URUSI: Wananchi wanapiga kura kuongeza muda wa Rais Putin

URUSI: Wananchi wanapiga kura kuongeza muda wa Rais Putin

Kwa nchi kama urusi,China,Korea,
Kiongozi kuongezewa muda wa kukaa madarskani,kuna faida kubwa,kwa sababu hapa yanaangaliwa maslahi mapana ya nchi,
Mfumo kama wa China,kila anayeingia kuwa raisi anazingatia maslahi mapana ya nchi,hata raisi akila rushwa,anakula shaba tu,
Hivi ukiwa na raisi kama wa China,anayeifsnya nchi yake inakuwa superpower,ktk kila sekta,tekinolojia,jeshi,kilimo,usalama,utataka atoke??
Tofauti yetu na wao,sie huku,wanataka waongezewe muda,ili walinde maslahi ya chama,na ya kwao binafsi,hawana master plan ya kunufaisha nchi nzima,wanawaza kunufsisha mikoa yao,kabila lao,familia zao,hawana vision ya kuifsnya bongo iwe kama Malaysia,Philippine,SA,au India,wao ni majigmbo,uteuzi,matusi,chuki,
Imagine
 
faida ni nyingi,

, moja ni huyu akitoka tutapata Rais mwenye maono na sera tofauti za kuendeleza watu pia ambao wametupiwa virago mfano yule kijana aliemwita Rais mshamba amesema bungeni nikimsikia huku Bwana Februari yuko pembeni akichekelea basi bwana Nipe alisema kuwa pamoja na mshua kujenga miundombinu bora kakosea mno na haelewi kabisa ilani ya chama chao inayotaka raia wawe na hali bora sababu kwasasa hata buku tu ni ngumu mno kuipata familia nyingi zinashinda njaa!! yule bwana wa kusini anasema Rais hafanyi alichotumwa na sisiem yao!

pili kwasasa ni wasukuma wanakula nchi wengine wamepewa vyeo vikubwa kuliko akili zao na wana vyeti feki hawa waropokaji wakitoka Rais mpya atakuja na timu yake na wengine walio taabani kiuchumi kwasasa nao watapata masurufu! kutesa kwa zamu mkuu!

tatu, sisi wazenji ni sehemu ya muungano nasi ni haki yetu kuongoza nchi hii mbona machogo mwajifanya hamnazo eti? yakhe muungano gani wa pande moja si ukoloni tu huu?

nne, pesa za ikulu ziendazo kuendeleza makanisa zitaendea kuendeleza misikiti!

tano, baraza la mawaziri lililojaa wakristo litabalansi akiingia muislam sababu sote tuna haki na nchi hii, kumbuka wazee wa kiislam ndio walimlipia Mwalimu nauli kwenda nje kudai uhuru au hujui?

sita akija Rais kama mkwere hana shida na sheria za vyama vingi kufuatwa wapinzani hawataumizwa wala kupotezwa!

saba, akija muislam nasi wazenji tutasikia raha ati kama vile wewe usikiavyo raha kanisa kuongoza nchi kwasasa usiwe mbinafsi ndugu utaleta vita isiyohitajika watu wasio na hatia watakufa bure! Burundi ya Nkurunzinza haikaliki leo hii wanauana kila siku baada ya bwana yule kuibaka katiba mwaka 2015! wakimbizi wamejaa kigoma au hujui?
chogo baba yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namkubali Putin lakin hapa ameanza kunifelisha.
Hana tofauti na wengine Kama akina Lukashenko.
Siku moja alihojiwa akasema hawezi kuongeza mda madarakani. Lakini sa anafanya Nini. Mpumbavu fala
Akufelishe vipi !? Wakati yupo kwaajili ya maslahi mapana ya nchi
 
Vladmir sio dikteita kwan c anapigiwa kura nawananchi MKUU ama kajiongezea kinguvu hayo mamlaka ?!

Kama kupenda watawala wpumbavu wasiopenda kutoka madarakani US anaongoza kuaanzia kwa SAUDIA QATAR BAHRAIN YEMEN KUWAIT UAE nakwengineko

Muache kua wanafiq aseee....
Ni wapi ulisikia ama ni nani alikuambia kuwa dikteta hawezi kupigiwa kura?

Pia ni wapi uliposikia kuwa udikteta ni kukaa muda mrefu madarakani?

Hizo ni hoja nyepesi mno kutokana na wewe kushindwa kuelewa maana halisi ya udikteta.

Tafuta kujua kwanza maana halisi ya udikteta na jinsi unavyofanya kazi.
 
Hahaha wewe jamaa .. Unaleta vituko sasa kumbe unaleta udini katika masuala ya utawala
mkuki kwa nguruwe! udini uko ndani yetu sote tunaukandamiza tu! nyie kwanini mnataka kuibaka katiba? udini mnao nyie! ni haki yetu kusema msitufunge mdomo! ingekuwa ni mwislam mkwere anataka kuongeza muda mngekubali?
 
Ni wapi ulisikia ama ni nani alikuambia kuwa dikteta hawezi kupigiwa kura?

Pia ni wapi uliposikia kuwa udikteta ni kukaa muda mrefu madarakani?

Hizo ni hoja nyepesi mno kutokana na wewe kushindwa kuelewa maana halisi ya udikteta.

Tafuta kujua kwanza maana halisi ya udikteta na jinsi unavyofanya kazi.
Uliwahi kuona wapi dikteit anachaguliwa kwakupitia kura ?!
 
Sasa habari umeangalia aljazeera sawa hii. Habari aliyoleta mtoa mada amei copy BBC ... How come una muambia kuwa aimalizie wakati vyombo vilivyo tumika kutoa habari za puttin ni vyombo viwili tofauti ...!!?
kila mtu ana haki kuangalia habari za chombo cha nje anachopenda wewe lazima umesoma st open university swali moja jibu moja tu la mwalimu! mtabaki maskini bongo hadi mwisho wa dunia! nani kakwambia BBC ni Mungu sote tumfuate?
 
Mkishampata mtu sahihi (kwa mujibu wa wapiga kura) mnaendelea naye hadi afe au achoke kufikiri.

Katiba ya Marekani haikuwa na ukomo wa mihula kwa Rais ila Washington (Rais wa kwanza) aliweka utamaduni wa mihula miwili ambao ulifuatwa na marais 31 waliomfuatia.

Miaka 114 baadae akapatikana mwamba FDR (Rais wa 32) akawakosha wamarekani,wakamchagua mihula minne hadi akafia madarakani.

Alipokufa tu Roosevelt akaingia Harry Truman ghafla tu yakafanywa marekebisho ya katiba kuweka ukomo.

Why ukomo kwa Truman akiwa hajamaliza hata ile awamu iliyoachwa na FDR?

Mbona huo mchakato haukuwepo kipindi FDR akiwa hai?
 
Ni wapi ulisikia ama ni nani alikuambia kuwa dikteta hawezi kupigiwa kura?

Pia ni wapi uliposikia kuwa udikteta ni kukaa muda mrefu madarakani?

Hizo ni hoja nyepesi mno kutokana na wewe kushindwa kuelewa maana halisi ya udikteta.

Tafuta kujua kwanza maana halisi ya udikteta na jinsi unavyofanya kazi.
nisaidie maana ya udikteta mkuu na namna unafanya kazi!
 
nisaidie maana ya udikteta mkuu na namna unafanya kazi!
Udikteta ni mfumo wa kiutawala ambapo mtu mmoja ama kikundi cha watu wachache kinamiliki mamlaka au madaraka 'yote' ya nchi bila mipaka ya kikatiba.

Msingi mkuu hasa wa udikteta ni katika 'mamlaka yote' au kwa lugha nyingine 'absolute power' na haijalishi kiongozi huyo aliingia mamlakani kwa mapinduzi, kurithi nafasi ya uongozi ama kwa kura za wananchi.

Pia, udikteta si katika kukaa muda mrefu madarakani bali ni jinsi ambavyo mgawanyiko wa madaraka katika nchi ulivyo. Uongozi unaweza kuwepo muda mchache tu madarakani na ukawa na sifa kamili za udikteta.

Katika udikteta, huo mgawanyiko wa kimadaraka ama kwa lugha nyingine 'separation of power' haupo kwa maana ya kwamba mamlaka zote za nchi katika masuala ya utungaji wa sheria (bunge), utafsiri wa sheria (mahakama), dola n.k. ziko katika udhibiti wa kiongozi mmoja wa juu (dikteta) ama kikundi cha watu wachache.
 
Udikteta ni mfumo wa kiutawala ambapo mtu mmoja ama kikundi cha watu wachache kinamiliki mamlaka au madaraka 'yote' ya nchi bila mipaka ya kikatiba.

Msingi mkuu hasa wa udikteta ni katika 'mamlaka yote' au kwa lugha nyingine 'absolute power' na haijalishi kiongozi huyo aliingia mamlakani kwa mapinduzi, kurithi nafasi ya uongozi ama kwa kura za wananchi.

Pia, udikteta si katika kukaa muda mrefu madarakani bali ni jinsi ambavyo mgawanyiko wa madaraka katika nchi ulivyo. Uongozi unaweza kuwepo muda mchache tu madarakani na ukawa na sifa kamili za udikteta.

Katika udikteta, huo mgawanyiko wa kimadaraka ama kwa lugha nyingine 'separation of power' haupo kwa maana ya kwamba mamlaka zote za nchi katika masuala ya utungaji wa sheria (bunge), utafsiri wa sheria (mahakama), dola n.k. ziko katika uthibiti wa kiongozi mmoja wa juu (dikteta) ama kikundi cha watu wachache.
Kila siku mnautaftia udikteita sura Mpya kwamaslahi yawamagharibi

Hakuna dikteita anaechaguliwa kupitia kura ila anaweza akawa dekteita baada yakuchaguliwa hapa nakubali ila katika mchakato wakumpata dikteita kura haina nafasi.....
 
Ndio unihabarishe wapi na lini natoka lini dikteita akachaguliwa kwakupigiwa kura.....

Kama ndio hvyo dikteita anapigiwa kura na asiepigiwa kura anakua nani ?!
Hilo swali umeuliza sababu bado haujaelewa vyema kuhusu udikteta.

Elewa kwanza kuhusu udikteta.
 
Kila siku mnautaftia udikteita sura Mpya kwamaslahi yawamagharibi

Hakuna dikteita anaechaguliwa kupitia kura ila anaweza akawa dekteita baada yakuchaguliwa hapa nakubali ila katika mchakato wakumpata dikteita kura haina nafasi.....
Udikteta hauna sura mpya wala tofauti tofauti; hauna umagharibi wala umashariki ama ukusini wala ukaskazini. Udikteta ni udikteta tu!

Rudi katika historia upate kujua udikteta ulivyoanza pia fuatilia taarifa za habari hasa chaguzi za nchi mbalimbali na michakato ya kuongeza muda wa madaraka.

Hiki kinachofanyika Urusi hivi sasa si kitu kipya, kimekwisha kufanyika hapo awali na kama unaamini sana katika kura, tambua kuwa hata hizo kura zinaweza pia kuchakachuliwa na kiongozi akaonekana ameshinda kwa asilimia hata 99.98 wakati alichokifanya ni kucheza tu na namba.

Zinduka!
 
mkuu malizia stori nzima unakimbilia wapi? nimeangalia Al Jazeera leo! tukumbuke Putin ni dikteta na anaipenda Africa na wale watawala wake wapumbavu wasiong’oka madarakani! hili amezungumza mwenyewe! Putin ana laana sababu anahudumia vita nyingi za mashariki ya kati mf Syria na Africa mf Libya ambako mamilioni ya watu wasio na hatia kama watoto na kinamama na wazee wanakufa na kukimbia ovyo! Putin ana makosa mengi ya mauaji ndani na nje ya Urusi anaogopa mkono wa sheria kiti cha urais kinamlinda!

Kuhusu kura za maoni wamesema Al Jazeera kuwa asilimia zaidi ya sitini ya vijana wanapinga hawamtaki, theluthi moja tu ya vijana ndio wanaomkubali, wanaopigania avunje katiba kwa ulafi wake wa madaraka na kuongeza tena vipindi viwili ni wazee wajinga wachumia tumbo na wapumbavu kama ilivyo hapa bongo ambao wengi wao wamebakiza miongo miwili tu kuaga dunia kwa takwimu za life span ya mtu mweusi si kwa mujibu wa Allah of course!

Putin kaona viongozi wajinga wanavunja katiba Afrika raia wako kimya hadi wajifie wenyewe kama Nkurunzinza basi kawaiga ili aendelee kutesa watu duniani!

ikumbukwe pia Putin ni mmoja wa genge la majasusi la Urusi ambao ni matajiri wakubwa na kutoka kwake madarakani ni kudhoofisha pia uchumi wa kundi hilo na genge haliko tayari kwa hilo(Russian oligarchy)

Bongo tunaelewa pia siasa za nje hatuna la kuiga kutoka kwa Putin!
kati
ya USA na urusi ni nani anaongoza kwa maovu.... ni nchi ngapi usa kavamia na hakuwa na ushahidi wa kutosha kuwa nci hzo ni za kidokteta au znamiliki nyuklia
 
kati
ya USA na urusi ni nani anaongoza kwa maovu.... ni nchi ngapi usa kavamia na hakuwa na ushahidi wa kutosha kuwa nci hzo ni za kidokteta au znamiliki nyuklia
pointi nzuri sana ila pia uovu wa USA haufuti uovu wa Russia! yaani uhalifu wa mtu mmoja si kigezo cha wewe nawe kuwa mhalifu mnahukumiwa wote tu!
 
Uoga.
Ukitawala nchi vibaya huku ukijua kuwa umejijengea chuki dhidi ya wananchi walio wengi unajikuta umeshakuwa mwoga kuishi bila madaraka.
Uoga huu ndiyo hupelekea mtu kutaka kung'ang'ania madaraka kwani unahisi pindi ukiwa umestaafu na pengine uliowaudhi ndio wako madarakani basi waweza chukuliwa hatua kali.

Ushauri: Tenda mema unapokuwa umeshika rungu ili siku ukimkabidhi mwenzio usiwe na wasiwasi wa maisha. Huu mtindo wa kubadili katiba na kujifanya wewe ni wa muyaya huwa hauna mwisho mzuri. Utakuja udhalilike uzeeni.
 
Back
Top Bottom