KERO Us dollar bado inatufinya wapangaji wa maeneo prime area Dar

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Issue hii kama haikugusi huwezi ona shida ambayo Serikali imeacha bila kushughulikia,ilipaswa wasimamie Kwa kupiga marufuku mikataba ya dolla nchini. Shida wao ndio wamiliki wa majengo yenye mikataba ya Dollar
Ni lzm uishi maeneo hayo ?
 
Very true
 
Hivi kuna mtu wa kawaida anayemiliki nyumba Masaki, Mikocheni etc? Ukweli ni kwamba wanaofaidika ni watunga sera waliouziana nyumba za serikali mitaa hiyo, those days

Ni kama huu utaratibu wa kulipa rent kwa mwaka..hivi kweli kama usipokuwa mwizi, how do you get money kulipa rent ya mwaka mzima? especially kwa vijana wanaojitafuta bado hapa mjini? Lakini kwa sababu wakubwa hili haliwagusi...siyo kipaumbele kwao. Na hawa wapiga kula.....wako kwenye usingizi pono baada ya kuuliza maswali magumu kwa wawakilishi wao....

Sidhani kwa siasa na uongozi tulionao wanaweza kutatua hizi changamoto tulizonazo.

Kulipa rent kwa dollar inaumiza. Lakini ndo uhalisia wenyewe. Hakuna mtu anaweza jenga nyumba ya million 500M halafu akupe kwa rent isiyotabirika.
 
Mdau analalamikia fluctuations ya bei ya dollar, sio malipo kwa dollar
Fluctuation hii inasababisha mtu asiwe na uhakika analipa kiasi gabi cha kodi kila mwezi na ndo kero ilipo
 
Iweke kiusahihi zaidi: … mpaka siku wananchi watakapokuwa na uelewa na nguvu kamili ya kuiwajibisha serikali kidemokrasia.

Hiyo ndiyo namna pekee ambayo kwayo wananchi tunaweza kujihakikishia kuwa na serikali na uongozi makini katika masuala yote ya nchi.

Nchi zilizoendelea viongozi wanachaguliwa na kuondolewa madarakani bila simile kwa kuangalia viashiria vya uchumi (economic indicators): thamani ya pesa, viwango vya riba, mfumuko wa bei, ongezeko la kodi na tozo mbali mbali, sera za biashara, n.k.

Sisi huku viongozi wanajinasibu kwa ongezeko la madarasa, mabweni, matundu ya vyoo, majengo ya vituo vya afya, kuanza safari fupi za SGR, madege uwanjani, huku huduma mbovu zimatamalaki kwenye shule, vyuo, hospitali, usafiri, sekta ya biashara, n.k. Tunasikitisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…