Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,753
Well said, nimekuelewa vizuri, shukrani - kusema kweli pale Ukraine hapakutimika ushawishi hata kidogo,kilicho fanyika pale kilitokana na vyombo vya kijasusi vya magharibi kujipenyeza nchini Ukraine pamoja na NGO za uongo na kweli hao ndio walitumika ku-fund vijana na kuchochea colour revolution,wakawapa mafunzo na kuwalipa snippers wa kulenga shabaha na kuuwa watu - in short creating chaos/turmoil ili nchi hisitawalike, kama unakumbuka hata seneta wa Merikani marehemu McCain na Nulad walikuwa wanafunga safari ya zaidi 3000Km kutoka Merikani kuja Ukraine kuja kuchochea vurugu hizo nchini Ukraine -why Ukraine?? Kilicho fanyika pale ni mapinduzi kuiondoa madarakani Serikali halali iliyo chaguliwa kidemokrasia na sio ushawishi.Mkuu, naomba nikuulize, hivi taifa la Ukraine halikuwahi kuangukia na kufuata sera za urusi?
Kama taifa la Ukraine liliwahi kuwa mfuasi mwaminifu wa sera za urusi, marekani na mataifa ya magharibi yalifanyaje Ili kuirudisha Ukraine ifuate sera za magharibi??
Je marekani na washirika wake waliivamia Ukraine wakiilazimisha ifuate sera za magharibi??..,bila shaka hapana,
Je marekani na washirika wake waliwezaje kuifanya Ukraine awe mfuasi mwaminifu wa sera za magharibi? .., jibu utakalolipata hapa ni USHAWISHI.,kwa nini urusi haamini katika USHAWISHI na badala yake anaona matumizi ya nguvu pekee ndo njia ya kutimiza malengo yake?
Dunia ya Leo haiitaji matumizi ya nguvu Bali USHAWISHI tu,ukishindwa kunishawishi Ili nifuate sera zako,basi kubali maumivu tu,
Mwanamke mwenyewe anaitaji ushawishi Ili uweze kumpata sembuse taifa[emoji848]
Cha ajabu jaribio kama hilo lilipo fanyika mjini Washington DC pale Bungeni, waandamanaji wakilalama kwamba Trump ndiye alishinda kura kwa hiyo ndiye alipashwa kuwa Rais na sio Biden,je,kama wabunge wa Urusi wangefunga safari kuja Merikani kuwaunga mkono waandamanaji,je, Serikali ya Merikani ingesemaje?? Labda tuanzie hapo.