Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani,
Mimi sioni ajabu maana mengi hukanushwa na viongozi wetu na mwisho yanaonekana na wala hakuna anayeuliza.
Sasa nikisikiamipango hii sishangai. Na wala msitegemee mtu kujitokeza kusema ukweli hadhalani. Maana sana sana watakuja na utetezi kuwa hilo linahusu ni usalama wa taifa. Sijui ni usalama wa taifa gani hilo!
Kweli kazi iposasa tunajua sababu ya safariya Bush nazile dola 758 millioni kwasababu nchi zote za Afrika magharibi walikataa. Kazi ipo!!
Kamundu, hakuna anayebisha hoja yako.Swala gumu zaidi hapa ni mwendelezo wa mwenendo wa usiri usio na manufaa kwetu, unaofanywa na viongozi wetu wa ngazi zote.
Hakuna afisa wa serikali [si mtendaji wa kijiji wala waziri] anayejitokeza wazi hadharani kuwaeleza wananchi kuhusu kinachokusudiwa kukifanya kuhusu "Kigamboni City Project", lack of transparency ndiyo issue.We need to be involved.Do they have anything to hide? Probably your guess is as good as mine.
All in all, let them come as long as we are not being forced into this partnership and as long as there is strategic and mutual benefits for both sides.
Mwanzoni mwa mwezi Januari 2009, nikiwa safarini kutoka Djibouti kupitia Ethiopia kwenda Great Britain nilikutana na "agent" mmoja wa shirika ambalo siwezi kutaja jina lake, akanieleza kuwa Marekani iko katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kutaka kujenga kambi ya jeshi la majini [strategic naval base] katika eneo kuizunguka Kigamboni.
Baada ya kufika huku ughaibuni ndipo nikasikia Bw John Chiligati ametoa kauli bungeni kuhusu ardhi yetu ya Kigamboni.Tatizo ni kwamba "mwekezaji" anayetaka kuihodhi ardhi hiyo amekuwa akieleza kuwa na mpango wa kuendeleza mradi as vague as 'Kigamboni City'.Chiligati aulizwe kuhusu habari hizi, msikie atasema nini.
Mpango huo unaelezewa kuhamisha "raia" katika radius ya kilometa kumi plus, kuwezesha ujenzi wa kambi itakayokuwa extension ya United States Africa Command ambayo inazidi kupewa uzito kule Djibouti.Watafanya dredging kuongeza kina kuhimilia mikiki ya "ndonga za kivita" kama aircraft carriers na submarines.Vile vile kutakuwa na airstip kwa ajili ya midege yao mizito kama B-52.
Kisa na Mkasa
Sababu ya wanyamwezi kukita mizizi ya ubepari wao katika majabali ya Tanzania ni kwamba wanataka kuiziba China isipate kujijenga Afrika Mashariki na vile vile Afrika Kusini ambayo pia imekuwa ikiwania sana pande hiyo ya Afrika.
Naomba nisisitize kuwa sina ushahidi kuthibitisha concern hiyo, lakini viongozi wetu wanajulikana kwa ulaghai na uhujumu.Something fishy is going on behind the scenes, only time will tell.Hakuna anayejitokeza kulizungumza head-on.Wote wanapiga porojo tu, at our expense.
Consipiracy Theory
Itakumbukwa kuwa rais mstaafu wa Marekani, George W Bush, alifanya ziara "unique" nchini kwetu Februari 2008, pasipo maelezo ya kina ni kitu gani kilimfanya awe mgeni wetu kwa siku nne!
Inadhaniwa katika ziara hiyo aliamua kufika mwenyewe na makubaliano yote yafanyike katika adhi ya Tanzania, kuepusha zengwe kama la Karamagi kusaini mkataba famba hotelini jijini London.Alikamilisha mambo mengi, tuliyoambiwa ni asilimia 20 tu - mengine ni CLASSIFIED.
Je visa vya maharamia katika pwani ya Afrika Mashariki ni njama au hali halisi ya maisha ya wasomali waliokata tamaa?Tutasema nini tukiambiwa meli haziwezi tena kupita pwani ya Somalia?Je wakituambia wanataka kutusaidia tutakataa?Itakuwaje tukatae wakati bei ya mafuta itakuwa imefika shilingi 3000 kwa lita? Ah!! waache waje watukomboe bwana, japo wachache baadhi yetu tutapinga - majority ya wana JF watasema hapana, hatutaki.Lakini walioshika mpini watakuwa na maono sawa?
Mikakati
Tayari Marekani imeongeza presence yake katika nyanja mbali mbali kwetu Tanzania.Hivi karibuni wamekata mshipa wa soni kwa kuanza kusaidia kambi ya jeshi la JWTZ pale Kigamboni.
Paradox?Sijui....kinachosubiriwa ni uchaguzi mkuu wa 2010, baada ya hapo tutaanza kuuziwa longo longo kwamba hali ya usalama ni mbaya na tunahitaji uwepo wa Marekani kusaidia kujenga ngome ya ulinzi.Tutasema nini watanzania sisi, wakati haya tuliyonayo mezani ya EPA, Richmond, na kashfa za migodi madini yetu yametushinda?Ni wazi kuwa kama wamekusudia watafanikisha lengo lao, tukilazia damu.
Anyway, ningependa kueleza mengi zaidi, lakini nasita.Lakini kama tukiwa hai, mengi yatajitokeza very soon.
Mwanzoni mwa mwezi Januari 2009, nikiwa safarini kutoka Djibouti kupitia Ethiopia kwenda Great Britain nilikutana na "agent" mmoja wa shirika ambalo siwezi kutaja jina lake, akanieleza kuwa Marekani iko katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kutaka kujenga kambi ya jeshi la majini [strategic naval base] katika eneo kuizunguka Kigamboni...