Urusi na China; Kuanguka kwa Dola na kuinuka kwa Yuan

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
URUSI NA CHINA;KUANGUKA KWA DOLA NA KUINUKA KWA YUAN.

Leo 14:30pm 06/03/2022

Rais wa Urusi,Vladimir Putin hakuivamia Ukraine bila mipango (kwa bahati mbaya),Urusi haifanyi kitu chochote bila mipango,Urusi na China wameisubiri siku hii kwa muda mrefu na sasa wameipata fursa adimu ya kuiangusha dola,tarehe 24/02/2022 haikuwa siku ya bahati mbaya kwa Urusi kuivamia Ukraine,Urusi ilitoa tahadhari mapema ya kwamba NATO kujitanua ndani ya Ukraine ni mstari mwekundu usiovumilika kwa Urusi,

Urusi na China zilitambua kuivamia Ukraine hakuzuiliki na itasababisha vikwazo kama kutolewa kwenye mfumo wa kuhamisha dola kupitia Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunications (SWIFT system) na vikwazo vya kiuchumi,hivyo basi Urusi na China wamejiandaa kwa jawabu la tatizo hilo kwa miaka mingi wakisubiri siku hiyo swift system itakapofungwa kwa wao kukatazwa kuitumia,China na Urusi wanayo Yuan-Ruble system,Kwa ufupi wapo Waafrika waliojaribu kuupinga mfumo wa malipo ya dola hata kuuliza kwa nini dola zichapishwe tu na nchi nyingine ziwe zinaomba kibali kuchapisha pesa zao,kwa nini tusitumie Dhahabu kama mfumo wa malipo ya Kimataifa badala ya kutumia dola tu.

-Kampuni zilizokodisha ndege Urusi kulipwa kwa pesa ya China,Yuan.

Makampuni ya ndege ya Ulaya mfano Boeing wameikodishia Urusi ndege zaidi ya 500 na makampuni hayo yanategemea Urusi iwalipe ili yaweze kuendelea na shughuli zake,Urusi ipo tayari kulipa fedha hizo lakini tatizo Urusi imefungiwa kulipa dola kwa mfumo wa SWIFT,kwa maana hiyo mfumo uliopo ni wa YUAN,hivyo basi Urusi inaweza kulipa kwa mfumo wa YUAN! Je makampuni hayo ya Ulaya yatakataa kulipwa kwa kutumia YUAN!? basi wazichukue ndege zao lakini je zitapita katika anga lipi wakati Mrusi kafunga anga lote la Soviet Union,je makampuni mengine hayakuja kumkodishia ndege mrusi kwa malipo ya YUAN!? tuendelee kunywa supu nyama tutazikuta chini.

-Urusi kufunga bomba lake la Mafuta na Gesi.

Baada ya kuivamia Ukraine,ikiwa na maana Urusi kuivamia NATO,ama kwa namna nyingine nchi zinazotegemea mafuta na Gesi ya Mrusi kuisaidia Ukraine basi Mrusi amefunga bomba lake la Mafuta na Gesi,Je kufungwa kwa bomba la Mafuta na Gesi kutaiathiri Urusi,jibu ni hapana,Mrusi amejiandaa kwa miaka kusubiri siku hii adimu ya yeye kuwafungia mafuta na Gesi mataifa ya Ulaya,Kwa taarifa tu Urusi imekuwa ikiweka akiba ya dhahabu na akiba ya pesa ya Yuan kwa muda mrefu,hivyo basi Urusi ina akiba kubwa ya Yuan na Dhahabu kiasi cha kutotikiswa kwa namna yoyote ile na kukosa pesa ya mafuta na Gesi kutoka nchi za Ulaya,kukosekana kwa mafuta na Gesi katika nchi za Ulaya kutasababisha bei ya gesi na mafuta kupanda kwa nchi za Ulaya hivyo basi kusababisha kuyumba kwa upatikanaji wa dola,kusababisha mfumuko wa dola katika mfumo wa kifedha (Monetary system).

-Kufungua bomba la Mafuta na Gesi kwa malipo ya Yuan na sio dola tena.

Kwa miaka mingi Urusi na China imekuwa ikiisubiri siku hii,kutumia dhahabu kama mfumo wa malipo na kuutokomeza mfumo wa SWIFT unaotumia dola,nakumbuka Rais Magufuli alikuwa na ndoto hizi za kutumia rasilimali zetu na aliagiza benki kuu yetu iwe na akiba ya kutosha ya dola,Vita ya Urusi na Ukraine umefikia lengo la kuitokomeza dola,Urusi sasa inaweza kutangaza kutotumia tena mfumo wa kuhamisha dola kwa SWIFT,Urusi sasa inaweza kusema tutafungua mabomba ya mafuta na Gesi kwa malipo ya pesa ya China ya YUAN tu.Kwa yeyote mwenye kutaka mafuta ya Urusi au Gesi ya Urusi basi alipe kwa dhahabu au atumie mfumo wa ruble-yuan gold payment system,asiyetaka atakufa na baridi kwa kukosa gesi kuleta joto nyumbani na watakufa na njaa kwa kupungua uzalishwaji wa ngano katika bara la Ulaya.

-China yupo upande gani kwenye mgogoro wa Urusi na Ukraine.

Nani yupo kimya pasipo kusema lolote kwenye mgogoro wa Urusi na China!? Kimya wanasema kinamaanisha ndio,China hamtupi ndugu yake,atampa mkono rafiki "strategic partner" kwenye suala la Mafuta,Gesi na Kilimo cha ngano,mfumo wa Yuan-Ruble utaanza rasmi na kusaidiana na mfumo wa malipo ya dhahabu,kufikia hapa Vladimir Putin atahitimisha rasmi mfumo wa Petro-Dollar yaani malipo ya Dola kwenye soko la mafuta kwa kukasimiwa,kukaimiwa ama kuchukuliwa na mfumo Yuan-Ruble,Hivyo basi NATO wasahau kumtoa Putin kwa urahisi kama walivyomtoa Charles De Gaulle au Gaddafi baada ya kuchallenge Petro-Dollar system.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
URUSI NA CHINA;KUANGUKA KWA DOLA NA KUINUKA KWA YUAN.

Leo 14:30pm 06/03/2022

Rais wa Urusi,Vladimir Putin hakuivamia Ukraine bila mipango (kwa bahati mbaya),Urusi haifanyi kitu chochote bila mipango,Urusi na China wameisubiri siku hii kwa muda mrefu na sasa wameipata fursa adimu ya kuiangusha dola,tarehe 24/02/2022 haikuwa siku ya bahati mbaya kwa Urusi kuivamia Ukraine,Urusi ilitoa tahadhari mapema ya kwamba NATO kujitanua ndani ya Ukraine ni mstari mwekundu usiovumilika kwa Urusi,

Urusi na China zilitambua kuivamia Ukraine hakuzuiliki na itasababisha vikwazo kama kutolewa kwenye mfumo wa kuhamisha dola kupitia Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunications (SWIFT system) na vikwazo vya kiuchumi,hivyo basi Urusi na China wamejiandaa kwa jawabu la tatizo hilo kwa miaka mingi wakisubiri siku hiyo swift system itakapofungwa kwa wao kukatazwa kuitumia,China na Urusi wanayo Yuan-Ruble system,Kwa ufupi wapo Waafrika waliojaribu kuupinga mfumo wa malipo ya dola hata kuuliza kwa nini dola zichapishwe tu na nchi nyingine ziwe zinaomba kibali kuchapisha pesa zao,kwa nini tusitumie Dhahabu kama mfumo wa malipo ya Kimataifa badala ya kutumia dola tu.

-Kampuni zilizokodisha ndege Urusi kulipwa kwa pesa ya China,Yuan.

Makampuni ya ndege ya Ulaya mfano Boeing wameikodishia Urusi ndege zaidi ya 500 na makampuni hayo yanategemea Urusi iwalipe ili yaweze kuendelea na shughuli zake,Urusi ipo tayari kulipa fedha hizo lakini tatizo Urusi imefungiwa kulipa dola kwa mfumo wa SWIFT,kwa maana hiyo mfumo uliopo ni wa YUAN,hivyo basi Urusi inaweza kulipa kwa mfumo wa YUAN! Je makampuni hayo ya Ulaya yatakataa kulipwa kwa kutumia YUAN!? basi wazichukue ndege zao lakini je zitapita katika anga lipi wakati Mrusi kafunga anga lote la Soviet Union,je makampuni mengine hayakuja kumkodishia ndege mrusi kwa malipo ya YUAN!? tuendelee kunywa supu nyama tutazikuta chini.

-Urusi kufunga bomba lake la Mafuta na Gesi.

Baada ya kuivamia Ukraine,ikiwa na maana Urusi kuivamia NATO,ama kwa namna nyingine nchi zinazotegemea mafuta na Gesi ya Mrusi kuisaidia Ukraine basi Mrusi amefunga bomba lake la Mafuta na Gesi,Je kufungwa kwa bomba la Mafuta na Gesi kutaiathiri Urusi,jibu ni hapana,Mrusi amejiandaa kwa miaka kusubiri siku hii adimu ya yeye kuwafungia mafuta na Gesi mataifa ya Ulaya,Kwa taarifa tu Urusi imekuwa ikiweka akiba ya dhahabu na akiba ya pesa ya Yuan kwa muda mrefu,hivyo basi Urusi ina akiba kubwa ya Yuan na Dhahabu kiasi cha kutotikiswa kwa namna yoyote ile na kukosa pesa ya mafuta na Gesi kutoka nchi za Ulaya,kukosekana kwa mafuta na Gesi katika nchi za Ulaya kutasababisha bei ya gesi na mafuta kupanda kwa nchi za Ulaya hivyo basi kusababisha kuyumba kwa upatikanaji wa dola,kusababisha mfumuko wa dola katika mfumo wa kifedha (Monetary system).

-Kufungua bomba la Mafuta na Gesi kwa malipo ya Yuan na sio dola tena.

Kwa miaka mingi Urusi na China imekuwa ikiisubiri siku hii,kutumia dhahabu kama mfumo wa malipo na kuutokomeza mfumo wa SWIFT unaotumia dola,nakumbuka Rais Magufuli alikuwa na ndoto hizi za kutumia rasilimali zetu na aliagiza benki kuu yetu iwe na akiba ya kutosha ya dhahabu,Vita ya Urusi na Ukraine umefikia lengo la kuitokomeza dola,Urusi sasa inaweza kutangaza kutotumia tena mfumo wa kuhamisha dola kwa SWIFT,Urusi sasa inaweza kusema tutafungua mabomba ya mafuta na Gesi kwa malipo ya pesa ya China ya YUAN tu.Kwa yeyote mwenye kutaka mafuta ya Urusi au Gesi ya Urusi basi alipe kwa dhahabu au atumie mfumo wa ruble-yuan gold payment system,asiyetaka atakufa na baridi kwa kukosa gesi kuleta joto nyumbani na watakufa na njaa kwa kupungua uzalishwaji wa ngano katika bara la Ulaya.

Nimesoma kichwa cha habari tu, COW BOY aka Mnyamwezi yupo toka WW1 na WW2 na zote ameshiriki ipasavyo...ila bado anakamata usukani.... Mabepari walishaseti misingi ya kuishi na kuishika dunia..

Movement za China wanazijua na kuzibalance vizuri sana, Mrusi ameshafanyiwa tathmini na pale Ukraine ni chambo tu kile kuliangusha Taifa la Urusi jumla jumla na kummaliza kabisa Putin.

Europe na USA tayari wanabudget ya shughuli yote ya ukraine bila kuyumbisha chumi zao na mwisho wa siku raia wa Urusi wataiangusha serikali yao wenyewe kwa njaa...
 
aise ,ikiwa itakuwa ni hivyo kazi na kimbembe kitakuja kwetu sisi wadanganyika,ambao dhabu machimbo yapo kwetu lkn dhahabu hatuna akiba yoyote,hiyo dhahabu ya kulipia mafuta tutaipata wapi!? twafaa ,twafaa jamani[emoji24]
 
URUSI NA CHINA;KUANGUKA KWA DOLA NA KUINUKA KWA YUAN.

Leo 14:30pm 06/03/2022

Rais wa Urusi,Vladimir Putin hakuivamia Ukraine bila mipango (kwa bahati mbaya),Urusi haifanyi kitu chochote bila mipango,Urusi na China wameisubiri siku hii kwa muda mrefu na sasa wameipata fursa adimu ya kuiangusha dola,tarehe 24/02/2022 haikuwa siku ya bahati mbaya kwa Urusi kuivamia Ukraine,Urusi ilitoa tahadhari mapema ya kwamba NATO kujitanua ndani ya Ukraine ni mstari mwekundu usiovumilika kwa Urusi,

Urusi na China zilitambua kuivamia Ukraine hakuzuiliki na itasababisha vikwazo kama kutolewa kwenye mfumo wa kuhamisha dola kupitia Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunications (SWIFT system) na vikwazo vya kiuchumi,hivyo basi Urusi na China wamejiandaa kwa jawabu la tatizo hilo kwa miaka mingi wakisubiri siku hiyo swift system itakapofungwa kwa wao kukatazwa kuitumia,China na Urusi wanayo Yuan-Ruble system,Kwa ufupi wapo Waafrika waliojaribu kuupinga mfumo wa malipo ya dola hata kuuliza kwa nini dola zichapishwe tu na nchi nyingine ziwe zinaomba kibali kuchapisha pesa zao,kwa nini tusitumie Dhahabu kama mfumo wa malipo ya Kimataifa badala ya kutumia dola tu.

-Kampuni zilizokodisha ndege Urusi kulipwa kwa pesa ya China,Yuan.

Makampuni ya ndege ya Ulaya mfano Boeing wameikodishia Urusi ndege zaidi ya 500 na makampuni hayo yanategemea Urusi iwalipe ili yaweze kuendelea na shughuli zake,Urusi ipo tayari kulipa fedha hizo lakini tatizo Urusi imefungiwa kulipa dola kwa mfumo wa SWIFT,kwa maana hiyo mfumo uliopo ni wa YUAN,hivyo basi Urusi inaweza kulipa kwa mfumo wa YUAN! Je makampuni hayo ya Ulaya yatakataa kulipwa kwa kutumia YUAN!? basi wazichukue ndege zao lakini je zitapita katika anga lipi wakati Mrusi kafunga anga lote la Soviet Union,je makampuni mengine hayakuja kumkodishia ndege mrusi kwa malipo ya YUAN!? tuendelee kunywa supu nyama tutazikuta chini.

-Urusi kufunga bomba lake la Mafuta na Gesi.

Baada ya kuivamia Ukraine,ikiwa na maana Urusi kuivamia NATO,ama kwa namna nyingine nchi zinazotegemea mafuta na Gesi ya Mrusi kuisaidia Ukraine basi Mrusi amefunga bomba lake la Mafuta na Gesi,Je kufungwa kwa bomba la Mafuta na Gesi kutaiathiri Urusi,jibu ni hapana,Mrusi amejiandaa kwa miaka kusubiri siku hii adimu ya yeye kuwafungia mafuta na Gesi mataifa ya Ulaya,Kwa taarifa tu Urusi imekuwa ikiweka akiba ya dhahabu na akiba ya pesa ya Yuan kwa muda mrefu,hivyo basi Urusi ina akiba kubwa ya Yuan na Dhahabu kiasi cha kutotikiswa kwa namna yoyote ile na kukosa pesa ya mafuta na Gesi kutoka nchi za Ulaya,kukosekana kwa mafuta na Gesi katika nchi za Ulaya kutasababisha bei ya gesi na mafuta kupanda kwa nchi za Ulaya hivyo basi kusababisha kuyumba kwa upatikanaji wa dola,kusababisha mfumuko wa dola katika mfumo wa kifedha (Monetary system).

-Kufungua bomba la Mafuta na Gesi kwa malipo ya Yuan na sio dola tena.

Kwa miaka mingi Urusi na China imekuwa ikiisubiri siku hii,kutumia dhahabu kama mfumo wa malipo na kuutokomeza mfumo wa SWIFT unaotumia dola,nakumbuka Rais Magufuli alikuwa na ndoto hizi za kutumia rasilimali zetu na aliagiza benki kuu yetu iwe na akiba ya kutosha ya dhahabu,Vita ya Urusi na Ukraine umefikia lengo la kuitokomeza dola,Urusi sasa inaweza kutangaza kutotumia tena mfumo wa kuhamisha dola kwa SWIFT,Urusi sasa inaweza kusema tutafungua mabomba ya mafuta na Gesi kwa malipo ya pesa ya China ya YUAN tu.Kwa yeyote mwenye kutaka mafuta ya Urusi au Gesi ya Urusi basi alipe kwa dhahabu au atumie mfumo wa ruble-yuan gold payment system,asiyetaka atakufa na baridi kwa kukosa gesi kuleta joto nyumbani na watakufa na njaa kwa kupungua uzalishwaji wa ngano katika bara la Ulaya.

-China yupo upande gani kwenye mgogoro wa Urusi na Ukraine.

Nani yupo kimya pasipo kusema lolote kwenye mgogoro wa Urusi na China!? Kimya wanasema kinamaanisha ndio,China hamtupi ndugu yake,atampa mkono rafiki "strategic partner" kwenye suala la Mafuta,Gesi na Kilimo cha ngano,mfumo wa Yuan-Ruble utaanza rasmi na kusaidiana na mfumo wa malipo ya dhahabu,kufikia hapa Vladimir Putin atahitimisha rasmi mfumo wa Petro-Dollar yaani malipo ya Dola kwenye soko la mafuta kwa kukasimiwa,kukaimiwa ama kuchukuliwa na mfumo Yuan-Ruble,Hivyo basi NATO wasahau kumtoa Putin kwa urahisi kama walivyomtoa Charles De Gaulle au Gaddafi baada ya kuchallenge Petro-Dollar system.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Kweli kila kitu ni mipango kumbe ndio maana Putin bado ni jeuri ......hatetemeki[emoji23][emoji23]
 
Hizi nazo ni njozi
Eti pesa ya Russia sijui China itaizidi $$$$
Acha wazifyeke kwenye matumizi ya vita isiyo na kichwa wala mguu wakija tahamaki umaskini utawatawala.. ....
Marekani ipo kama haipo huko vitani kwa vile wanajua MRussia atajitutumua weeee kabla ya maridhiano atampiga moja la kumnyamazizisha milele
 
Those are Thinkful wishes.

Dollar haitakufa kwa Boycott(Kususiwa) Bali kwa kupata Mshindani kwenye Soko la Dunia.

Kila siku Mchina akishikwa Pumbu kwenye EXPORT anaamua kushusha thamani ya Pesa yake ili kuongeza EXPORT. Sijawahi kusikia Serikali ya Marekani ikitangaza kuishusha thamani Dollar ya Marekani,laaa hasha,kupanda na kushuka kwa Dollar kunatokana na Soko. Sasa ni nchi gani iko tayari kuweka hadhina yake kwa YUAN ya China ambayo Kesho unashangaa Rais wa China kaishusha thamani? China yenyewe ina hadhina ya Matrillioni ya Dollar ili kutoa backup ya uchumi wake.

Sijaona fedha mbadala wa Dollar kwa miongo mingi ijayo zaidi zaidi naona hasira za Mchina na Urusi dhidi ya Marekani,lakini Uhalisia wanaujua bila Shaka.
 
Yote kwa yeyote, pamoja na kwamba sikusoma bandiko lako lote, maoni yangu kwa ufupi ni kwamba huu mzozo na vikwazo vinavyotolewa havitamuumiza mrusi peke yake, hata hao wanaoweka vikwazo wanajua wanajiwekea vikwazo pia kinamna, pamoja na kwamba wanachagua wapi pa kuweka vikwazo na kuacha kwingine kunakowaumiza wao zaidi ya huyo anayewekewa vikwazo.

Hawa watu wa Magharibi pamoja na washirika wao wanaonyesha dhahiri jinsi gani wanavyoendelea kuitawala dunia kibiashara, na dunia nayo sasa itaanza kudai uhuru kutoka kwenye makucha ya hawa wakoloni.
Naamini huu utakuwa ni mwanzo wa harakati za ukombozi katika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom