Sasa jichanganye waweke pembeni sheria za kimataifa waingie kwenye death mode.
Ulihadithiwa na nani kwamba pale ndiyo kwao hao Wayahudi?

Hizo hadithi za biblia ya mchongo unaziamini na bado tukuite umestaraabika na unajitambua kwa kuamini myth?
 
Uhuru wa Palestina hauwezi kupatikana bila usuluhishi wa pande zote 2 kuhusishwa na kukubaliana. Palestina atataka baadhi ya maeneo na miji kutoka Israel ili aanzishe taifa hilo, je Israel atakubali takwa hilo? Hicho kitu haliwezekani, jambo jema ambalo lingezaa matunda ni kuundwa kwa taifa moja tu la jamuhuri ya muungano wa Israel na Palestina ili iwe jamii moja, Hamas waache misimamo yao ya kidini. Bila hivyo itazuka vita vya 3 vya dunia, Israel hatanii na wala hawezi kuogopa mikwara ya Russia, China hata USA, tusubiri vita vikali sana kati ya Israel na maarifa ya kiarabu
bila USA Israel ni nyuki wa mashineni
 
Umri wangu ndiyo chanzo cha vifo?Uwe na maswali ya maana.Mwaka 1948 tu?Uliza Kaini alimuua Abili mwaka gani?
Wewe kweli punguani hata huweleki unaandika nini.

Wewe si unasema Hamas ndiyo waliaznsha vagi, waliazisha wapi?
 
Kwani Hamas walivyoanzisha vagi walotarajia kutatokea nini?
walipanga mashambuli baada ya kuona hakuna njia na kwa kuchagua vyema wakati baada ya matayarisho makubwa ya kivita kwa kadri ya hali zao.
Walijua nini kitatokea mwisho wake na baada ya maumivu makubwa.Ndio hiki cha kuundwa kwa taifa la Palestina.
historia ya dunia na kivita itawapandisha hadhi sana Hamas.
 
Si anakalia Jerusalem ambayo huko nyuma ilishakubaliwa kuwa itakuwa makao makuu ya nchi ya Palestina.
Israel wataachiwa kule kule Tel Aviv japo nako ni sehemu ya taifa hilo la Palestina.
Sasa akina Netanyahu wanataka wachukue kila kitu na wasitoe chochote .Matokeo yake wanaweza wakakosa pakubwa.
 
walipanga mashambuli baada ya kuona hakuna njia na kwa kuchagua vyema wakati baada ya matayarisho makubwa ya kivita kwa kadri ya hali zao.
Walijua nini kitatokea mwisho wake na baada ya maumivu makubwa.Ndio hiki cha kuundwa kwa taifa la Palestina.
historia ya dunia na kivita itawapandisha hadhi sana Hamas.
Basi ni vema kama walijiandaa kwa maumivu wang'ate kamba sauti ya mayowe isitoke sana.
 
Kwa maoni yangu naona Russia inatafuta platform ya kimataifa ili kuionyesha jumuia ya Kimataifa kuwa bila Russia dunia haina uwezo wa kumaliza migogoro mbali mbali ya kivita, nk
Marekani na nchi za Magharibi licha ya kupiga kelele Israel isitishe vita zimeshindwa! Diplomasia yao kimataifa kutatua mgogoro imeshindwa!
Kwa muda mrefu Israel imekuwa ikiitaka Russia kuingilia kati mgogoro huo!
Russia inaushawishi mkubwa kwa pande zote!
Russia kuwaita Wapalestina ni jitihada za kuwashawishi kusitisha vita na kuirudishia Israel mateka wao!
Sambamba na kuundwa kwa Taifa la Palestina!
Tukubalieni tu kwa sisi pro-Israel, Israel imeshindwa kutimiza lengo yake ya kukofuta kikundi cha Hamasi ili kuwakomboa Mateka wanaoshikiliwa na Hamas!
 
Hiyo ardhi ilipogawanywa na UN Israel walipewa 55% na Wapalestina wakapewa 45% wakakataa wakitaka 100% yote. Wapalestina mpaka leo kuna makundi yanataka maeneo ambayo Israel haiwezi yatoa nayo yawe sehemu ya Palestina. Au wengine wanataka kabisa Israel ifutike waende sijui wapi na ardhi nzima iwe Palestina.

Kama unadhani Israel inatishika na mikutano wewe jidanganye tu, hiyo ni mikwara mbuzi kwao. Hakuna taifa la Palestina litaanzishwa kwa maeneo yaleyale wanayodai Wapalestina. Na hakuna taifa lolote litailazimisha Israel ikubali taifa la Palestina kinyume na msimamo wao wa do or die.

Pale suluhu ilikuwa ni mataifa mawili jambo ambalo wote hawataki. Huwezi wafukuza Wapalestina sababu walipolowea hapo baada ya Waisraeli kupigwa na Babylonian empire, utawala wa Byzantine, Roman empire na Muslim crusaders walizaliana hivyo ni kwao. Waisraeli walikimbia eneo lao sababu ya kuteswa na kunyanyaswa na kila jirani na kila state, hawakuikana au kuisahau ardhi yao (rejea wimbo wao wa taifa - Hatikva). Walikuwa goigoi, leo hii huwatoi hapo bora uwaue.

Huwezi waondoa Waisraeli sababu zaidi ya miaka 1400 nyuma ile ni ardhi yao, wana historia nayo na ushahidi kama magofu ya temple ya Suleiman upo.

Kwa akili ya kawaida tu, jiulize Wayahudi kwao wapi? Walijikusanya kutoka Uingereza, Ufaransa, Marekani, Canada, Misri, Uturuki, Urusi na kote uko walikuwa na tamaduni zilezile, lugha ileile na dini ileile. Kwahiyo Myahudi wa Marekani ilitokea zari tu akafanana kilakitu na Myahudi wa Uturuki maelfu ya kilometers mbalimbali? Jibu ni lazima kuna chimbuko lao, ndio hapo Israel sasa.

Ukitaka kuunda Palestina kwa masharti ya Wapalestina hawa basi waue Waisraeli wote. Nao wamejipanga kukusubiri, wakiwa na machungu na hasira za kuzunguka dunia nzima wakinyanyaswa kisa wamekimbia kwao. Sasa jichanganye waweke pembeni sheria za kimataifa waingie kwenye death mode.
Baadhi ya unayosema yana msingi.Tatizo hujaliona kuwa mayahudi wana tabia ya kuona maumivu yao tu makali na ya wengine si chochote.Na hawataki kutoa haki za wengine .Wanajimilikisha kila kitu na kufanya ukatili mkubwa kuzuia haki za wengine.
Hapo ndipo wanapotibua kila kitu na kuwafanya na wengine waamue kupambana nao.
 
Urusi ndio mbabe wao ngoja tusubiri wayahudi wa daslam utasikia urusi inaendeshwa na wayahudi [emoji1787]
 
UONGO mtupu..
Hiyo link haisemi hivyo. Kinachoongelewa hapo ni Urusi kujaribu kufanya upatanishi wa makundi hasimu ya Palestina.
-‐--------------------------
Palestinian Authority's Mohammed Shtayyah has revealed that Russia is set to host Palestinian factions for reconcilliation talks in its capital.

"Russia has invited all Palestinian factions who will be meeting on the 26 of this month in Moscow. We will see if Hamas is ready to come to the ground with us" Mohammad Shtayyeh told the Munich Security Conference.

Hamas has always welcomed Russian reconciliation efforts. Leaders of the Palestinian Islamist factions have repeatedly visited Moscow, which maintains good relations with Hamas.

Hamas and the Palestinian Authority have failed to end their power disputes since 2007. Hamas and the smaller Islamic Jihad group demand to join the PLO but say it should be reformed.......
Kuonesha kuwa lengo ni kutafuta umoja ili kuendeleza Oslo accord juu ya kuundwa kwa taifa la Palestina.Baada ya hapo ikaendelea kama hivi....

"We are ready to engage. If Hamas is not then that's a different story. We need Palestinian unity," he said, adding that to be part of that unity Hamas needed to meet certain prerequisites.

Set up as part of the 1993 Oslo Peace Accords between Israel and the Palestine Liberation Organization (PLO) that raised hopes of Palestinian statehood, the PA has seen its legitimacy steadily undermined by Israeli settlement building in the occupied West Bank.

Many Palestinians now regard it as corrupt, undemocratic and out of touch.
 
Urusi baada ya kupata ushindi mnono kule Advidika dhidi ya Ukraine imejiona ina wajibu wa kushauriana na makundi yote ya kipalestina wakati ambapo vita vya Gaza navyo viko ukingoni kumalizika.
Inawezekana harakati hizo za Urusi ni kupiga hatua za mbele za mbele katika mchakato wa kuundwa kwa taifa la Palestina kuwahi kupata ushawishi mkubwa kwenye taifa hilo jipya ambalo tayari mataifa kadhaa ya Ulaya yameshatoa wito kwa Benjamin Netanyahu aondoe vikwazo vyake visivyokuwa na mashiko kuhusiana na taifa hilo.
Makundi yaliyoalikwa huko Moscow ni pamoja na Hamas wenyewe,Islamic Jihad yenye makao makuu Syria,PLO iliyoanzishwa na Yasser Arafat na makundi kadhaa mengine.kIkao hicho kinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Katika siku za karibuni viongozi wa Ufaransa,Uiengereza,Hispania na Ujerumani wamekuwa wakimshinikiza sana waziri mkuu wa Israel aache vipingamizi dhidi ya uundwajji wa taifa la Palestina.Macron wa Ufaransa amesema taarifa za kudai kuundwa kwa taifa la Palestina si siri tena na kwamba anataka ifanyike haraka.
Raisi wa Brazil kwa upande wake amepuuza sasa madai ya vifo vingi vya holocast.
Russia invites Palestinian factions to meet next week: Palestinian Authority PM
Kumbe ndiyo maana hizi habari zenu ni matokeo ya kujipotosha ambako huwa mmafanya kwa kushindwa kuelewa?
1. Russia hana uwezo wa kuleta hiyo suluhu. Yaani akae na wapalestina kufanya maamuzi bila kuihusisha Israel? Mbona mnawafanya Rusia waonekani ni wapuuzi fulani wa level yenu?

2. Hakuna mahala Russia kasema anawaita na kuwakutanisha, yeye amesema aya host, uelewe kwamba hosting haina maana kwamba wao watakuwa mediators. Ukumbuke kuwa hawa viongozi wa vikundi vya kipalestina wanaishi sehemu mbalimbali, anachofanya Russia ni kutaka kugharamia ili wakutane wakaongee mambo na mustakabali wao
 
Hapa ndio huwa nakuona uko mpumbavu[beyond ignorant].
Upumbavu wangu uko wapi.We unadhani mimi nazungumza porojo kama wewe.
Mimi natumia vipengele vya Usuulul fiqh.
 
Back
Top Bottom