Hiyo ardhi ilipogawanywa na UN Israel walipewa 55% na Wapalestina wakapewa 45% wakakataa wakitaka 100% yote. Wapalestina mpaka leo kuna makundi yanataka maeneo ambayo Israel haiwezi yatoa nayo yawe sehemu ya Palestina. Au wengine wanataka kabisa Israel ifutike waende sijui wapi na ardhi nzima iwe Palestina.
Kama unadhani Israel inatishika na mikutano wewe jidanganye tu, hiyo ni mikwara mbuzi kwao. Hakuna taifa la Palestina litaanzishwa kwa maeneo yaleyale wanayodai Wapalestina. Na hakuna taifa lolote litailazimisha Israel ikubali taifa la Palestina kinyume na msimamo wao wa do or die.
Pale suluhu ilikuwa ni mataifa mawili jambo ambalo wote hawataki. Huwezi wafukuza Wapalestina sababu walipolowea hapo baada ya Waisraeli kupigwa na Babylonian empire, utawala wa Byzantine, Roman empire na Muslim crusaders walizaliana hivyo ni kwao. Waisraeli walikimbia eneo lao sababu ya kuteswa na kunyanyaswa na kila jirani na kila state, hawakuikana au kuisahau ardhi yao (rejea wimbo wao wa taifa - Hatikva). Walikuwa goigoi, leo hii huwatoi hapo bora uwaue.
Huwezi waondoa Waisraeli sababu zaidi ya miaka 1400 nyuma ile ni ardhi yao, wana historia nayo na ushahidi kama magofu ya temple ya Suleiman upo.
Kwa akili ya kawaida tu, jiulize Wayahudi kwao wapi? Walijikusanya kutoka Uingereza, Ufaransa, Marekani, Canada, Misri, Uturuki, Urusi na kote uko walikuwa na tamaduni zilezile, lugha ileile na dini ileile. Kwahiyo Myahudi wa Marekani ilitokea zari tu akafanana kilakitu na Myahudi wa Uturuki maelfu ya kilometers mbalimbali? Jibu ni lazima kuna chimbuko lao, ndio hapo Israel sasa.
Ukitaka kuunda Palestina kwa masharti ya Wapalestina hawa basi waue Waisraeli wote. Nao wamejipanga kukusubiri, wakiwa na machungu na hasira za kuzunguka dunia nzima wakinyanyaswa kisa wamekimbia kwao. Sasa jichanganye waweke pembeni sheria za kimataifa waingie kwenye death mode.
Mkuu HAKUNA JAMII ILIYOPEWA ARIDHI HAPA DUNIANI NA MUNGU
Binadamu ni kiumbe wa kuhama hama vinginevyo wahindi wekundi wangedai aridhi yao na kuwafukuza wahamiaji wote
Mipaka ya nchi ilijitengeneza baada ya binadamu kuzidi kustaarabika baada ya vita za kugombania maeneo
Leo hii unaambiwa Wangoni asili yao SA, Wairaki asili yao Somalia nk nk
Leo hii tunaambiwa Waarabu wote asili yao ni mashariki ya kati lakini walikuja kulowea Afrika nk nk
Ustaarabu wa mipaka ulipoanza kufanyika basi jamii iliokua inaishi sehemu husika ndio walitambulika kama eneo lakwao
Wapalestina wapo pale kwa miaka zaidi ya 600, wamezaliana vizazi kwa vizazi pale ni kwao
Tatizo kubwa la mgogoro huu ni Waisrael kuamini ile ni aridhi yao kwa mujibu wa imani yao walipewa na invincible God ambaye HAYUPO
Kwa mujibu wa taratibu za kidunia ile aridhi ni halali kwa wapalestina walioishi pale kwa miaka zaidi ya 600
Hakuna namna waarabu wa Afrika wanaweza kwenda nchi yoyote ya Mashariki ya kati na kudai ni kwao
Au haiwezekani hata kwa Black America kuja Africa kudai Afrika ni kwao..... wao ni wamarekani
Tatizo hili alilizalisha Mwingereza baada ya kuwa ignore wapalestina na kuanzisha mchakato wa taifa la waisrael kwenye aridhi yao walio ikalia miaka kwa miaka kisa imani ya dini yao inayosema ile ni aridhi walipewa na Mungu na kuna mahekalu yao
Baada ya hapo wakaanza kuokotezwa waisrael popote pale duniani na kuanza kuletwa Palestine
Na mbaya zaidi ni pale Umoja wa mataifa wa enzi hizo kukubali ombi la Waisrael kuanzisha taifa bila kushirikisha pande zote mbili na kuainisha mipaka anuai
Tatizo kubwa la mgogoro huu watu wengi hawajui Wapalestina wanadai nini?
Two states solution bado inakuwa inawapendelea zaidi Waisrael
Ilianza na 60/40 sasa hivi ipo almost 80/10
Kuna watu hata hawajui maisha ya Gaza na West Bank yakoje
Wanaona ni kama wanavyoishi kwenye nchi zao tu
Gaza ni JELA ya wazi ile
West Bank inakaliwa kibabe kuliko hata makaburu walivyo ikalia Soweto
Dunia nzima tumewa lebel wapalestina kama MAGAIDI as if jamaa ni wajinga sana kudai HAKI yao
Kwa hali ilivyo sasa hakuna pa kuwapeleka mahali Waisrael wala wapalestina
Taifa moja haitakuja kukaa iwezekane.... chuki ni kubwa mmno
Two state solution ya 50/50 ikiwemo Jerusalem angalau ikifanikiwa inaweza kuleta amani