Urusi yaituhumu idara ya Ujasusi ya Uingereza MI6 kuunda kikundi cha mauaji kutoka Ukraine dhidi ya viongozi wa Afrika wanaoshirikiana na Russia

Urusi yaituhumu idara ya Ujasusi ya Uingereza MI6 kuunda kikundi cha mauaji kutoka Ukraine dhidi ya viongozi wa Afrika wanaoshirikiana na Russia

Nilikuwa nafanya makosa Sana kuwashabikia wamagharibi hawa jamaa sio watu kabisaa
.
IMG_20230814_163442.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa akili ya kawaida ambayo hauhitaji uwe na PhD, Ukraine kipindi hichi yupo vitani na Urusi,anaweza kusumbuka kupeleka wanajeshi nje ya nchi wakati wenyewe wapo kwenye changamoto?
Nakumbuka Ukraine walikuwa na wanajeshi walinda amani nchini DRC ambao walikuwa sehemu ya vikosi vya umoja wa mataifa.Baada ya vita na Urusi kuanza wale wanajeshi walirudishwa Ukraine.Leo Ukraine wapeleke wanajeshi wao nje ?
Putin angetunga uongo mwingine lakini sio huu🤔
Imejen!!.
Et, makomando mia 1 wa kuua viongozi wa Africa!!
Nchi 54, ulete makomando 100 wa kuua Marais wa hizo Nchi!!.

Ukiamini Urusi inachokisema basi upo kwenye levo ya kuamini chochote kile.
 
Kwa akili ya kawaida ambayo hauhitaji uwe na PhD, Ukraine kipindi hichi yupo vitani na Urusi,anaweza kusumbuka kupeleka wanajeshi nje ya nchi wakati wenyewe wapo kwenye changamoto?
Nakumbuka Ukraine walikuwa na wanajeshi walinda amani nchini DRC ambao walikuwa sehemu ya vikosi vya umoja wa mataifa.Baada ya vita na Urusi kuanza wale wanajeshi walirudishwa Ukraine.Leo Ukraine wapeleke wanajeshi wao nje ?
Putin angetunga uongo mwingine lakini sio huu🤔
Mkuu, hivi Ukraine waichukuliaje?

Ukraine ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Ulaya baada ya Russia.

Yaani kikosi cha watu 100 ni vigumu kukitayarisha na special missions?
 
Imejen!!.
Et, makomando mia 1 wa kuua viongozi wa Africa!!
Nchi 54, ulete makomando 100 wa kuua Marais wa hizo Nchi!!.

Ukiamini Urusi inachokisema basi upo kwenye levo ya kuamini chochote kile.
Kwani ni lazima utambue kama wote wapo Afrika?

Unafahamu namna hizi operesheni zinavyofanywa usidhani kwamba utakuja kufahamu ni leo au kesho.

Ndo maana kuna kikosi maalum na chaweza kufanya kazi zake kwa miaka kadhaa na kwa mbinu tofautitofauti.

Na pia si nchi zote 54 zahusika ni baadhi ya nchi za Afrika zilizo na ukaribu na Russia au kuonyesha kuiunga mkono waziwazi.
 
Russia imeituhumu idara ya ujasusi wa nje ya Uingereza ya MI6 kuhusika na mpango wa kuunda kundi la wauaji au "Assassination Squad" ambalo kazi yake kuu itakuwa ni kuharibu miundombinu na kufanya mauaji ya viongozi wa nchi za Afrika ambao watakuwa wakishirikiana na Russia kiuchumi na kidiplomasia.

Shirika la habari la Russia limekariri chanzo cha kuaminika cha kijeshi kuwa Uingereza iliiomba Ukraine iandae kundi hilo la kufanya mauaji au "assassination squad" ambalo litakuwa na watu wapatao 100 ambao kazi yao kuu itakuwa ( kwa maagizo ya nchi za magharibi) kufanya uharibu wa miundombinu na mambo mengine yaani "sabotage" pamoja na kufanya mauaji ya viongozi wa nchi za Afrika ambao wameonyesha misimamo kuhusu kushirikiana na Russia kijeshi, kidiplomasia na kibiashara.

Chanzo hicho cha Tass ambacho inaaminika ni kutoka idara ya ujasusi wa kijeshi ya Russia ya GRU kimesema lengo kuu la operesheni hiyo itakuwa ni kuzuia nchi za Afrika kushirikiana na Russia kwa namna yoyote ile.

Mwezi ulopita Russia iliwakaribisha viongozi kadhaa wa nchi za Afrika mjini St Petersburg ambapo nchi hizo ziliahidi kushirikiana na Russia na pia kuahidiwa na Russia kupata msaada wa ngano bure. Kati ya nchi hizo nchi sita zilitoa tamko la kupinga azimio la Umoja wa Mataifa la kupinga uvamizi wa Russia kwa Ukraine.

Pia kwa muendelezo huo wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Russia kikundi cha askari wa kukodiwa cha Wagner kimekuwa ni sehemu ya majeshi ya nchi za Mali, Burkina Faso, Guinea na sasa Niger katika eneo la Sahara.

Katika mashinikizo yake kwa nchi za Afrika na kuwa kutumia nguvu yake ya pesa nchi za Magharibi zimeweza kuushawishi umoja wa kiuchumi wa nchi za magharibi wa ECOWAS kuhakikisha waunda jeshi la pamoja ambalo litaweza kuivamia nchi ya NIger kwa ajili ya kuirudisha madarakani serikali ilopinduliwa na jeshi ya raisi Mohamed Bazoum.

Wiki chache zilizopita jeshi la Niger likiongozwa na mkuu wa kikosi cha kumlinda raisi Omar Tchieni lilitanganza kufanya mapinduzi na kuondoa katiba ya nchi hiyo kisha baadae kutangaza baraza la mawaziri baadhi yao wakiwemo mawaziri wa zamani katika serikali ya raisi aliepita bwana Mahamoudou Issoufou.

Madai ya Russia juu ya kuundwa kwa kundoi la mauaji dhidi ya viongozi wa Afrika ni madai ambayo ni very serious na yaopaswa kuchukuliwa kwa uzito wake hususan katika kioindi hichi ambapo viongozi wengi wa bara hili wamegawanyika juu ya mgogoro wa Russia. ECOWAS ni umoja ambao umekuwa ukipokea fedha nyingi kutoka nchi za magharibi fedha ambazo nyingi huishia mifukoni mwa viongozi hao kwa kufanya vikao visivyoeleweka.

Hivi sasa pia kumetokea mgawanyiko ndani ya ECOWAS juu ya uamuzi wa kuunda jeshi la pamoja ambalo kwa msaada wa nchi za Ufaransa na Marekani wa kutumia vyombo ya satelite na ndege zisizo na rubani litaweza kuivamia Niger kijeshi na huku wakti huohuo NIger ikiwa imepokea msaada wa kijeshi kutoka katika kundi la Wagner, Korea Kaskazini pamoja na nchi za Mali na Burkina Faso ambazo nazo zimeweka tayari majeshi yake kuisaidia Niger.

Mgogoro wa Russia na Ukraine na matukio yanoendelea ya Niger pamoja na madai ya Russia kuhusu kuundwa kwa kundi la mauaji dhidi ya viongozi wa Afrika ni uthibitisho rasmi kwamba sasa hivi bara la Afrika ni uwanja wa mapambano baina ya mataifa makubwa yalogombani rasilimali barani humo na pia ni kipimo cha akili na fikra za viongozi wetu wa kiafrika ambao hivi sasa wapo kwenye mtihani mkubwa.

Kulikuwa na mkutano wa Berlin mwaka 1884 hadi 1885 wa kuligawa bara la Afrika baina ya mataifa ya magharibi uliotishwa na Kansela Bismark lakini sasa hivi hakuna mkutano wa aina hiyo na kila nchi ya Afrika ijitafakari upya.

Mara hii kama ilivyokuwa kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia bara la Afrika limejikuta tena katikati ya viya ya Russia na Ukraine. Bara la Ulaya limeazimia kutoliachia bara la Afrika na uzalishaji wake wa rasilimali kuu na malighafi ambazo zahitajika sana huko Ulaya na Marekani. Halikdhalika Russia na China nao wameazimia kutoliacha bara hili na kulipoteza hivyo kukosa raslimali zake muhimu hususan madini ya Urainium na gesi asilia.

Uchambuzi huu umetumia vyanzo mbalimbali kama shirika la habari la Russia-Tass, Sky news, kijarida cha Spytalk na Bloomberg Surveillance.
Putini aache chokocho na kujifanya na mapenzi na Africa, kama anawapenda Africa apeleke miradi mikubwa ya maendeleo Africa kama walivyoweza Magharibi na US ambapo miradi yote inayotekelezwa 80% inafadhiliwa na magharibi na US.,

Putini ameshindwa kupeleka umeme wa kudumu South Africa wanalala gizani na huyu ni M-Brics mwenzake tena founder analala gizani.
 
Mkuu, hivi Ukraine waichukuliaje?

Ukraine ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Ulaya baada ya Russia.

Yaani kikosi cha watu 100 ni vigumu kukitayarisha na special missions?
Wanajes
Mkuu, hivi Ukraine waichukuliaje?

Ukraine ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Ulaya baada ya Russia.

Yaani kikosi cha watu 100 ni vigumu kukitayarisha na special missions?
Wanajeshi 100 tena ambao ni special forces ni wengi Sana kwenye battlefield.Manake huwezi kupeleka wanajeshi wa kawaida kwenye special mission🤔
Kuliko kupelekwa kwingine wangepelekwa frontline kumpelekea moto mvamizi.Vinginevyo Putin atuambie kuna kila dalili Ukraine wanashinda vita dhidi ya Urusi!
 
Back
Top Bottom