Urusi yapokea msaada wa silaha kutoka kwa waasi wa Iraq, kwa kupitia Iran - hali mbaya

So mzee unahisi Russia anatoboa kabisa kwenye hili against the western countries
Russia anaweza akafanikiwa endapo western wakaamua iwe hivyo, lakini wasipoamua ni ngumu Russia kuibeba Ukraine. Vita vya kisasa ni pesa, huwezi kupambana pasipo pesa. Nchi za magharibi zina pesa chafu mno.
 
Russia anaweza akafanikiwa endapo western wakaamua iwe hivyo, lakini wasipoamua ni ngumu Russia kuibeba Ukraine. Vita vya kisasa ni pesa, huwezi kupambana pasipo pesa. Nchi za magharibi zina pesa chafu mno.
Na huo ndiyo ukweli wenyewe,Warusi n watu wa ajabu Sana Yani upigane na western countries ushinde kweli?Hao jamaa ndo wanaendeaha mifumo yote ya uchumi Duniani hivo Wana Kila kitu .Putin akubali yaishe tu Kwa Sababu mwisho wa siku ataumiza Sana nchi yake na huo utakua mwisho wake kama kiongozi wa Russia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha maneno tuoneshe silaha alizo pewa masaada na china.
 
Sasa mara ya ngapi anashinda, Mbona kwa Mariopo hawaja amua asishinde...?, wawafate mateka wao tuone huo uwezo, Crimea ilienda walifanya nn zaidi ya kumtoa G8, kama sijakosea.
Acheni porojo zenu bana.
 
Baada ya ku post habari hii unalipwa sh ngapi?
 
Mkubwa anaazilika huko😂
 
Mtoa mada inaonekana Ni mkenya ila hata kingereza hujui,

Tangu lini Kitu Cha ku"Smuggle" kikawa official Kama ulivoandika kwenye heading

Wapi nimetumia neno official, mpaka sasa kila anayempa Putin msaada anafanya kwa siri maana mauaji aliyofanya ya kimbari yamempotezea points nyingi hadi hana uungwaji mikono wa moja kwa moja, hata China walitoa tamko juzi wakasema litafutwe suluhu la huu ugomvi, walitumia maneno ya kiufundi ila ni wazi na wao wamemchoka.
 
Leo watu wanasifu kuwa uchumi wa Russia bado uko strong licha ya vikwazo vyote, mtu mpaka unajiuliza hivi wana akili timamu kweli? Sanctions zote hizi bado zimuache mtu vile vile kama alivyo?

Wanafika mbali na kusema Ulaya inaumia zaidi, wanaona kama vile US na Ulaya imekurupuka juu ya maamuzi yao. Kitu pekee ninachoona ni kuwa, Westerns wana propaganda saana, wanaweza wakalia wakasema wana njaa ukadhani kweli njaa imewapiga haswa, kumbe walaa kawaida tu.

Hii vita kuna namna anavyotafutwa mtu, ni suala la muda tu. Kwa bahati mbaya saana, ni kosa la jinai vyombo vya habari Urusi kuzungumza kitu negative kuhusiana na mzozo huu la sivyo tungefahamu mengi.
 
Vp NATO uliwajumuisha kwenye hiyo dhahania yako au la? Tuanzie hapo kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…