Udikteta hauna sura mpya wala tofauti tofauti; hauna umagharibi wala umashariki ama ukusini wala ukaskazini. Udikteta ni udikteta tu!
Rudi katika historia upate kujua udikteta ulivyoanza pia fuatilia taarifa za habari hasa chaguzi za nchi mbalimbali na michakato ya kuongeza muda wa madaraka.
Hiki kinachofanyika Urusi hivi sasa si kitu kipya, kimekwisha kufanyika hapo awali na kama unaamini sana katika kura, tambua kuwa hata hizo kura zinaweza pia kuchakachuliwa na kiongozi akaonekana ameshinda kwa asilimia hata 99.98 wakati alichokifanya ni kucheza tu na namba.
Zinduka!