Urusi walalamika kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Marekani wanaoelekeza namna ya matumizi ya HIMARS

Well said, nimekuelewa vizuri, shukrani - kusema kweli pale Ukraine hapakutimika ushawishi hata kidogo,kilicho fanyika pale kilitokana na vyombo vya kijasusi vya magharibi kujipenyeza nchini Ukraine pamoja na NGO za uongo na kweli hao ndio walitumika ku-fund vijana na kuchochea colour revolution,wakawapa mafunzo na kuwalipa snippers wa kulenga shabaha na kuuwa watu - in short creating chaos/turmoil ili nchi hisitawalike, kama unakumbuka hata seneta wa Merikani marehemu McCain na Nulad walikuwa wanafunga safari ya zaidi 3000Km kutoka Merikani kuja Ukraine kuja kuchochea vurugu hizo nchini Ukraine -why Ukraine?? Kilicho fanyika pale ni mapinduzi kuiondoa madarakani Serikali halali iliyo chaguliwa kidemokrasia na sio ushawishi.

Cha ajabu jaribio kama hilo lilipo fanyika mjini Washington DC pale Bungeni, waandamanaji wakilalama kwamba Trump ndiye alishinda kura kwa hiyo ndiye alipashwa kuwa Rais na sio Biden,je,kama wabunge wa Urusi wangefunga safari kuja Merikani kuwaunga mkono waandamanaji,je, Serikali ya Merikani ingesemaje?? Labda tuanzie hapo.
 
umeandika pumba sn yaan bajeti ya Urusi ni mara mbili ya USA hlf atumie 5% ya nguvu yake kupambana na nchi inayosaidiwa na USA na west
Daaaa[emoji2] defence budget US Ni $700b+ Russia ni$69+nb
 
Cha kushangaza haijasaidia kurudisha maeneo yaliyochukuliwa.
 
Inawezekana umesoma vitu vingi ila kuviunganisha upate hoja ndio tatizo lilipo. Ilibidi ueleze sababu za hao Waukraine wenye asili ya Urusi kuuwa ni zipi. Kwa kifupi ni kuwa, Urusi haiamini kama ni taifa huru, ndio maana hata hii vita ilipokuwa inaanza Mandonga (Putin)alisema anataka kusahihisha makosa ya kihistoria (kuirudisha Ukraine kuwa sehemu ya Urusi).
Ikumbukwe kwenye 2014 Urusi iliitwaa Crimea kwa nguvu kutoka Ukraine. Ili kuendeleza mipango yake miovu, akapandikiza mamluki kwenye majimbo ya Donesk na Luhansk ambayo yana raia wengi wanaoongea Kirusi. Mamluki hawa wamekuwa wakipewa Mafunzo na silaha kutoka Urusi ili wapambane na Serikali ya Kyiv kwa ajili ya kujitenga.
Hakuna taifa ambalo linaweza kuruhusu baadhi ya maeneo yake kujitangazia uhuru kienyeji namna hii. Urusi mwenyewe alitumia vita wale Chenchen walipotaka kujitenga kutoka Urusi, Nigeria iliwahi kupigana vita vya Biafra kwa ajili hii, mtiti wa Catalan tuliuona.
Hawa waasi wanaozungumza Kirusi ndio walikuwa wanauawa kutokea 2017 kutokana na uasi wao. Ati Urusi alienda kuwalinda waasi dhidi ya Serikali halali ili uasi ukamilike vizuri. Mandonga aache janjajanja zake.
 
Leo Pekee kuna Mji Umepigwa chakari ni maghala ya hizo Himars aliyanunu tajiri mmoja wa Ukraine nae kajumlishwa anaitwa Vadatusrsky....
 
Video please
 
Kulinganisha US kutumia HIMARS Afghanistan na Ukraine kutumia HIMERS dhidi ya Urusi ni vitu viwili tofauti. Hizi HIMERS kwa kiasi kikubwa naona zinalenga military infrastructures na kuziharibu. Taleban kwa kiasi kikubwa hawakuwa na military hardware za kushambulia, wala walikuwa walikuwa hawapigani conventional war, walikuwa na bunduki na wanashambulia kwa kuvizia na kurudi majumbani. Hapo HIMERS haziwezi kuwa na matokeo makubwa.
Kwa vita ya Ukraine, Urusi ana vifaa vingi na vikubwa vya kijeshi pamoja na miundombinu wezeshi. Hivyo matokeo ya HIMERS yataonekana vizuri tofauti na huko Afghanistan.
 
HIMARS ni zao la zamani sana, sio la New Millenium ni la 20th century ila laisumbua systems za 21st century
 
Package ya msaada inayofuata ya $280mil kutoka USA ina siraha za high and very advanced technology nyingi. Wa Ukraine wengi wapo Marekani wakipata maujuzi ya kuzitumia
Si hivyo tu, bali silaha advanced lazima wamarekani wawepo ili kuzuia kuuzwa kwa Urusi
 
Yaani hata mimi nakuunga mkono,Urusi ilitakiwa within 7 days iwe tayari imemaliza vita .Vita ikichykua muda mrefu adui anakusomal na hata kama ni nunda atakushinda tuu kwa sababy umejiaminin sana.
UK asingekubali Ukraine kudondoka, ndo maana alikuwa wa kwanza kabisa kupeleka silaha
 
Kiuhalisia Marekani ana uzoefu sana, yeye vitani haendi jaribisha, anaenda piga
 
Afu mwambie Taliban walikuwa wanatumia raia kama kinga
 
Hizo zote ni propaganda, tulishaona nia ovu za Russia kwa majirani zake kuanzia Georgia mpaka hapo Ukraine, acheni kuibebesha uchafu Marekani.
Mkuu hizi akili sijui pro russia huwa wanatoa wapi nadhani hata Putin akiwasikia atashangaa.

Wakati hii the so called operation inaanza walivyoanza ku mobilize vikosi walisema wako kwenye mazoezi US akaiambia dunia kwamba russia ana mpango wa kuivamia Ukraine ajabu wakapinga hawana nia hiyo siju kadhaa wanaingiza jeshi ukraine western allies wote walijua ndio basi Putin kashachukua ukraine yote to their suprise wakagundua kumbe ukrainians hawako tayari kuchukuliwa kirahisi na wana morali ya kupambana ndio kama unakumbuka support ilianza kutolewa baadae mpaka watu humi wakawa wanasema US anaogopa kumpa silaha ukraine.

Ajabu mrusi wa sokomatola anasema western ndio walitaka vita. Kama kawaida mambo yameanza kuwa magumu anabebeshwa mzigo US ambae ana support tu wakati walionza kuvamia nchi ni wao.
 
Atakuwa amekuelewa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…