URUSI: Wananchi wanapiga kura kuongeza muda wa Rais Putin

Imagine
 
chogo baba yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namkubali Putin lakin hapa ameanza kunifelisha.
Hana tofauti na wengine Kama akina Lukashenko.
Siku moja alihojiwa akasema hawezi kuongeza mda madarakani. Lakini sa anafanya Nini. Mpumbavu fala
Akufelishe vipi !? Wakati yupo kwaajili ya maslahi mapana ya nchi
 
Ni wapi ulisikia ama ni nani alikuambia kuwa dikteta hawezi kupigiwa kura?

Pia ni wapi uliposikia kuwa udikteta ni kukaa muda mrefu madarakani?

Hizo ni hoja nyepesi mno kutokana na wewe kushindwa kuelewa maana halisi ya udikteta.

Tafuta kujua kwanza maana halisi ya udikteta na jinsi unavyofanya kazi.
 
Hahaha wewe jamaa .. Unaleta vituko sasa kumbe unaleta udini katika masuala ya utawala
mkuki kwa nguruwe! udini uko ndani yetu sote tunaukandamiza tu! nyie kwanini mnataka kuibaka katiba? udini mnao nyie! ni haki yetu kusema msitufunge mdomo! ingekuwa ni mwislam mkwere anataka kuongeza muda mngekubali?
 
Uliwahi kuona wapi dikteit anachaguliwa kwakupitia kura ?!
 
Sasa habari umeangalia aljazeera sawa hii. Habari aliyoleta mtoa mada amei copy BBC ... How come una muambia kuwa aimalizie wakati vyombo vilivyo tumika kutoa habari za puttin ni vyombo viwili tofauti ...!!?
kila mtu ana haki kuangalia habari za chombo cha nje anachopenda wewe lazima umesoma st open university swali moja jibu moja tu la mwalimu! mtabaki maskini bongo hadi mwisho wa dunia! nani kakwambia BBC ni Mungu sote tumfuate?
 
Mkishampata mtu sahihi (kwa mujibu wa wapiga kura) mnaendelea naye hadi afe au achoke kufikiri.

Katiba ya Marekani haikuwa na ukomo wa mihula kwa Rais ila Washington (Rais wa kwanza) aliweka utamaduni wa mihula miwili ambao ulifuatwa na marais 31 waliomfuatia.

Miaka 114 baadae akapatikana mwamba FDR (Rais wa 32) akawakosha wamarekani,wakamchagua mihula minne hadi akafia madarakani.

Alipokufa tu Roosevelt akaingia Harry Truman ghafla tu yakafanywa marekebisho ya katiba kuweka ukomo.

Why ukomo kwa Truman akiwa hajamaliza hata ile awamu iliyoachwa na FDR?

Mbona huo mchakato haukuwepo kipindi FDR akiwa hai?
 
nisaidie maana ya udikteta mkuu na namna unafanya kazi!
 
nisaidie maana ya udikteta mkuu na namna unafanya kazi!
Udikteta ni mfumo wa kiutawala ambapo mtu mmoja ama kikundi cha watu wachache kinamiliki mamlaka au madaraka 'yote' ya nchi bila mipaka ya kikatiba.

Msingi mkuu hasa wa udikteta ni katika 'mamlaka yote' au kwa lugha nyingine 'absolute power' na haijalishi kiongozi huyo aliingia mamlakani kwa mapinduzi, kurithi nafasi ya uongozi ama kwa kura za wananchi.

Pia, udikteta si katika kukaa muda mrefu madarakani bali ni jinsi ambavyo mgawanyiko wa madaraka katika nchi ulivyo. Uongozi unaweza kuwepo muda mchache tu madarakani na ukawa na sifa kamili za udikteta.

Katika udikteta, huo mgawanyiko wa kimadaraka ama kwa lugha nyingine 'separation of power' haupo kwa maana ya kwamba mamlaka zote za nchi katika masuala ya utungaji wa sheria (bunge), utafsiri wa sheria (mahakama), dola n.k. ziko katika udhibiti wa kiongozi mmoja wa juu (dikteta) ama kikundi cha watu wachache.
 
Kila siku mnautaftia udikteita sura Mpya kwamaslahi yawamagharibi

Hakuna dikteita anaechaguliwa kupitia kura ila anaweza akawa dekteita baada yakuchaguliwa hapa nakubali ila katika mchakato wakumpata dikteita kura haina nafasi.....
 
Ndio unihabarishe wapi na lini natoka lini dikteita akachaguliwa kwakupigiwa kura.....

Kama ndio hvyo dikteita anapigiwa kura na asiepigiwa kura anakua nani ?!
Hilo swali umeuliza sababu bado haujaelewa vyema kuhusu udikteta.

Elewa kwanza kuhusu udikteta.
 
Kila siku mnautaftia udikteita sura Mpya kwamaslahi yawamagharibi

Hakuna dikteita anaechaguliwa kupitia kura ila anaweza akawa dekteita baada yakuchaguliwa hapa nakubali ila katika mchakato wakumpata dikteita kura haina nafasi.....
Udikteta hauna sura mpya wala tofauti tofauti; hauna umagharibi wala umashariki ama ukusini wala ukaskazini. Udikteta ni udikteta tu!

Rudi katika historia upate kujua udikteta ulivyoanza pia fuatilia taarifa za habari hasa chaguzi za nchi mbalimbali na michakato ya kuongeza muda wa madaraka.

Hiki kinachofanyika Urusi hivi sasa si kitu kipya, kimekwisha kufanyika hapo awali na kama unaamini sana katika kura, tambua kuwa hata hizo kura zinaweza pia kuchakachuliwa na kiongozi akaonekana ameshinda kwa asilimia hata 99.98 wakati alichokifanya ni kucheza tu na namba.

Zinduka!
 
kati
ya USA na urusi ni nani anaongoza kwa maovu.... ni nchi ngapi usa kavamia na hakuwa na ushahidi wa kutosha kuwa nci hzo ni za kidokteta au znamiliki nyuklia
 
kati
ya USA na urusi ni nani anaongoza kwa maovu.... ni nchi ngapi usa kavamia na hakuwa na ushahidi wa kutosha kuwa nci hzo ni za kidokteta au znamiliki nyuklia
pointi nzuri sana ila pia uovu wa USA haufuti uovu wa Russia! yaani uhalifu wa mtu mmoja si kigezo cha wewe nawe kuwa mhalifu mnahukumiwa wote tu!
 
Uoga.
Ukitawala nchi vibaya huku ukijua kuwa umejijengea chuki dhidi ya wananchi walio wengi unajikuta umeshakuwa mwoga kuishi bila madaraka.
Uoga huu ndiyo hupelekea mtu kutaka kung'ang'ania madaraka kwani unahisi pindi ukiwa umestaafu na pengine uliowaudhi ndio wako madarakani basi waweza chukuliwa hatua kali.

Ushauri: Tenda mema unapokuwa umeshika rungu ili siku ukimkabidhi mwenzio usiwe na wasiwasi wa maisha. Huu mtindo wa kubadili katiba na kujifanya wewe ni wa muyaya huwa hauna mwisho mzuri. Utakuja udhalilike uzeeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…