US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

Kinetiq01,
Seems you know more than you are letting on. Mwaga data ndugu yetu hapa ndipo penyewe. Mwalimu aliwahi kusema mkiwakaribisha Wamarekani (militariry) hawataondoka.
 
Y'allah twafwa,

Sie wa Mbwamaji tutapona kweli?
 
Jamani,
Mimi sioni ajabu maana mengi hukanushwa na viongozi wetu na mwisho yanaonekana na wala hakuna anayeuliza.
Sasa nikisikiamipango hii sishangai. Na wala msitegemee mtu kujitokeza kusema ukweli hadhalani. Maana sana sana watakuja na utetezi kuwa hilo linahusu ni usalama wa taifa. Sijui ni usalama wa taifa gani hilo!
 
Jamani,
Mimi sioni ajabu maana mengi hukanushwa na viongozi wetu na mwisho yanaonekana na wala hakuna anayeuliza.
Sasa nikisikiamipango hii sishangai. Na wala msitegemee mtu kujitokeza kusema ukweli hadhalani. Maana sana sana watakuja na utetezi kuwa hilo linahusu ni usalama wa taifa. Sijui ni usalama wa taifa gani hilo!

sasa tunajua sababu ya safariya Bush nazile dola 758 millioni kwasababu nchi zote za Afrika magharibi walikataa. Kazi ipo!!
 
Hakuna sababu za msingi za kukataa base Japan and German kuna base na tunaona mafanikio yake, base siyo kitu kibaya kama tutaingia mikataba ya kusaidia nchi kwasababu tukikataa majina zetu watakubali na tutajuta. German wanaomba marekani isifunge base kwasababu imesaidia sana kiuchumi, kama kuna mtu hakubaliani basi atoe sababu za msingi???!!!
 
Kamundu, hakuna anayebisha hoja yako.Swala gumu zaidi hapa ni mwendelezo wa mwenendo wa usiri usio na manufaa kwetu, unaofanywa na viongozi wetu wa ngazi zote.

Hakuna afisa wa serikali [si mtendaji wa kijiji wala waziri] anayejitokeza wazi hadharani kuwaeleza wananchi kuhusu kinachokusudiwa kukifanya kuhusu "Kigamboni City Project", lack of transparency ndiyo issue.We need to be involved.Do they have anything to hide? Probably your guess is as good as mine.
 
Kamundu, hakuna anayebisha hoja yako.Swala gumu zaidi hapa ni mwendelezo wa mwenendo wa usiri usio na manufaa kwetu, unaofanywa na viongozi wetu wa ngazi zote.

Hakuna afisa wa serikali [si mtendaji wa kijiji wala waziri] anayejitokeza wazi hadharani kuwaeleza wananchi kuhusu kinachokusudiwa kukifanya kuhusu "Kigamboni City Project", lack of transparency ndiyo issue.We need to be involved.Do they have anything to hide? Probably your guess is as good as mine.

Ambassador was asked

Answering another question on claims that President Bush`s visit was intended to facilitate the establishment of the United States Africa Command (Africom) in Tanzania, Ambassador Green said: ``This is absurd. I have never heard anyone discuss that issue.``

source:
Why George Bush is coming to Tanzania

mwaandishi huyu alikuwa na wasiwasi

Kinachomleta Bush si kingine bali ni suala zima la AFRCOM na kulinda maslahi ya uwekezaji wa Kimarekani katika maeneo mbalimbali nchini, na hasa katika migodi ambako makampuni kadhaa kama Barrick, yana uhusiano na wakubwa nchini Marekani.

source:
Karibu Rais George Bush, lakini…

google may reveal more... 🙂
 
Well, I would rather have Americans on our motherland than Chinese! What has happened to Sudan amidist massive investments of Chinese, is just scary to contemplate.

Transparency? I guess we should just fight, the battle we are likely to win. Our governement and specifically our leaders have never been transparent, so I dont expect them to be in this issue. mbayo hata wananchi wengi hawaelewi. Sana sana tuwabane kwa yale ambayo tunajua wanaweza kuwa responsive.

Ukweli ni kwamba this particular issue can not even be a winning political card! because few (save elites na wasomi wa JF) hardly understand such millitary issues.

All in all, let them come as long as we are not being forced into this partnership and as long as there is strategic and mutual benefits for both sides.
 
Plans hizi za extension of United States Africa Command/Africom yalikuwa ni ya GWB na administration yake. Chance ya kutekelezwa kwa sasa ni 50/50. BHO/Democratic administration wana agenda zao - sasa hivi wanazungumzia kupunguza matumizi ya kijeshi, wafikiria kuachana na plans za missile defense system huko Poland & Czech Republic, etc.
 
Nakubaliana nawewe lakini inawezekana mipango haijakamilika
 
All in all, let them come as long as we are not being forced into this partnership and as long as there is strategic and mutual benefits for both sides.

Masanja,
Nashindwa kuona mutual benefits for both sides kati yetu na Marekani. As long as the imperialistic nature of the American military industrial complex does not change a small country like Tanzania cannot claim to have mutual benefits from having an American military base on its territory.
 
Mwanzoni mwa mwezi Januari 2009, nikiwa safarini kutoka Djibouti kupitia Ethiopia kwenda Great Britain nilikutana na "agent" mmoja wa shirika ambalo siwezi kutaja jina lake, akanieleza kuwa Marekani iko katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kutaka kujenga kambi ya jeshi la majini [strategic naval base] katika eneo kuizunguka Kigamboni.

Baada ya kufika huku ughaibuni ndipo nikasikia Bw John Chiligati ametoa kauli bungeni kuhusu ardhi yetu ya Kigamboni.Tatizo ni kwamba "mwekezaji" anayetaka kuihodhi ardhi hiyo amekuwa akieleza kuwa na mpango wa kuendeleza mradi as vague as 'Kigamboni City'.Chiligati aulizwe kuhusu habari hizi, msikie atasema nini.

Mpango huo unaelezewa kuhamisha "raia" katika radius ya kilometa kumi plus, kuwezesha ujenzi wa kambi itakayokuwa extension ya United States Africa Command ambayo inazidi kupewa uzito kule Djibouti.Watafanya dredging kuongeza kina kuhimilia mikiki ya "ndonga za kivita" kama aircraft carriers na submarines.Vile vile kutakuwa na airstip kwa ajili ya midege yao mizito kama B-52.

Kisa na Mkasa

Sababu ya wanyamwezi kukita mizizi ya ubepari wao katika majabali ya Tanzania ni kwamba wanataka kuiziba China isipate kujijenga Afrika Mashariki na vile vile Afrika Kusini ambayo pia imekuwa ikiwania sana pande hiyo ya Afrika.

Naomba nisisitize kuwa sina ushahidi kuthibitisha concern hiyo, lakini viongozi wetu wanajulikana kwa ulaghai na uhujumu.Something fishy is going on behind the scenes, only time will tell.Hakuna anayejitokeza kulizungumza head-on.Wote wanapiga porojo tu, at our expense.

Consipiracy Theory​

Itakumbukwa kuwa rais mstaafu wa Marekani, George W Bush, alifanya ziara "unique" nchini kwetu Februari 2008, pasipo maelezo ya kina ni kitu gani kilimfanya awe mgeni wetu kwa siku nne!

Inadhaniwa katika ziara hiyo aliamua kufika mwenyewe na makubaliano yote yafanyike katika adhi ya Tanzania, kuepusha zengwe kama la Karamagi kusaini mkataba famba hotelini jijini London.Alikamilisha mambo mengi, tuliyoambiwa ni asilimia 20 tu - mengine ni CLASSIFIED.

Je visa vya maharamia katika pwani ya Afrika Mashariki ni njama au hali halisi ya maisha ya wasomali waliokata tamaa?Tutasema nini tukiambiwa meli haziwezi tena kupita pwani ya Somalia?Je wakituambia wanataka kutusaidia tutakataa?Itakuwaje tukatae wakati bei ya mafuta itakuwa imefika shilingi 3000 kwa lita? Ah!! waache waje watukomboe bwana, japo wachache baadhi yetu tutapinga - majority ya wana JF watasema hapana, hatutaki.Lakini walioshika mpini watakuwa na maono sawa?

Mikakati​

Tayari Marekani imeongeza presence yake katika nyanja mbali mbali kwetu Tanzania.Hivi karibuni wamekata mshipa wa soni kwa kuanza kusaidia kambi ya jeshi la JWTZ pale Kigamboni.

Paradox?Sijui....kinachosubiriwa ni uchaguzi mkuu wa 2010, baada ya hapo tutaanza kuuziwa longo longo kwamba hali ya usalama ni mbaya na tunahitaji uwepo wa Marekani kusaidia kujenga ngome ya ulinzi.Tutasema nini watanzania sisi, wakati haya tuliyonayo mezani ya EPA, Richmond, na kashfa za migodi madini yetu yametushinda?Ni wazi kuwa kama wamekusudia watafanikisha lengo lao, tukilazia damu.

Anyway, ningependa kueleza mengi zaidi, lakini nasita.Lakini kama tukiwa hai, mengi yatajitokeza very soon.

Pamoja na kusita kwako juu ya uhakika wa ulichokieleza yaelekea ulidodosa vya kutosha kwa hilo JASUSI la kigeni kiasi kwamba una kiporo cha Datas unazuia. Na kwa elimu na uzoefu wa Majasusi nae alijua bila shaka amepata Sub agent wa kumwaga Mchele kwa Kuku wengi,kwani kwa mjadala huu tunaanza kuvunja Makali ya tukio halisi hapo litakapokuwa linatokea.katika jamvi huria nachukua nafasi ya Kuspekulet hilo jasusi uwezekano mkubwa ni kutoka C I A. Je waTZ, yaelekea mpira uko upande wetu wa kiwanja na MABEKI wetu ie VIONGOZI wetu ndio hao TAMAA mpaka Puani je hatujauzwa huku tunatembea???????
 
So does anybody actually have some evidence or is it just the same old rumours we have been hearing for years.
 
Sina uzoefu wa swala hili lakini silioni kama linatatizo sana naomba kama kuna mtaalamu atufanyie ''Cost Benefit Analysis'' ya mradi huu usiorasmi.

Usiri wa serikali kwakweli unaonyesha kutojiamini na maamuzi yao kwani hawana uwezo wakutetea huja kitaalamu. otherwise wanatakiwa kuwa wazi na kujiamini kama Gorge Bushi. Sifa ya kiongozi nikusimamia maamuzi yako na kuyatetea hatakama umekosea basi kilamtu ajue ni wewe uliye kosea sio kukwepa lawama. na kwa hili namfagilia George Bushi. Namtakia mapumziko mema
 
Haya ndio Guantanamo Bay nyingine hiyooooo!..
Yaliyowakuta Cuba ku lease ardhi yao kwa maswala ya base za Kiamerika, kisha wakashindwa kuirudisha baada ya kuona hawafaidiki isipokuwa shari tupu, ndiyo yatakayo fuata kwetu.. Tujifunze kutoka Cuba jamani..
 
JK atamwomba Obama asijenge kambi hiyo na atamwambia zile hela zilikuwa tu mambo ya njaa. Kwa sababu jirani ataelewa na huo mpango hautakuwepo tena. ...Just kidding. Kuna mahali nilisoma kuwa America have permanent interests and not permanent friends!!
 
Mwanzoni mwa mwezi Januari 2009, nikiwa safarini kutoka Djibouti kupitia Ethiopia kwenda Great Britain nilikutana na "agent" mmoja wa shirika ambalo siwezi kutaja jina lake, akanieleza kuwa Marekani iko katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kutaka kujenga kambi ya jeshi la majini [strategic naval base] katika eneo kuizunguka Kigamboni...

Duh, yaani huyo "agent" ulivyokutana naye akaamua tu kukupa hizo habari....haya bana, na mimi nina mpango wa kupita huko Djibouti na Ethiopia huenda huyo "agent" akanimegea na mimi hizo taarifa...
 
Back
Top Bottom