Urusi yaunda jeshi baada ya kuazimia kukalia moja kwa moja mikoa ya Ukraine iliyoiteka

Urusi yaunda jeshi baada ya kuazimia kukalia moja kwa moja mikoa ya Ukraine iliyoiteka

Biden ameshaacha kusalimia vivuli?
Dish limeshacheza uyu nyumbu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
IMG_20220914_163726_627.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kupata kipigo kizito kwenye uwanja wa vita Sasa wameamua kujificha kwenye kichaka Cha referendum
Referendum ni mbinu ya kupata wapiganaji ila mwamba nguvu zimeisha mimi pia nililua namwamini sana ila katutia aibu bora asingepigana hao Ukraine kwao pana vita wengine walikua DRC Kongo wametoka wiki iliyopita kama wanajeshi 250 inaonekana Ukraine ni mabingwa wa vita vya ardhini na hapo Urusi anapigwa maeneo aliyovamia na kuonekana kushindwa angekua anapigwa kwake nae ingekua habari ingine..
 
Limeshindwa jeshi, ndo mgambo wataweza?.

Putin anapeleka raia wake kuuliwa bila sababu!
Kama raia wanauliwa mbona bado anayakalia maeneo aliyoyachukua?? Na je mlipotuambia Russia wamefurushwa Kherson mbona nao wanapiga kura? Je wanapiga kura wakiwa chini ya Ukraine? 😄😄😄😄 fungua macho na akili wewe
 
Inachekesha na kustaajabisha mno kweli. Yaani Putin na uzee wake, vita aliyoianzisha mwenyewe imemchanganya akili hadi amefikia hatua ya kuzoa-zoa watu anawakusanya toka mitaani alimradi tu wavae kombat na kuwapa vijikaratasi vya utambulisho eti ni wanajeshi wa Urussi. Mbona analidhalilisha mno jeshi lake mwenyewe? Nadhani Huyu jamaa afungwe tu kamba sasa kwani ameshakuwa ni kichaa kamili. HIMARS umenena sawasawa. Mtindo Ni kuweka "Full Bust" na magazine ziwe 3 full loaded kwani kazi itakayokuwapo hapo ni ya kuua tu hata kama umefumba macho -unaminya trigger tu hakuna hata cha shabaha. Aisee! hiki ni mojawapo ya vituko vya Wakubwa duniani.
......Amesema kuwa raia wote ambao watakusnywa watakuwa na hadhi kamili ya jeshi
Sio watu wanazolewa mitaani, ni wale wapigani wa hayo maeneo wanaopambana kujitenga na UKRAINE. Taarifa imeeleweka ila ww unahisi wanakuja kwenu hapo Mbalizi wanakuchukua ukapigane tu.
 
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kukusanya wanajeshi wa ziada kwa ajili ya vita nchini Urusi - kulingana na shirika la habari linalomilikiwa na serikali TASS.

Anasema kuwa nchi za Magharibi zimeonyesha kuwa lengo lake ni kuiangamiza Urusi na kwamba zimejaribu kuwageuza watu wa Ukraine kuingia kwenye vita kwa lazima.

Lengo letu ni kuikomboa Donbas, anasema.

Rais Putin anasema nchi za Magharibi zimeonyesha kuwa hazitaki amani kati ya Ukraine na Urusi.

Putin pia anasema kuwa atatoa hadhi ya kisheria kwa ‘’wanaojitolea’’ wanaopigana huko Donbas.

Putin ametangaza kuwa kuanzia leo ni muhimu kuchukua uamuzi wa haraka ili kulinda watu katika ‘’ardhi zilizokombolewa’’.

“Ndiyo maana niliiomba wizara ya ulinzi kukusanya jeshi kwa ajili ya vita,” anasema.

Amesema agizo hilo tayari limetiwa saini na linaanza kutekelezwa leo.

Amesema kuwa raia wote ambao watakusnywa watakuwa na hadhi kamili ya jeshi.

Putin ameongeza kuwa nchi za Magharibi zimekuwa zikiichafua Urusi lakini Urusi ina silaha nyingi za kujibu.

“Tutatumia rasilimali zote tulizonazo kuwatetea watu wetu,” anasema.

‘’Nina imani na msaada wako,’’ anahitimisha.

==============
Ikumbukwe mikoa anayoikalia ndio yenye utajiri wa viwanda, gesi, madini na mashamba ya Ngano.

Ukraine amepoteza pakubwa sana. Sasa ni mwendo wa kulinda alichojitwalia

#chanzobbcswahili
#StarTvUpdate

View attachment 2363393
Mikwara mbuzi
 
mzee ameangukia pua hili halipingiki kukusanya raiya mitaani wakalinde maeneo waliyoteka nyara ni ishara ya kuangikia mdomo kama wanajeshi walio na mafunzo hawakuwa na morali vipi kwa raiya ...
 
Umesema Ukraine "wasiyachukue"?? Hata wasiposhawishiwa bado Ukraine hawana uwezo wa kuyarudisha maana hawakugawiwa waliyachukua kwa nguvu na watatumia nguvu kuyalinda
Urusi kashindwa Vita ana siraha za zamani tuu na pia hana nguvu kazi ndio maana anaomba msaada China na India nimesikia Turkey nae anataka kujiunga ila juzi tuu hapa alipata msaada Nchi yao ilipopata matatizo ya Uchumi..
 
Referendum ni mbinu ya kupata wapiganaji ila mwamba nguvu zimeisha mimi pia nililua namwamini sana ila katutia aibu bora asingepigana hao Ukraine kwao pana vita wengine walikua DRC Kongo wametoka wiki iliyopita kama wanajeshi 250 inaonekana Ukraine ni mabingwa wa vita vya ardhini na hapo Urusi anapigwa maeneo aliyovamia na kuonekana kushindwa angekua anapigwa kwake nae ingekua habari ingine..
Kweli kabisa, huwezi kufanikiwa kwa kuvamia ardhi ya mwenzio

Urusi anajaribu kushindana na nature
 
Back
Top Bottom