Kila mtu kwa sasa anajua Russia imechoka na kachapika vibaya, ground battle tayari Russia ilishapoteza toka kitambo, alikuwa anategemea air forces ambazo kwa sasa zimepukutishwa kwa zaidi ya 50%. Msaada wa mitambo ya kivita ambayo Ukraine wameipata kutoka USA imemvuruga Russia kupita maelezo.
Majimbo yote manne ambayo Russia ilitangaza kuyatwaa huenda ndani ya miezi mitatu ijayo yatakuwa mikononi mwa Ukraine.
Kwa sasa Russia ni bora ikaelekeza nguvu zake kuidhibiti Crimea, maana vita ya Ukraine chimbuko lake ni huko na hitimisho lake huenda likawa huko huko.