Mkuu HAKUNA JAMII ILIYOPEWA ARIDHI HAPA DUNIANI NA MUNGU
Binadamu ni kiumbe wa kuhama hama vinginevyo wahindi wekundi wangedai aridhi yao na kuwafukuza wahamiaji wote
Wahindi wekundu walishindwa wakapotezwa kama ambavyo Waisraeli wakishindwa watapotezwa. Ni kazi ya jamii kuhamua hatma yake, Israel imechagua kutokubali kupotezwa.
Mipaka ya nchi ilijitengeneza baada ya binadamu kuzidi kustaarabika baada ya vita za kugombania maeneo
Leo hii unaambiwa Wangoni asili yao SA, Wairaki asili yao Somalia nk nk
Leo hii tunaambiwa Waarabu wote asili yao ni mashariki ya kati lakini walikuja kulowea Afrika nk nk
Hivi Waarabu walipolowea Misri, Algeria, Tunisia, Morocco na Libya ardhi ya Waafrika weusi kwanini wamekuwa dominant kuliko weusi asilia? Kilitokea kitu gani hapo katikati mpaka weusi wakapotea.
Ndio yaleyale ya Waarabu kuingia ardhi ya Wayahudi kuzaliana na baadae kuifanya yao.
Ustaarabu wa mipaka ulipoanza kufanyika basi jamii iliokua inaishi sehemu husika ndio walitambulika kama eneo lakwao
Wapalestina wapo pale kwa miaka zaidi ya 600, wamezaliana vizazi kwa vizazi pale ni kwao
Waisraeli walikuwepo pale vizazi na vizazi pia kabla ya kuhamishwa. Nao wana haki pale.
Tatizo kubwa la mgogoro huu ni Waisrael kuamini ile ni aridhi yao kwa mujibu wa imani yao walipewa na invincible God ambaye HAYUPO
Huna jukumu la kupanga Mungu ni yupi na yupi sio Mungu, kama unatetea haki za binadamu Wapalestina kuishi hapa unataka kuvunja mojawapo ya fundamental human rights ya Waisraeli, haki ya kuabudu.
Kwa mujibu wa taratibu za kidunia ile aridhi ni halali kwa wapalestina walioishi pale kwa miaka zaidi ya 600
Hakuna namna waarabu wa Afrika wanaweza kwenda nchi yoyote ya Mashariki ya kati na kudai ni kwao
Nchi ipi na mji upi, Waarabu wa mji wa Misrata pale Libya wanajua chimbuko lao ni mji gani nchi gani kwamba warudi, wana ushahidi wa kihistoria wa magofu, walifukuzwa kwamba itabidi warudi kama ilivyofanyika kwa Waisraeli?
Au haiwezekani hata kwa Black America kuja Africa kudai Afrika ni kwao..... wao ni wamarekani
Black American yupi anaongea mfano kilugha cha Igbo kinachotumika Nigeria na kuabudu mungu wa Waigbo kwamba atarudi ajue kwao ni wapi.
Wote hawajui kwao wapi, wataenda kudai nini.
Tatizo hili alilizalisha Mwingereza baada ya kuwa ignore wapalestina na kuanzisha mchakato wa taifa la waisrael kwenye aridhi yao walio ikalia miaka kwa miaka kisa imani ya dini yao inayosema ile ni aridhi walipewa na Mungu na kuna mahekalu yao
Baada ya hapo wakaanza kuokotezwa waisrael popote pale duniani na kuanza kuletwa Palestine
Na mbaya zaidi ni pale Umoja wa mataifa wa enzi hizo kukubali ombi la Waisrael kuanzisha taifa bila kushirikisha pande zote mbili na kuainisha mipaka anuai
Mgawanyo ulikuwa 55/45. Walipopigana ndio kila Israel ikishinda inafanya annexation.
Ushahidi wa kihistoria upo, sio suala la imani wala dini. Nabii Issa bin Mariam kazaliwa wapi na alikuwa kabila gani.
Tatizo kubwa la mgogoro huu watu wengi hawajui Wapalestina wanadai nini?
Two states solution bado inakuwa inawapendelea zaidi Waisrael
Ilianza na 60/40 sasa hivi ipo almost 80/10
Kuna watu hata hawajui maisha ya Gaza na West Bank yakoje
Wanaona ni kama wanavyoishi kwenye nchi zao tu
Gaza ni JELA ya wazi ile
West Bank inakaliwa kibabe kuliko hata makaburu walivyo ikalia Soweto
Dunia nzima tumewa lebel wapalestina kama MAGAIDI as if jamaa ni wajinga sana kudai HAKI yao
Kwa hali ilivyo sasa hakuna pa kuwapeleka mahali Waisrael wala wapalestina
Taifa moja haitakuja kukaa iwezekane.... chuki ni kubwa mmno
Two state solution ya 50/50 ikiwemo Jerusalem angalau ikifanikiwa inaweza kuleta amani
Two state solution ya 50/50 ni ngumu sana kufikiwa maana hata 45% Wapalestina waliikataa mwanzoni, wala sidhani kama Israel itakubali 55% kwa sasa.
Wajaribu kukubaliana kama hawataki waendelee kupigana muda bado upo. Dunia ina mambo mengi ya kufanya sio vifo vyao tu.