Unapoamua kuwa mkweli tumia akili. Nami nakuomba tumia sasa akili zako zote.
Unaposema Haki unamaanisha haki kweli,. Je hujui kama palestina ni taifa lenye mipaka? Historia unayoidai inatambuliwa na UN?
Kufa kwa wapalestina ni sawa na kifo cha wengine.
Kwani hujui kuwa NATO na washirika wake wamekuwa wakianzisha vita duniani kwa mwamvuli wa demokrasia?.
Ningeona uko neutral kama kama ungeilaumu pia ukraine kwa kutumiwa kama kondom ili NATO anatanue wigo wake na kukiuka mkataba wa Minsk, uongozi mbovu ndio unaochangia kuua raia wake.
Kuhusu Wapalestina, sielewi kama unaujua kikamilifu huo mgogoro. Ungekuwa unaufahamu wala usingelinganisha mgogoro huo na wa Ukraine na Russia.
Ufahamu kuwa Ukraine ni nchi, na Russia ni nchi. Nchi moja imeenda kuivamia nchi nyingine.
Mgogoro wa Wayahudi na wapalestina, kwa urahisi ungeweza kusema ni mgogoro wa kijamii, yaani jamii mbili, jamii ya wayahudi na jamii ya Wapalestina, lakini wote wakiwa kwenye nchi moja.
Jamii ya Wapalestina inaona inaonewa na jamii ya Wayahudi kwa kunyang'anywa ardhi yao. Kwa miaka mingi, kwa sababu ni ndani ya nchi moja, imekuwa ni shida sana mataifa mengine kuingilia mgogoro huo moja kwa moja. Na pia kitendo cha makundi ya itikadi kali kutoka kwa Wapalestina mara kwa mara kurusha makombora kwa wayahudi, tena yakilenga raia, kumeyafanya makundi hayo kuonekana ya kigaidi, na hivyo kutoonewa huruma. Makundi hayo yamekuwa yakiua hata viongozi wa kipalestina wanaoonekana kutaka kufanya mazungumzo na Israel.
Mwaka 1988, ndipo kwa mara ya kwanza wanaharakati wa Palestina walitangaza kuwa Palestina ni nchi huru, na hawatakuwa chini ya Israel. Hata hivyo, azimio hilo halikutambuliwa na jamii ya kimataifa. Miaka ya karibuni, kwa usimamizi wa UN, kumeundwa mamlaka ya Palestina (haina hata kiti UN). Kuna maazimio mengi UN kuhusiana na mgogoro kati ya mamlaka ya Palestina na Serikali ya Israel. Mipaka ya mamlaka ya Palestina inafahamika, na wala haijaingiliwa na Israel. Hata hivyo kilio cha Wapelestina ni yale maeneo ambayo yalichukuliwa na Wayahudi mwaka 1967.
Na ukumbuke kuwa kwa miaka mingi Palestina imekuwa inapigania ardhi siyo utaifa kwa sababu hakuna nchi inayoitwa Palestina.
Kwa hiyo mgogoro wa Wapalestina na Wayahudi siyo mgogoro wa nchi na nchi bali ni mgogoro wa jamii mbili ndani ya nchi moja.
Lakini, iwe Palestina ni Taifa kamili au mamlaka, wananchi wake wana haki zote, ikiwepo haki ya kuishi, kama binadamu wengine. Lakini kutokywepo kwa hali hiyo, atizo halipo kwa wayahudi pekee, na huenda zaidi lipo upande wa makundi yenye itikadi kali ya Wapalestina. Mathalani Hamas, hawautambui hata uongozi wa mamlaka ya Wapalestina, nao wamejitwalia sehemu ya ardhi iliyo chini ya mamlaka ya Wapalestina na kulitawala, na kisha kursha makombora dhidi ya Israel kutokea maeneo hayo.
Na haya makundi hayataki mazungumzo yoyote na wayahudi, na wao wanaamini na wametangaza wazi kuwa suluhisho la mgogoro huo ni kufutwa kwa wayahudi Duniani. Sasa kwa fikra hizo, unadhani utaungwa mkono na jamii ya kimataifa?
Kwa wanaojua historia, neno Wapalestina linatokana na neno la kigiriki 'Philistines' (wafilisti - kwa Kiswahili). Hawa waliishi kwenye nchi ya Judea, na Judea ni jina lililotokana na jina la Judah (Yuda, mtoto wa kwanza wa Yakobo). Ni katika nchi hii ya Judea, ndiko Yesu alizaliwa, wayahudi na Wafilisti waliishi maeneo hayo pamoja lakinj kwa uhasama. Hivyo Judea (leo inajumuisha Israel na Palestine) ni nchi ya jamii hizo zote mbili. Kama wote wangejaliwa hekima, wangetafuta namna ya kuishi pamoja na siyo hizo fikra za kwamba kuna jamii mojawapo inatakiwa kupotezwa, isiwepo duniani.
Kuhusu mkataba wa Minsk, nadhani hata huuelewi. Kwanza haukuwa na kipengere cha kuizuia Ukraine kujiunga na EU au NATO. Na pia mkataba huo ambao uliosainiwa mwaka 2014, haukuheshimiwa, na kiongozi wa waasi, ndiye alikuwa wa kwanza kusema mkataba huo hawautaki na wameuvunjilia mbali. Hivyo mwaka 2015, ulivunjika rasmi.
Soma hapa chini utaelewa zaidi:
Text of the protocol
The text of the protocol consists of twelve points:[13]
To ensure an immediate bilateral ceasefire.
To ensure the monitoring and verification of the ceasefire by the OSCE.
Decentralisation of power, including through the adoption of the Ukrainian law "On temporary Order of Local Self-Governance in Particular Districts of Donetsk and Luhansk Oblasts".
To ensure the permanent monitoring of the Ukrainian-Russian border and verification by the OSCE with the creation of security zones in the border regions of Ukraine and the Russian Federation.
Immediate release of all hostages and illegally detained persons.
A law preventing the prosecution and punishment of people in connection with the events that have taken place in some areas of Donetsk and Luhansk Oblasts.
To continue the inclusive national dialogue.
To take measures to improve the humanitarian situation in Donbas.
To ensure early local elections in accordance with the Ukrainian law "On temporary Order of Local Self-Governance in Particular Districts of Donetsk and Luhansk Oblasts".
To withdraw illegal armed groups and military equipment as well as fighters and mercenaries from the territory of Ukraine.
To adopt a programme of economic recovery and reconstruction for the Donbas region.
To provide personal security for participants in the consultations.