Urusi kuwa na mji wa Bakhmut na Soledar, hasara ni kubwa kuliko faida

Wabongo mna shida sana.
Unaulizwa maswali unashindwa kuyajibu na badala yake unapiga blablaa ambazo ni tofauti na ulichoulizwa. Si bora ungeuchuna tu ungeepuka aibu ya kukosa hoja.
Ombea amani na usalama wa dunia. Huna maswali ya msingi. Yote uliyouliza ni mepesi na inaonyesha kuna vitu huvijui. Amani amani. 🙏🙏🙏
 
Unapoingia vitani huendi kufanya mzaha, hasa vita unayojua ni kwa uhai wa nchi yako, tofauti kabisa na kwenda kutalii kule kwa akina Taliban.
Hahahahaaah ndo maana wanaitaga Tour, 'I had a tour in Iraq and Afghanstan' utawaskia.

Linganisha na kauli nzito ilobeba mamlaka 'We are conducting a special Military operesheni in Ukraine'
 
Lini Putin alitamka hilo? Hebu tutajie tu siku na tarehe aliyotamka hilo
Lengo la putini ni kurudisha ukreni yote iwe ya urusi na ndo lengo na alishasema yeye ni peter the great.
Na bdo anataka moldova pia.

Romania na poland wangekuwa sio ndani ya NATO nao yangewakuta.
 
Kwa mfuatiliaji mzuri wa vita hii, nadhani aliisikia ile kauli kuwa wataivuta vita hii kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana mpaka watakapohakikisha Urusi siyo tishio tena kwa Taifa lolote.

Ushindi kwa nchi za Magharibi dhidi ya Urusi, wala siyo kuikomboa Bakhmut bali ni kuifanya Urusi imalize resources zake zote kwenye vita. Na baada ya hapo iwe Taifa dhaifu ambalo halitaweza kuwa tishio kwa usalama wa mataifa jirani, na wala asiwe na uwezo ya kusaidia tawala za kidikteta Duniani.

Hiyo ndiyo sababu ya kauli inayorudiwa mara kwa mara, 'tutaendelea kuisaidia na kuiunga mkono Ukraine bila ya kujali vita itachukua muda mrefu kiasi gani'.

Na sasa hivi, tayari uchumi wa Urusi umeanza kuyumba, sarafu inaanguka, mauzo ya mafuta na gas yanashuka, na India ambaye ni mnunuzi mkuu wa mafuta ya Russia amepewa onyo kuwa kama ataendelea kununua mafuta ya Russia, hataruhusiwa kuuza bidhaa yoyote inayotokana na mafuta kwa nchi za Magharibi. Vijana, hasa wataalam wa fani mbalimbali wanazidi kuikimbia Russia wakuenda nchi za Magharibi.
 
Nadhani ungefatilia usingeuliza hili la ukreni kupiga urusi
Kama angeruhusiwa hata urusi ingekuwa na maumivu mabaya ila wanazuiwa sana na mghalibi na ndo maana siraha za maghalibi hazitakiwi kurushwa urusi kwa kuwa wanajua urusi itasikia maumivu na kuamua kutumia nyukria kwa kisingizio cha maghalibi.

Urusi ki ujumla vita imemshinda maana amepigana na watu ambao wana siraha za kiwango cha chini ili hali yeye anatumia vyanzo vyake vyote vyenye uwezo mkubwa.
 
Nadhani huyo Covax siyo mfuatliaji mzuri wa hiyo vita. Vifo vya askari wa Urusi ni vingi sana, na hiyo siyo kwa hisia bali kwa uthibitisho toka upabde wa Russia. Hata mkuu wa Wagner aliongea akiwa amesimama katikati ya maelfu ya majeneza ya askari waliokufa vitani akilalamika kuwa askari wake wamekuwa wanakufa kwa maelfu kutokana na kutokuwa na silaha za kutosha. Akatishia hata kuwaondoa askari waliobakia hai.
 
Ukraine hawana chaguo jingine zaidi ya kupigana. Huwezi kuuliza eti wanapata faida gani!! Adui ameingia nchini kwao ametwaa maeneo, utakaa kimya?

Kwa upabde wa NATO, kumbuka kuna mataifa wanachama wa NATO yaliyokuwa sehemu ya USSR ambayo tayari yalikwishatishiwa na Russia, nayo kuvamiwa. Kama Russia angefanikiwa alichokitaka kwa Ukraine, next yangekuwa ni hayo mataifa. Mataifa haya yanaiona Ukraine inapigana kwa niaba ya mataifa yao pia.
 
Upo wrong kabisa. Fuatilia historia ya mgogoro kuanzia 2014.
 
Urusi atashinda vita hii hata Nato waje na propaganda zipi hawataweza kumshinda Urusi
Kushinda vita ingekuwa ni rahisi kama hii kauli yako, Urusi ingekuwa aliishaikamata Ukraine ndanibya masaa 72 kama alivyotamka Putin.
 
Urusi hana sabau wala nia ya "kuichukua Ukraine yote", kwa hiyo hapa ndipo uchambuzi wako unapoonyesha udhaifu wake na katika mambo mengine uliyoyataja kwenye mada yako.

Sitayaghusa hayo mengine na kuyapa ufafanuzi kwa sasa hivi.
Kama mleta mada ni dhaifu, wewe utakuwa ni dhaifu mara 4 yake.

Mashambulizi ya mwanzo ya Russia yalikuwa wapi? Kwa kushambulia mji mkuu wa Ukraine, alilenga kitu gani? Ukijibu maswali hayo mawili itajulikana kama unaujua huo mgogoro au unausikia juu juu tu.
 
Mkuu umeanza mada vizuri sana kuelezea umuhimu wa Bakhmurt kwa ufasaha kabisa.

Lakini maswali yako yanajijibu yenyewe kwenye hoja yako.

Kwenye swali 1, nguvu kubwa sio kumiliki eneo bali kukalia eneo ili kuwezesha operation kwenye mingine. Hii sio kwa Urusi tu hata Ukraine imefanya hivyo kwa kujua kuippteza Bakhmurt ni kupoteza maeneo mengi yanayolindwa strategically na Bakhmurt. Ni kama hapa Tanzania poppte unapoona kuna kambi ya jeshi hilo eneo ni mahsusi kulinda maeneo fulani nyeti.

Swali 2: swali lina ukakasi kwa maana umeifanya Urusi kwa miazi 15 imechukua mile 59. Hii si kweli chukua eneo lote la Ukraine lilichukuliwa gawanya na miezi ndio ujue kwa kipindi chote amefanikiwa kwa kiasi gani kwa siku, week, Mwezi au miezi 15. Ni kweli maeneo hayo mawili yalikua na ugumu sana kwa sababu tu ya unyeti wake.

USA amepigana miaka 11 huko Afganistan lakini alishindwa kuyafikia baadha ya maeneo na ndio maana siku tatu tu US walipotangaza kuondoka wenyewe walichukua nchi yao na vifaa vita vyote vya kijeshi vya US vilichukuliwa. Nimekupa huu mfano utambue ugumu wa kufika baadhi ya strategic area au umuhimu wa kuwa na stratevic position over your opponent.

Swali 3:Umelijibu katika maelezo yako kwamba kuanguka kwa Bakhmurt kunaongeza urahisi wa usafirishaji wa vifaa na wapiganaji na kurahisisha kuvamia maeneo mengine. Ingawa lengo la Urusi sio kukalia maeneo ya Ukrain bali kuondoa silaza zote za NATO, kuifanya Ukraine isiingie NATO, na kuondoa element zote za kinazi.

Swali 4 n 5, yanashabihiana. Umetoa mfano wa Kakhiv na kwengine waliwithdraw ndio kwa sababu ya risk kubwa iliyokuwepo ya kubomoa dam na kuvunja Daraja na kugawa wanajeshi waliopo ngambo ambapo wangekosa namna ya kupata msaada wa haraka wa vifaa na hata wapogananaji busara ikaonekana warudi nyuma hadi ngambo ya mto. Sambamba na hilo hata walichokuwa wanataka kukilinda hakipo eneo husika wakarudi nyuma kulinda askari na vifaa badala vipelekwe sehemu yenye uhitaji.

Kumbuka Ukraine anapigana na kikundi cha mgambo well trained Wagner, hawana ndege, hawana air power vyote vipo kwenye jeshi la Urusi. Unawezaje kuhoji uwezo wa Jeshi la Urusi kushilikia eneo husika kama Wagnerwataenda mapumziko.

Tutapata taarifa ya raia wa nchi ngapi wamehusika kupigania Bakhmurt upande wa Ukraine soon tutapata taaifa na wangapi walikuwa neutralized
 
Una flaws nyingi kwenye andiko lako:
1. Unaongelea ukubwa wa gharama ila hauzitaji.
2. Umeweka baadhi ya namba ila hujaweka Source.
3. Hebu jiridhishe hapo kwenye 'SQM'. Unajua Heka Moja ya shamba Ina SQM 70?
 
Ukweli ni Urusi yupo Ukraine kwa miezi kibao sasa na Uongo ni Ukraine kudai atawapiga Urusi licha ya kupata misaada mingi tokea NATO
Hebu tutajie misaada ambayo Ukraine amepata kutoka NATO ni ipi na ni lini
 
Afadhali umemjibu na hiyo no.2
Kwa maelezo yake ana amini kwakuwa eneo lenye ukubwa fulani, limetekwa kwa muda fulani basi na eneo lililobaki litatekwa kwa proportional hiyo hiyo.
Kwakua mpaka dakika ya 15 tumeshashinda goli moja basi ikifika dakika 90 tutakuwa tumeshapata magoli 6.
Mpaka HT watujaruhusu goli, basi hadi kipenga cha mwisho hatutakua tumefungwa.
Ameathiriwa sana na Somo la physics.
 

Youn have a point. Kwamba;
1. Bakhmut imetumika kama trapping position kwa Russia ndo maana akapeleka resources kubwa. Matokeo yake kapoteza wanajeshi wengi na vifaa vingi (Heavily inflicted) with small gain. Ni njia ya ku drain resources zake. Kwenye hilo kuna hoja.

2. USA, German and allies wana prolong vita kwa lengo la kumdhoofisha Russia na kujua uwezo wake unakoishia ili mwisho wa siku asiwe na madhara kwa nchi zingine. Hiyo ni hoja ya msingi ina mashiko.

3. Russia anazoofishwa kiuchumi. Uchumi wake unazidi kusinyaa. Vita ikiendelea atashindwa kui finance na hataweza kushinda hii vita.
 
Wewe tumainie una uandishi fulani wa kiboya sana. Eti unasema "kuna siri siwezi kuziandika hapa" !! Una siri gani wewe mlamba makombo wa Sukuma Gang?
 
Hapo kwenye SQM uko sahihi kweli!!!?? Yaani mji uwe na SQM 53!!!???
 
Sitaki kuamini kuwa unamaanisha ulichoandika! Kama unamaanisha basi pole sana, ujinga ni mzigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…