Urusi kuvamia na kuteka Ukraine sio habari ila Ukraine kuvamia kilomita 1,000 ndani Urusi na kuteka ni habari kubwa Sana ya kusisimua

Urusi kuvamia na kuteka Ukraine sio habari ila Ukraine kuvamia kilomita 1,000 ndani Urusi na kuteka ni habari kubwa Sana ya kusisimua

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
1,856
Reaction score
2,417
Tangu mwanzo wa vita wengi walitarajia Urusi kuvamia Ukraine na kuteka yote NDANI Ya muda mfupi Sana
Na pengine kumfurusha Zelensky Kama sio kumuangamiza kabisa

Lakini Cha ajabu huu ni mwaka wa pili Urusi inapambana na Ukraine
Huu ni ushindi mkubwa kwa ukraine

Lakini Cha ajabu Leo wamevamia Eneo la Urusi na kuliteka
Pamoja na kwamba Urusi atatumia nguvu kubwa Sana kumuondoa Kama baba baunsa anavyofanya akiona mtoto mdogo anaelekea kumzidi maarifa ya mapigano

Ukraine kuendelea kuilinda serikali yake isipinduliwe mpaka Leo na nchi iliyojitapa ni super power ni ushindi mkubwa

=====

Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi: Maswali matano muhimu - BBC News Swahili​

Maswali 5 kuhusu uvamizi wa Ukraine mjini Kursk, Urusi​


Wanajeshi wakiwa vitani

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mashambulizi ya Ukraine katika eneo la Kursk yataathiri jinsi vita vitakavyoendelea

Uvamizi wa Ukraine katika eneo la Urusi tarehe 6 Agosti ulipokelewa kwa mshangao sio Moscow pekee, bali pia kwa raia wa Ukraine hasa wale wanaofuatilia vita hivyo kutoka nje ya nchi.
Kwa nini Kyiv iliamua kufanya shambulio hili la kushtukiza? Hili ni swali ambalo watu wanajiuliza hasa ikizingatiwa kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kuingia karibu kilomita1,000 ndani ya Urusi na takriban wiki moja baadaye, jeshi la Urusi bado linajitahidi kuzuia uvamizi huo. Lengo la operesheni hiyo inaanza kuibuka.
Haya hapa ni maswali matano muhimu kuhusu matukio mapya katika vita vya Ukraine ambayo huenda yakachagiza jinsi mambo yatakavyoendelea katika miezi ijayo.

Nini kilifanyika mjini Kursk?​


Tarehe 6 Agosti vikosi vya Ukraine vilifanya mashambulizi ya kushtukiza katika eneo la Kursk nchini Urisi, linalopakana na Ukraine. Hakuna haarifa za kuaminika kuhusu ukubwa wa shambulio hilo zimekuwa haba.
Hapo awali, ilionekana kuwa operesheni hiyo ilikuwa katika kiwango cha uvamizi wa mara kwa mara wa vikundi vya hujuma vya Urusi, kinyume na serikali ya Vladimir Putin. Walikuwa wamejaribu kuja Urusi kutoka Ukrainia na walionekana kuhusisha mamia ya wafanyakazi wa kabila la Kirusi.

Lakini shambulizi hili la hivi punde liliposonga zaidi katika eneo la Urusi - huku wanablogu wa kijeshi wa Urusi wakiripoti mapigano makali umbali wa kilomita 30 kutoka mpakani na gavana wa eneo la Kursk akimwambia Rais Putin kwamba vijiji 28 vya Urusi viko mikononi mwa Ukraine, ikawa wazi kuwa wanajeshi wa kawaida wa Ukraine walihusika.
Jengo la ghorofa lililoharibiwa huko Kursk, nchini Urusi.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kulingana na mamlaka za mitaa, jengo hili la ghorofa mjini Kursk liliharibiwa kwa kombora lililorushwa na Ukraine.

Inaonekana wakati Urusi ilikuwa inaelekeza nguvu zake za kijeshi katika maeneo kadhaa muhimu ya mstari wa mbele ambapo mapigano yanaendelea kuwa mazito, Ukraine iliamua kuchukua fursa ya mpaka huo uliokuwa na ulinzi mdogo na kuvuka hadi ndani ya Urusi.

Afisa mkuu wa usalama wa Ukraine ambaye jina lake halikutajwa ameliambia shirika la habari la AFP: "Tuko kwenye mashambulizi. Lengo ni kumvuruga adui, kumtia hasara kubwa na kuyumbisha hali ya Urusi kwani hawawezi kulinda mpaka wao wenyewe.
Map, Kursk region


Kwa nini Ukraine ilishambulia Urusi katika eneo la Kursk?​


Mwanzoni Kyiv ilikaa kimya kuhusu shambulio hilo, lakini rais Volodymyr Zelensky alithibitisha uvamizi huo kwa njia isiyo ya moja kwa moja tarehe 10 Agosti.

Alidai kwamba Ukraine iliendelea "kuelekeza vita kwenye eneo la wavamizi". Hakutoa sababu za wazi au malengo ya operesheni hiyo, lakini mnamo Agosti 12 alitangaza kuwa karibu kilomita 1,000 mraba za eneo la Urusi sasa zilikuwa chini ya udhibiti wa Kyiv.

Wachambuzi wa kijeshi na kisiasa wanaojaribu kujibu swali la "kwa nini", wanakubali zaidi kwamba kuvuruga kwa mbinu kunaweza kuwa mojawapo ya malengo makuu ya uvamizi huu.

Kwa miezi kadhaa iliyopita, Ukraine ilijitahidi kuzuia vikosi vya Urusi mashariki mwa Ukraine, ambavyo vimekuwa vikisonga mbele, na kuuteka mji wa kimkakati wa Chasiv Yar mwezi uliopita. Katika maeneo ya kaskazini-mashariki na kusini, hali ni ngumu pia.

Licha ya kuzidiwa nguvu na Urusi katika maeneo mengi ya mstari wa mbele wa kilomita 1,100, mamlaka ya Ukraine iliamua kucheza kamari ili kuunda eneo la mapigano lililo umbali wa mamia ya maili, ili kumfanya mpinzani kutumia rasilimali zake, na kuelekeza shinikizo kutoka mashariki mwa Ukraine. eneo la Kursk nchini Urusi.
Inadaiwa kuwa vikosi vya Ukraine vlilishambulia eneo la mpakani la Kursk, nchini Urusi. Picha kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha hii, iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, inadaiwa inaonyesha vikosi vya Ukraine vikifyatua mizinga katika eneo la mpaka la Kursk

Mtaalamu wa masuala ya usalama profesa Mark Galeotti aliiambia BBC kwamba Ukraine imenaswa katika vita vya uhasama kwa muda wa miezi kadhaa iliyopita, huku kukiwa na harakati kidogo ardhini, sasa inahitajika kupata faida ya hatua yake ya sasa.

Manauchumi huyo, pia alisema hii ilikuwa kamari: "Tulituma vikosi vyetu vilivyokuwa tayari kwa mapigano kwenye sehemu dhaifu zaidi ya mpaka wao". Aliongeza kuwa hatua hiyo imefikia haraka lengo la Kyiv kuliko ilivyotarajia.

"Makamanda wao sio wajinga ... wanaleta vikosi vyao mbele, lakini sio haraka kama tunavyotaka. Wanajua hatuwezi kutanua wigo wetu zaidi ya kilomita 80 au 100.
Vifaru vya Ukraine

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Magari ya kivita ya Ukraine iliyoonekana katika ardhi ya Urusi yana alama nyeupe ya pembetatu, haijawahi kuonekana tena.

Urusi imeitikiaje?​


Vyombo vya propaganda za Urusi ziliandika haraka juhudi za kudhibiti uvamizi wa Ukraine na kuziita "operesheni ya kupambana na ugaidi".

Hadi watu 121,000 wameambiwa kuhama kutoka eneo la Kursk na wengine 11,000 walihamishwa kutoka eneo jirani la Belgorod. Mamlaka ya Urusi ilitangaza hali ya dharura katika eneo hilo na kutoa fidia ya $ 115 kwa wakazi wa eneo hilo.

Mkuu wa Jeshi la Urusi, Jenerali Valery Gerasimov alidai mara kadhaa wiki iliyopita kwamba uvamizi wa Ukraine umesimamishwa, kiuhalisia mambo yalikuwa tofauti.

Jenerali Gerasimov hakuwa katika mkutano wa hivi punde zaidi wa Baraza la Usalama la Urusi, chini ya uenyekiti wa Rais Putin, uliojitolea kusuluhisha mzozo huu. Kwa upande mwingine, mashirika wa karibu wa Putin alikuwepo, mkuu wa huduma ya usalama ya Urusi FSB, Alexander Bortnikov.

Katika taarifa yake ya hivi punde kuhusu matukio hayo, Rais Putin ameishutumu Ukraine kwa kushambulia raia wake na kuahidi "jibu linalostahili".

Profesa Galeotti anasema Ukraine inakabiliwa na hatari ya Urusi kulipiza kisasi kutoka.
"Putin anaweza kuanzisha wimbi lingine la uhamasishaji na kujumuisha askari laki kadhaa kwenye vikosi vyake vya jeshi."

Anaongeza kuwa Urusi inaweza kutafuta njia zingine za kuzidisha mzozo huo. Katika miezi ya hivi karibuni Ukraine imekabiliwa na mashambulizi ya mabomu ya Urusi yaliyolenga miundombinu yake ya nishati. Mapambano yatakayofuata uvamizi huu wa Ukraine yatakuwa makali zaidi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, katika mahojiano ya awali na BBC

Maelezo ya picha, Kwa Rais Zelensky, uvamizi huu ndani ya Urusi unaweza kugeuka kuwa mgumu

Je, mapigano ya Kursk yanamaanisha Ukraine iligeuza mkondo wa vita?​


Hatua ya Ukraine kuvamia Urusi inahitaji ikiwekwa kwenye mizani- huenda taifa hilo lisishangilie mwisho wa mzozo huu hivi karibuni.

Kama anavyosema Mark Galeotti, "ni eneo la takriban maili 50, katika muktadha wa ukubwa wa Urusi na Ukraine, hilo haliwezekani. Lakini athari za kisiasa ni muhimu zaidi.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa Ukraine ilikuwa na nia ya kuonyesha washirika wake wa Magharibi, hususan Marekani hasa, kwamba majeshi yake yana uwezo wa kuendelea na mapigano. Hii pia imeimarisha, angalau kwa muda, nguvu ya mazungumzo ya Kyiv: na askari wao waliopo kilomita 30 ndani ya eneo la Urusi.
Operesheni hiyo pia imebadilisha mtazamo wa vita hivi na kwa Warusi ndani ya nchi - huu sio tena mzozo wa mbali unaoitwa "operesheni maalum ya kijeshi", bali ni mzozo unaowaathiri moja kwa moja.

Mwandishi wa BBC wa Ulaya Mashariki Sara Rainsford anasema: "Ukifuatilia kwa makini baadhi ya ripoti zinazotoka eneo la Kursk, hata kwa kuzingatia mazingira yaliyodhibitiwa ya vyombo vya habari vya Urusi, ni wazi kwamba baadhi yanauliza maswali."
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiongoza mkutano wa Maziri.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Maelezo ya picha, Shinikizo linaongezeka kwa serikali ya Putin

Je, uvamizi huu utaathiri vipi mustakabali wa Zelensky na Putin?​


Kwa viongozi wa Urusi na Ukraine huu ni wakati mahimu wa urais wao.

Kwa Vladimir Putin, kiongozi wa kiimla wa muda mrefu asiyebadilika, ambaye amezoea kutegemea wandani wake hususanwa huduma wa usalama, uvamizi huu unaleta changamoto kubwa. Ni vigumu kubaini kiwango cha majeruhi wa jeshi la Urusi. Kutokana na idadi kubwa ya Warusi (maelfu) na kwamba hatua hiyo haijafikia vita kamili.

Kama anavyosema Mark Galeotti, "kila wakati Kremlin inazidi kuimarisha propaganda."
"Tumeona hili katika vita vya zamani, kutokazama za vita vya Usovieti huko Afghanistan hadi vita vya Urusi huko Chechnya, Kremlin inaweza kudumisha msimamo fulani lakini baada ya muda, ukweli unabainika."
Kwa Volodymyr Zelensky uvamizi nchini Urusi unaweza kugeuka kuwa ngumu sawa, lakini kwa sababu tofauti.
Mchanganuzi Emil Kastehelmi anasema matokeo bora zaidi kwa Ukraine ni kwamba Urusi inaelekeza "rasilimali nyingi kutoka sehemu muhimu zaidi ili kukomboa [eneo la Urusi] lililotekwa."

Kuongeza matumaini ya watu wa Ukraine kwa muda mfupi, kunaweza kusababisha hasara kubwa zaidi katika eneo la mashariki, ambapo mapigano yanaendelea kuwa mazito na baadhi ya wanablogu wa kijeshi wa Urusi wanasifia hatua iliyopigwa, ingawa madai yao hayajathibitishwa kwa sasa.

Profesa Galeotti anasema msukosuko wa sasa katika vita ulihitaji ili kubadili mkondo wa mambo. Matokeo ya mabadiliko hayo hayajakuwa wazi.
 
Putin alipaswa aimarishe ulinzi kwenye mipaka yake sio kuvamia nchi nyingine
Kiwendawazimu tuu
Alijua vita ni kupiga mdomo tu askari wake ata idadi hawana washaenda na maji saiv ana jeshi la kumlinda yeye tu, anategekea North Korea wamuazime jeshi au ama china
 
mi naamini kabisa hao wanajeshi wametumia mbinu za kigaidi kuingia ndani ya mipaka ya urusi kitakachofuata ni kwamba hakuna hata mmoja atakayerejea ukraine...ngoja tusubiri muda ni mwalimu.......
Na Urusi kuvamia Ukraine ambayo ilikuwa haijawahi kurusha hata jiwe Urusi hizo ni mbinu za namna gani
Usichangie tu kishabiki mkuu
Hio ni vita sio mpira
 
Alijua vita ni kupiga mdomo tu askari wake ata idadi hawana washaenda na maji saiv ana jeshi la kumlinda yeye tu, anategekea North Korea wamuazime jeshi au ama china
Wamepata hasara za Mali na uhai wa watu kwa kukutakia tu
Mbaya wanaharibu nchi ya watu iliyojengwa kwa gharama kubwa alafu wanataka hao hao wananchi wawatawale
 
Putin alipaswa aimarishe ulinzi kwenye mipaka yake sio kuvamia nchi nyingine
Kiwendawazimu tuu
Karibu nusu ya Ukraine iko chini ya Russia na Ukraine haijafanikiwa kurudisha hata 1km ya eneo lake unadhani kazi iliyoko kule ni ndogo! Usipende kushabikia vita. Russia ni taifa lenye nguvu sana na hakuna anayependa Russia ije iiharibu Ukraine kabisa.
 
Bring news from your source
Even your phone and freedom of speech is western technology
I don't trust Western media at all. Most of the smartphones are under the tag of “Made In China”.
The famous iPhone is one of them
In western countries, "freedom of speech" refers to the freedom of the ruling class and capitalist interest groups, rather than the freedom of ordinary people.

Even if ordinary people can have some right to speak, it is just to decorate the facade of the power of capital. Anyway, no one cares how much people say, and such freedom is just a placebo to fool the ordinary people.
 
I don't trust Western media at all. Most of the smartphones are under the tag of “Made In China”.
The famous iPhone is one of them
In western countries, "freedom of speech" refers to the freedom of the ruling class and capitalist interest groups, rather than the freedom of ordinary people.

Even if ordinary people can have some right to speak, it is just to decorate the facade of the power of capital. Anyway, no one cares how much people say, and such freedom is just a placebo to fool the ordinary people.
China was aamong of country
Copy and paste tech from the western county

The advantage of china in production is just a cheap labour and population which increase size of market
That why western company invest in china
 
I don't trust Western media at all. Most of the smartphones are under the tag of “Made In China”.
The famous iPhone is one of them
In western countries, "freedom of speech" refers to the freedom of the ruling class and capitalist interest groups, rather than the freedom of ordinary people.

Even if ordinary people can have some right to speak, it is just to decorate the facade of the power of capital. Anyway, no one cares how much people say, and such freedom is just a placebo to fool the ordinary people.
China copy and the original tech or foundation of tech from western
 
Karibu nusu ya Ukraine iko chini ya Russia na Ukraine haijafanikiwa kurudisha hata 1km ya eneo lake unadhani kazi iliyoko kule ni ndogo! Usipende kushabikia vita. Russia ni taifa lenye nguvu sana na hakuna anayependa Russia ije iiharibu Ukraine kabisa.
Tuonyeshe hiyo nusu.Kama si msaada wa separist Russia angegongwa mapema.Sehemu aliyoteka amesaidiwa na mamluki wa Wegner lakini Mrusi yeye binafsi Hana mbinu zaidi kuharibu kila kilicho cha raia.Kuna nusu hapo?
 

Attachments

  • Screenshot_20240813-230948.png
    Screenshot_20240813-230948.png
    471.9 KB · Views: 8
Tangu mwanzo wa vita wengi walitarajia Urusi kuvamia Ukraine na kuteka yote NDANI Ya muda mfupi Sana
Na pengine kumfurusha Zelensky Kama sio kumuangamiza kabisa

Lakini Cha ajabu huu ni mwaka wa pili Urusi inapambana na Ukraine
Huu ni ushindi mkubwa kwa ukraine

Lakini Cha ajabu Leo wamevamia Eneo la Urusi na kuliteka
Pamoja na kwamba Urusi atatumia nguvu kubwa Sana kumuondoa Kama baba baunsa anavyofanya akiona mtoto mdogo anaelekea kumzidi maarifa ya mapigano

Ukraine kuendelea kuilinda serikali yake isipinduliwe mpaka Leo na nchi iliyojitapa ni super power ni ushindi mkubwa
Binadamu kula Samaki si issue ila Samaki akila Mtu ni Issue
 
Tuonyeshe hiyo nusu.Kama si msaada wa separist Russia angegongwa mapema.Sehemu aliyoteka amesaidiwa na mamluki wa Wegner lakini Mrusi yeye binafsi Hana mbinu zaidi kuharibu kila kilicho cha raia
Wagner ndio warusi wenyewe. Huko kuharibu ndio kazi ya jeshi na ndio mbinu mojawapo. Unaposema Russia hawana mbinu, hao Wagner nani aliwapa mafunzo ya kijeshi?
 
Back
Top Bottom