Hiyo ilikuwa ni mbinu ya kudhoofisha, asithubutu kuweka upinzani huko kunakotakiwa; hili nalo wewe huna akili ya kulitambua?
Toka mwanzo, lengo la Urusi lilifahamika ni eneo gani alilenga, lakini kwa watu kama wewe, ninayejua sababu zako za kufifisha akili, unajilazimisha iwe kama unavyota ionekane kuwa ndivyo.
Eneo la Mashariki mwa Ukraine na Crimea, ni maeneo ambayo siku zote Mrusi ana 'interest' nayo. Watu wa maeneo hayo wana asili ya Urusi.
Kabla ya hii vita aliyoingia, tayari kulikuwepo na mapigano kati ya vikosi vya Ukraine na waasi wa maeneo hayo; wewe haya huyajui, lakini unajidai hapa kuwa mjuaji kuliko wengine!
Rafiki yangu Kalamu, kwenye mambo mengi huwa una ufahamu wa kutosha ila kwenye hili inaonekana ni mtupu kabisa. Nenda kachimbue chanzo cha mgogoro. Nitakupa hints kidogo:
Russia haikutaka kabisa USSR ife. Lakini hali mbaya ya uchumi, kuongezeka kwa matendo ya kuihujumu serikali, upinzani mkubwa wa ndani dhidi ya Serikali, ni hali zilizojitokeza sana mwishoni mwa miaka ya 1980. Hali hizo ikailazimu USSR kutafuta urafiki na mataifa ya Magharibi. Urafiki na nchi za magharibi ulipojengeka, USSR ikaomba msaada wa kifedha kutoka nchi za magharibi ili kunusuru uchumi wake. Mataifa ya Magharibi yakaipa masharti USSR, mojawapo ni kuheshimu demokrasia na haki za watu. Na hapo kwenye demokrasia USSR ilitakiwa kuyaachia uhuru wa kuamua mataifa yale aliyokuwa akiyashikilia kwa nguvu, mojawapo Ukraine, yaseme kama yanataka kuendelea kuwa kwenye USSR. Mataifa 14, Estonia, Latvia, Lithuania, Armenia, Georgia, Moldova, Ukraine, Azerbaijan, Belarus, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan, na Uzbekistan, yaliyokuwa yanaunda USSR, yote yakaamua kuwa mataifa huru.
Mwaka 1991, USSR ikavunjika rasmi, na mwaka huo huo, Urusi ikamiminiwa misaada toka nchi za Magharibi, na ikafungua milango kwa mataifa ya magharibi kwenda kuwekeza Urusi. Mpaka mwaka 2020, kulikuwa na makampuni zaidi ya 3,000 kutoka nchini za magharibi nchini Russia.
Lakini Urusi, haikuwa imependezwa na mataifa haya yaliyokuwa sehemu ya Urusi, kujitenga moja kwa moja na Urusi, iliyataka yaendelee kuwa tegemezi kwa Urusi katika maamuzi.
Njia mojawapo ambayo Urusi ilihakikisha kuwa hilo linatokea na kuendelea kuwepo ni kuhakikisha marais wote katika nchi hizi wanakuwa watu ambao Urusi inawakubali. Hivyo mataifa haya mapya yakawa na marais vibaraka wa Urusi. Baadhi ya hayo mataifa, taratibu, kutokana na nguvu za wananchi, yakajitenga kabisa na Urusi na kujiunga na EEC. Nchi iliyokuwa ina nguvu na ambayo Urusi iliwekeza nguvu nyingi kuhakikisha inaendelea kuwekea serikali kibaraka cha Kremlin ikawa ni Ukraine. Lakini mwaka 2014, wananchi walichachamaa na kufanya maandamano makubwa, na Rais wa wakati huo Victor Yanukovych, alisalimu amri na kukimbia nchi. Baada ya Rais huyu kibaraka wa Urusi kutimliwa, Urusi ikaona wazi kuwa sasa haina maamuzi tena juu ya Ukraine. Ikaanza kuwatumia watu wa mpakani wanaoongea kirusi kuipinga Serikali yao ya Kiev. Urusi ikawa inawapa hawa wapinzani iliowatengeneza silaha na fedha kugharamia vita yao dhidi ya Serikali.
Wapinzani wa Serikali waliotengenezwa na Urusi, walipoonekana kuelemewa katika vita, ndipo Urusi ikaingia vitani moja jwa moja kwa madai inaenda kuokoa maisha ya wale wapinzani wa Serikali iliokuwa imewatengeneza. Na katika vita hivyo ndipo ilipoimega sehemu ya Ukraine, jimbo lote la Cremia. Hata hivyo Urusi wakati wote haikutulia, lengo likiwa kuhakikisha Ukraine lazima irudi kwenye utawala unaotengenezwa Russia.
Ukraine, wananchi wake walivyokuwa wakishuhudia chokochoko za Urusi kwa kupitia wapinzani wanaotengenezwa, wakawa wanaisukuma sana nchi yao kujiunga na NATO ili kupata ulinzi dhidi ya Russia. Kabla ya hilo halijatokea, Urusi ikaona njia pekee ya kuhakikisha hilo halitokei ni kuiangusha Serikali ya Ukraine na kusimika serikali mpya itakayopokea maelekezo toka Kremlin. Maandalizi ya kabla ya hilo kutokea ilihusisha kuwaandaa wananchi kuichukia Serikali iliyokuwepo ili wanajeshi wa Urusi watakapovamia Kiev, waonekane ni wakombozi. Vibaraka waliokuwa wanatumika na Urusi wakamhakikishia Putin kuwa wananchi wengi wa Ukraine hawaitaki kabisa Serikali iliyopo. Ndipo ikaandaliwa operation maalum ambayo lengo lilikuwa kuiondoa Serikali iliyopo, na watu watatu wakuu wa Serikali, akiwemo Rais walitakiwa kuuawa.
Jambo ambalo hawakulitegemea likatokea, wananchi hawakuwataka kabisa askari wa Urusi na wakaungana na askari wa serikali kuwaua askari wa Urusi. Kwa sababu Urusi haikujiandaa kwa hilo, ikabidi waikimbie Kiev, na kwenda mashariki mwa nchi ambako ndiko waliko wale wapinzani waliowatengeneza. Na ndiko waliko mpaka keo.
Kwa hiyo lengo la Urusi kuivamia Kiev ilikuwa ni kuiangusha Serikali ili isimikwe Serikali ambayo itapokea maelekezo toka Kremlin.
Maelezo haya mafupi, nadhani bwana Kalamu yatakupa mwanga kidogo.