URUSI: Wananchi wanapiga kura kuongeza muda wa Rais Putin

URUSI: Wananchi wanapiga kura kuongeza muda wa Rais Putin

mheshimiwamtemi

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Posts
291
Reaction score
218
Wananchi huko Urusi wameanza kupiga kura ya maoni ili kuruhusu Rais Putin kubakia madarakani kwa miaka 16 zaidi. Upigaji kura huyo utakamilika Julai mosi.

Urusi inafanya kura ya maoni ya kubadilisha Katiba ya nchi ili kumuwezesha Vladimir Putin asalie madarakani hadi mwaka 2036 na atekeleze itikadi zake za kihafidhina katika Katiba.

====

Kura hiyo inapigwa wakati nchi ya Urusi inaendelea kukabiliwa na janga hatari la Corona.

Tarehe rasmi ya "mashauriano ya kitaifa" ni Julai 1, lakini mamlaka ilifungua vituo vya kupigia kura Juni 25 ili kuepusha mikusanyiko mikubwa ya watu, kwa sababu ya janga la Covid-19.

Ili kuanzisha hatua kadhaa za kijamii, kura sasa zitatekelezwa kwa zaidi ya siku tano kote Urusi, hata katika mikoa ambayo inapambana na Covid-19 hivi sasa.

"Bila Putin, hakuna Urusi. " Haya ni maoni ya mkuu wa wafanyakazi wa Kremlin, na inadhihirishwa na mamilioni ya Warusi ambao kwa miongo kadhaa wamemchagua tena Vladimir Putin kuendelea kuwepo madarakani kama Waziri mkuu au rais.

Imani hii inaweza kurudiwa Julai 1, baada ya kura ya maoni ya kitaifa ya kurekebisha katiba ya Urusi, ili kumwezesha Rais Putin kupata nafasi nyingine ya miaka sita tena.

Ingawa Rais Putin hajasema kuwa anataka kuchaguliwa tena, hajakataa hilo, na kusababisha wakosoaji kumshtaki kwa kutengeneza njia ya kukaa madarakani kwa maisha, au angalau hadi 2036.

Mchakato huo wa kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba ulipendekezwa na rais Vladmir Putin na awali ulipangiwa kufanyika Aprili 22 lakini kutokana na kuzuka kwa janga la virusi vya Corona ukaakhirishwa.

Putin ameshakaa madarakani kama rais na pia kama waziri mkuu katika kipindi cha miongo miwili iliyopita na ni kiongozi aliyetawala kwa kipindi kirefu zaidi nchini Urusi tangu Joseph Stalin aliyekuwa kiongozi wa Soviet.


Source: BBC
 
mkuu malizia stori nzima unakimbilia wapi? nimeangalia Al Jazeera leo! tukumbuke Putin ni dikteta na anaipenda Africa na wale watawala wake wapumbavu wasiong’oka madarakani! hili amezungumza mwenyewe! Putin ana laana sababu anahudumia vita nyingi za mashariki ya kati mf Syria na Africa mf Libya ambako mamilioni ya watu wasio na hatia kama watoto na kinamama na wazee wanakufa na kukimbia ovyo! Putin ana makosa mengi ya mauaji ndani na nje ya Urusi anaogopa mkono wa sheria kiti cha urais kinamlinda!

Kuhusu kura za maoni wamesema Al Jazeera kuwa asilimia zaidi ya sitini ya vijana wanapinga hawamtaki, theluthi moja tu ya vijana ndio wanaomkubali, wanaopigania avunje katiba kwa ulafi wake wa madaraka na kuongeza tena vipindi viwili ni wazee wajinga wachumia tumbo na wapumbavu kama ilivyo hapa bongo ambao wengi wao wamebakiza miongo miwili tu kuaga dunia kwa takwimu za life span ya mtu mweusi si kwa mujibu wa Allah of course!

Putin kaona viongozi wajinga wanavunja katiba Afrika raia wako kimya hadi wajifie wenyewe kama Nkurunzinza basi kawaiga ili aendelee kutesa watu duniani!

ikumbukwe pia Putin ni mmoja wa genge la majasusi la Urusi ambao ni matajiri wakubwa na kutoka kwake madarakani ni kudhoofisha pia uchumi wa kundi hilo na genge haliko tayari kwa hilo(Russian oligarchy)

Bongo tunaelewa pia siasa za nje hatuna la kuiga kutoka kwa Putin!
 
Huyo ni Rais anayejitambua na mwenye nidhamu ya kuheshimu wajibu wake kwa nchi yake!

Anatawala nchi ya dunia kwanza yenye uchumi imara, teknolojia, taasisi imara, miundombinu, ajira, na huduma zote za jamii ambazo ni za uhakika.

Hata akiongoza miaka mia, nchi itazidi kwende mbele bila shida.

Huku kwenye manchi ya shithole yaliyojaa umasikini unakuta jitu linang'ang'ania madaraka huku liko incompetent, tapeli na dhulumati!

Manchi yetu haya bado sana. Bado tuko kwenye stage fulani ya kutafuta chakula.

Tukivuka hiyo stage ya kutafuta chakula huenda sasa tukaanza ku deal na serious issues.
 
mkuu malizia stori nzima unakimbilia wapi? nimeangalia Al Jazeera leo! tukumbuke Putin ni dikteta na anaipenda Africa na wale watawala wake wapumbavu wasiong’oka madarakani! hili amezungumza mwenyewe! Putin ana laana sababu anahudumia vita nyingi za mashariki ya kati mf Syria na Africa mf Libya ambako mamilioni ya watu wasio na hatia kama watoto na kinamama na wazee wanakufa na kukimbia ovyo! Putin ana makosa mengi ya mauaji ndani na nje ya Urusi anaogopa mkono wa sheria kiti cha urais kinamlinda!..
Story za vijiwe vya kahawa
 
Ulichoandika ndio muendelezo wa hiyo habari au ni maoni na mtazamo wako juu ya hiyo habari?

Habari nimeangalia mwenyewe leo asubuhi Al Jazeera imesema two third ya vijana hawamtaki Putin! ni wazee na genge lake wanalazimisha! hayo mengine ni news from other sources! usidanganywe mkuu uwe unacheki Al Jazeera na France 24 English daily!
 
Habari nimeangalia mwenyewe leo asubuhi Al Jazeera imesema two third ya vijana hawamtaki Putin! ni wazee na genge lake wanalazimisha! hayo mengine ni news from other sources! usidanganywe mkuu uwe unacheki Al Jazeera na France 24 English daily!
Wewe ni mtazamaji mzuri wa habari lakini si mchambuzi mzuri hasa media za kimataifa!
 
Wewe ni mtazamaji mzuri wa habari lakini si mchambuzi mzuri hasa media za kimataifa!
wewe unatazama na kuchambua vizuri ulielewaje mkuu? nisaidie uchambuzi pale!

kiufupi ili unielewe natumia combination ya habari na maoni katika aina yangu ya uandishi naiita ‘provocative’ , yani wahusika bongo kama wewe nawachukiza kwa kuwachana live humo humo!

mtu afanyae mabaya hawezi kujirudi kama hukumchukiza kwa kumchana na kukemea upumbavu wake!

unajifanya hamnazo eti hujui kuwa msingi wa huu uzi ni kuendeleza harakati za kipumbavu za washamba kutaka kumbakisha Rais wa bongo kwa kipindi cha tatu kama Nkurunzinza hiyo sio bongo wakafanye Burundi

sera ya kubaka katiba kwa kuongeza muda wa urais ni ulaya huko ila kwa Africa huleta vita na hatukubaliani nayo hapa bongo ni kwetu sote si kwa yule mgogo na yule mrangi mjinga peke yao , yule mrangi mpumbavu alieanzisha hiyo mada! kwanza akitoka Magu ni zamu yetu wazenji na ni zamu ya Rais muislam msitutoe kwenye mada miaka kumi tutakuwa tumechoka hoi kabisa kuongozwa na machogo na kanisa! Ni zamu ya Maalim sasa.

ukiwa mvivu wa kufikiri na uko mbali na update za siasa za bongo na za nje huwezi kunielewa kamwe!!
 
mkuu malizia stori nzima unakimbilia wapi? nimeangalia Al Jazeera leo! tukumbuke Putin ni dikteta na anaipenda Africa na wale watawala wake wapumbavu wasiong’oka madarakani! hili amezungumza mwenyewe! Putin ana laana sababu anahudumia vita nyingi za mashariki ya kati mf Syria na Africa mf Libya ambako mamilioni ya watu wasio na hatia kama watoto na kinamama na wazee wanakufa na kukimbia ovyo! Putin ana makosa mengi ya mauaji ndani na nje ya Urusi anaogopa mkono wa sheria kiti cha urais kinamlinda!..
Media ya Beberu iseme Putin mzuri?
 
wewe unatazama na kuchambua vizuri ulielewaje mkuu? nisaidie uchambuzi pale!

kiufupi ili unielewe natumia combination ya habari na maoni katika aina yangu ya uandishi naiita ‘provocative’ , yani wahusika bongo kama wewe nawachukiza kwa kuwachana live humo humo!..
ALIYEBAKA KATIBA YA CHAMA NA KUONDOA UKOMO WA KUGOMBEA UENYEKITI HATA YEYE AKIWA RAISI ATATAKA AENDELEE!

MADARAKA MATAMU!
 
Back
Top Bottom