- Thread starter
- #61
Ukraine hawana chaguo jingine zaidi ya kupigana. Huwezi kuuliza eti wanapata faida gani!! Adui ameingia nchini kwao ametwaa maeneo, utakaa kimya?
Kwa upabde wa NATO, kumbuka kuna mataifa wanachama wa NATO yaliyokuwa sehemu ya USSR ambayo tayari yalikwishatishiwa na Russia, nayo kuvamiwa. Kama Russia angefanikiwa alichokitaka kwa Ukraine, next yangekuwa ni hayo mataifa. Mataifa haya yanaiona Ukraine inapigana kwa niaba ya mataifa yao pia.
Wachangiaji na Pro Russia wengi wanashindwa kuelewa dhana hii kuhusu NATO na ushiriki wa nchi zilizojiunga NATO kuisaidia Ukraine.
NATO ni entity inayojitegema na ina resources zake (Financing, Military equipment na Human resources). Inachangiwa financing na wanachama wake tu. Inanunua vifaa vya kivita kwa mahitaji yake kwa technology inayoitaka kwa mazingira ua wakati husika. Siyo kwamba inapewa donation ya silaha kama nchi zinavyofanya kwa Ukraine la hasha.
Watu wengi wanafikiri USA, German, UK and allies kuisaidia kifedha, kujenga uwezo na vifaa vya kivita Ukraine kuwa ndo NATO anapigana na Russia. Hakuna kitu Russia anachokiogopa kama akiingia battle direct na NATO, hiyo mistake Russia hatakuja aifanye maana anajua hatachukia round. Russia anajua High precision equipment with high technology millitary equipments anazotumia NATO. Hakuna military equipment ambayo NATO anazitumie zimeenda Ukraine. Hata USA, German vifaa anavyotoa vina technology ya chini kuliko anavyotumia NATO.
Ushiriki wa NATO ni kutoa wataalam wa kuwafundisha Wanajeshi wa Ukraine kwenye vifaa vinavyotolewa kwa Ukraine maana yeye NATO amevitumia sana siku za nyuma ana uzoefu mkubwa sana kuhusu hivo vifaa. Pia kuwapa military tactical. Lakini siyo kwamba NATO anapeleka majeshi yake au vifaa vyake kwa Ukraine.