KERO Us dollar bado inatufinya wapangaji wa maeneo prime area Dar

KERO Us dollar bado inatufinya wapangaji wa maeneo prime area Dar

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Issue hii kama haikugusi huwezi ona shida ambayo Serikali imeacha bila kushughulikia,ilipaswa wasimamie Kwa kupiga marufuku mikataba ya dolla nchini. Shida wao ndio wamiliki wa majengo yenye mikataba ya Dollar
Ni lzm uishi maeneo hayo ?
 
Hapo sioni kama kuna namna nyingine yeyote ile zaidi ya kumbembeleza landlord wako akuonee huruma.

Hata huyo kuweka rent in US dollar ni kwa vile anajua hii shilingi yetu, kutokana na mifumo yetu mibaya ya uchumi, haitabiriki, na anaweza siku moja akaishia kulipwa pesa isiyoweza hata kutengeneza choo kikiharibika.

Watanzania tutaendelea na haya matatiźo mpaka siku tutakapowapata watu wenye uwezo wa kusimamia vizuri uchumi wa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Very true
 
Hivi kuna mtu wa kawaida anayemiliki nyumba Masaki, Mikocheni etc? Ukweli ni kwamba wanaofaidika ni watunga sera waliouziana nyumba za serikali mitaa hiyo, those days

Ni kama huu utaratibu wa kulipa rent kwa mwaka..hivi kweli kama usipokuwa mwizi, how do you get money kulipa rent ya mwaka mzima? especially kwa vijana wanaojitafuta bado hapa mjini? Lakini kwa sababu wakubwa hili haliwagusi...siyo kipaumbele kwao. Na hawa wapiga kula.....wako kwenye usingizi pono baada ya kuuliza maswali magumu kwa wawakilishi wao....

Sidhani kwa siasa na uongozi tulionao wanaweza kutatua hizi changamoto tulizonazo.

Kulipa rent kwa dollar inaumiza. Lakini ndo uhalisia wenyewe. Hakuna mtu anaweza jenga nyumba ya million 500M halafu akupe kwa rent isiyotabirika.
 
Serikali ilishapiga marufuku, ndio maana nasema, kama wewe umelazimishwa mktataba wa dola, mripoti anomimously landlord wako.

Mie ninachoelewa ni kwamba landlord anaweza kusema rent ni dola say 500, ila kila unapolipa rent unaweza kulipa hiyo $500 kwa equivalent ya Tshs. Sio akulazimishe ulipe in dollars. Mwambie kama anapenda dola akazinunue mwenyewe wewe utampa equivalent amount in Tshs. Ila sasa, rent yako in Tshs itakuwa inabadilika kila mwezi, kutegemea exchange rate.

Akikuletea figusu, mripoti na tafuta nyumba nyingine
Mdau analalamikia fluctuations ya bei ya dollar, sio malipo kwa dollar
Fluctuation hii inasababisha mtu asiwe na uhakika analipa kiasi gabi cha kodi kila mwezi na ndo kero ilipo
 
Hapo sioni kama kuna namna nyingine yeyote ile zaidi ya kumbembeleza landlord wako akuonee huruma.

Hata huyo kuweka rent in US dollar ni kwa vile anajua hii shilingi yetu, kutokana na mifumo yetu mibaya ya uchumi, haitabiriki, na anaweza siku moja akaishia kulipwa pesa isiyoweza hata kutengeneza choo kikiharibika.

Watanzania tutaendelea na haya matatiźo mpaka siku tutakapowapata watu wenye uwezo wa kusimamia vizuri uchumi wa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Iweke kiusahihi zaidi: … mpaka siku wananchi watakapokuwa na uelewa na nguvu kamili ya kuiwajibisha serikali kidemokrasia.

Hiyo ndiyo namna pekee ambayo kwayo wananchi tunaweza kujihakikishia kuwa na serikali na uongozi makini katika masuala yote ya nchi.

Nchi zilizoendelea viongozi wanachaguliwa na kuondolewa madarakani bila simile kwa kuangalia viashiria vya uchumi (economic indicators): thamani ya pesa, viwango vya riba, mfumuko wa bei, ongezeko la kodi na tozo mbali mbali, sera za biashara, n.k.

Sisi huku viongozi wanajinasibu kwa ongezeko la madarasa, mabweni, matundu ya vyoo, majengo ya vituo vya afya, kuanza safari fupi za SGR, madege uwanjani, huku huduma mbovu zimatamalaki kwenye shule, vyuo, hospitali, usafiri, sekta ya biashara, n.k. Tunasikitisha.
 
Back
Top Bottom