HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Urusi imeutaja uanachama wa Finland katika jumuiya ya Kujihami ya NATO kuwa ni uvamizi dhidi ya usalama wake na kusema itachukua hatua za kiufundi na kimkakati
Urusi imeutaja uanachama wa Finland katika jumuiya ya NATO kuwa ni uvamizi dhidi ya usalama wake na kusema itachukua hatua.
Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi habari mjini Moscow kwamba hatua hii ni shambulizi dhidi ya masilahi ya Urusi na wanalazimika kuchukua hatua za kiufundi na kimkakati bila kutoa maelezo zaidi.
Finland imejiunga na NATO leo na kuwa mwanachama wa 31 wa muungano huo wa kijeshi.
Katika taarifa tofauti wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema kwa kujiunga na NATO, Finland imejipoteza yenyewe na uhuru wowote ilionao.
Wizara hiyo pia imesema hatua zaidi za Urusi zitategemea kanuni za NATO kuijumuisha Finland ikiwa ni pamoja na upelekaji wa miundombinu ya kijeshi na mifumo ya silaza za mashambulizi katika himaya yake.