Naona kuna baadhi ya hawa majirani, wachawi. Ambao bado hawajachoka kungoja wakenya watwangane eti ili damu imwagike. Uchaguzi wa 2013 ulipita salama, wakingoja tu kwa hamu. Mwaka wa 2017 hivyo hivyo na sasa tupo 2022 na bado wanangoja tu, miaka kumi na bado wapo tu wakifanya dua zao nyeusi za kishirikina.
Tulieni majirani, hamna 'moral authority' yeyote ya kuzungumza na wakenya kuhusu uchaguzi au demokrasia. Sio baada ya ule usanii ambao mlifanya kwenye uchaguzi wenu mkuu uliopita. Pambaneni na hali yenu na matunda ya vibwenga vyenu hivyo. Ambayo najua mnayoana vizuri kwenye hilo bunge lenu la ajabu ajabu la sisiemu, ambalo halina mbele wala nyuma.