Yuko sahihi kabisa. Urusi inapigana kuyaleta maeneo ya asili ya warusi kwenye shirikisho la urusi.
Nchi za magharibi waache unafiki. Walipounga mkono kusambaratika shirikishi la yugoslavia kila kabila kua nchi walifikiri dunia haioni? Licha ya wayugoslavia kua mbari moja ya ki slav. Wakawatenga wa croatia na wa serbia, wakawatenga wa montenegro na wa serbia, wakaitenga cossovo na serbia etc etc yogoslavia ikasambaratika. Yote lengo likiwa kulivunja taifa lililojengwa kwa msingi wa kijamaa na taifa rafiki na urusi.
Leo hii tunaona tena marekani ikifunga kibwebwe kwa nia ya kuichoma kisu urusi. Kujaribu kuizingira kwa kuwageuza ndugu wa asili wa urusi kua maadui zake. Kwa hilo maeneo ya ukraine ya kabila la kirusi wamesema hapana na urusi iko tayari kuwasaidia kuungana na nchi yao shirikisho la urusi.