HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema pendekezo la kuhamisha makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka New York hadi nchi nyingine ni wazo zuri na linafaa kuzingatiwa.
Sergei Lavrov, ambaye yuko mjini New York, amewaambia waandishi wa habari kando ya mkutano usio rasmi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: "Itakuwa vyema sana ikiwa Umoja wa Mataifa utahamisha makao yake makuu kutoka New York na kuupeleka mahali pengine popote".
Kuhusiana na suala hilo, Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Kremlin, amesema wazo la kubadilisha makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka New York hadi nchi nyingine linaweza kutathminiwa.
Akizungumzia tatizo la utoaji viza linalosababishwa na Marekani kwa jumbe za kidiplomasia na timu za vyombo vya habari vya nchi mbalimbali, msemaji huyo wa Kremlin amesema: Russia haiko peke yake katika tatizo la utoaji wa viza unaokwamishwa na Marekani ikiwa ni mwenyeji katika Umoja wa Mataifa.
Kuhusu hatua ya kutowapatia viza waandishi wa habari wa Russia wanaokusudia kwenda kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa, Peskov amesisitiza kwa kusema: "hili ni suala linalohitaji majadiliano mazito na nchi ambazo, nazo pia zinalalamikia vikali suala hili".
Kabla ya hapo, waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov aliielezea kuwa ni ujinga hatua ya Marekani ya kukataa kutoa viza kwa waandishi wa habari wa Russia.