Urusi yapendekeza makao makuu ya UN yaondolewe Marekani na kuhamishiwa nchi nyingine

Urusi yapendekeza makao makuu ya UN yaondolewe Marekani na kuhamishiwa nchi nyingine

View attachment 2599432

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema pendekezo la kuhamisha makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka New York hadi nchi nyingine ni wazo zuri na linafaa kuzingatiwa.

Sergei Lavrov, ambaye yuko mjini New York, amewaambia waandishi wa habari kando ya mkutano usio rasmi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: "Itakuwa vyema sana ikiwa Umoja wa Mataifa utahamisha makao yake makuu kutoka New York na kuupeleka mahali pengine popote".

Kuhusiana na suala hilo, Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Kremlin, amesema wazo la kubadilisha makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka New York hadi nchi nyingine linaweza kutathminiwa.

Akizungumzia tatizo la utoaji viza linalosababishwa na Marekani kwa jumbe za kidiplomasia na timu za vyombo vya habari vya nchi mbalimbali, msemaji huyo wa Kremlin amesema: Russia haiko peke yake katika tatizo la utoaji wa viza unaokwamishwa na Marekani ikiwa ni mwenyeji katika Umoja wa Mataifa.

Kuhusu hatua ya kutowapatia viza waandishi wa habari wa Russia wanaokusudia kwenda kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa, Peskov amesisitiza kwa kusema: "hili ni suala linalohitaji majadiliano mazito na nchi ambazo, nazo pia zinalalamikia vikali suala hili".

Kabla ya hapo, waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov aliielezea kuwa ni ujinga hatua ya Marekani ya kukataa kutoa viza kwa waandishi wa habari wa Russia.
Wamewakomesha waandishi wa habari wa taifa la kipuuuzi la russia. Asilimia kubwa ya waandishi wa habari ni makachero tuuu
 
..catch ni money [emoji383] [emoji857] [emoji389]!,USA inachangia almost 35%ya kuendesha hii UN!,itahamishiwa nchi gani itakayokua na uwezo to bankrolls UN?,tujiulize Tanzania tunadaiwa kiasi gani cha michango yetu kule SADC, AU, na UN, then tujadili hoja hii kisayansi

Kwasabu UN ni kichaka chake.
 
Hili niliwahi kulisema miaka kadhaa iliyopita baada ya US kuzidisha misbehaving!!! Bora, Russia wameuona ukweli!!!
 
vipi bush na wenzie ulaya wanawalipa iraq sirya afghanistan kwa uvamizi wao au hizo habar ni za kale 19878 huko
Akili zako zimefikia hapo? Kwanini Russia hakuwa-army hizo nchi mbele ya USA the way USA wanavyofanya kwa Ukraine???
 
Naunga mkono hoja, lakini pia nchi hiyo itakayopewa Makao Makuu ijitolee kuwa mchangiaji Mkubwa wa umoja huo kama inavyofanya sasa Marekani.
Nani hata Russia hawezi thubutu USA ni level nyingine labda wajinga na waliochanganyikiwa kama akina Putin wanaosakwa kwa kuiba watoto huko, ni ngumu kuhamisha UN pale NY kama dollar tu kushusha tizi je UN wataweza?? labda madikteta waanzishe UN yao but not kuhamiha UN headquater bro!
 
we nae unaishi dunia ipi inaonekana umekurupuka ......em tafuta tafuta basi hata mitandaoni ili ujue lavrov kaenda fanyaje na kwa sasa hivi russia ni nani katika hilo baraza kaa mwezi huu
Nilimuona nikataka kumwelimisha lkn yupo bd sana!
 
Nani hata Russia hawezi thubutu USA ni level nyingine labda wajinga na waliochanganyikiwa kama akina Putin wanaosakwa kwa kuiba watoto huko, ni ngumu kuhamisha UN pale NY kama dollar tu kushusha tizi je UN wataweza?? labda madikteta waanzishe UN yao but not kuhamiha UN headquater bro!
Nami nilimaanisha hivyo. Kuna wengine wanafikiria kuhamisha tu bila kuangalia mambo mengine. Na hata hilo wazo la Urusi limechukuliwa kama mzaha tu!
 
Weee! Aliye muuwa Gaddafi alishtakiwa wapi? Aliyemuuwa Sadam Husen alishtakiwa wapi? Na uharibifu wa nchi hizo nani analipia? Je uvamizi wa nchi kamaa Syria, Afghastan na kwingineko nani alaumiwe na kushtakiwa? Mbona hapo Sudan hivi sasa hapakaliki vita kali na wao hao wanaojiona wanaustaarabu wanaondoka na kuacha machafuko?
Gaddafi aliuawa na wananchi wake na Saddam vilevile aliuliwa na wairaq wenzake kwa kuliwa kitanzi, hivyo usitake kutudanganya. Ushahidi wa matukio yote hayo upo.
 
Hapo kabla nilidhani ukubwa wa michango unatoka na ukubwa wa uchumi wa nchi husika kumbe kwa sababu ya ku host Makao Makuu.

Na AU nasi tuige huu utaratibu Makao tuyapeleke NIGERIA au SOUTH AFRICA.
 
Back
Top Bottom