USA hata kama akasimama pekeake dhidi ya dunia nzima kivita, bado tutapigwa tu

Ah wapi....kiboko ya vigogo wote hapa duniani ni Taliban. Hao ndio wanaweza pigana na Dunia nzima na kuibuka washindi
 
US hakushindwa vita katika uwanja wa vita bali aliamua kuachana na hivyo vita baada ya upinzani mkali wa hivyo vita nyumbani kutoka kwa raia ambao walikuwa hawaoni maslahi yoyote kwao kuongezeka.
Unapoingia vitani unakuwa na malengo, kwaiyo kama hukutimiza lengo la vita unayopigana we umeshindwa.
 
Minapenda. Tu kuyaona yale madege yake makuubwa ya kijesh..na yale ma meli makuubwa yakikatiza huko katikat yabahari huku yame beba ndege vita nyingi...kiukwei na enjoy
 
Marekani kuishi nje haihusiani na serikali, ni tabia za mtu ndo zitafanya akose pakuishi. Wapangaji wengi marekani wanafukuzwa majumbani na kukataliwa kupangishwa kwa sababu nyingi sana na moja wapo ni nidhamu, uchafu, kelele, uzembe wa kulipa kodi na kuvunja mkataba wa kupangishwa so kwenye hilo itoe serikali.
 
Of course ni kweli ilikuwa Italy na turqiye
Lakini Mrusi alifanya hivyo baada ya kujua kuwa US ameweka makombora huko naye akaona isiwe tabu, ata sasa ili umchokoze Marekani fanya biashara ya siraha na Cuba basi atakuona wewe adui yake, hivi kwanini kwake akifanya Ukraine, Finland na Georgia ni sawa anasema demokrasia ila wewe ukisogea Cuba na Mexico uonekane mbaya?
 
Vipi mzee mbona na USA hataki CUBA aweke kambi za kijeshi za RUSSIA? au na yeye anaogopa Jeshi kubwa ka RUSSIA mpakani mwake? Kabla ya kuporoja fanya utafiti wa kina.Vita ya USA na RUSSIA hakuna mshindi ni kitu kinaitwa MUD yaani ni uhakika wa dunia kujiangamiza.Leo ingekuwa RUSSIA kaweka kambi CUBA basi siku nyingi USA angeimaliza DUNIA.Kikawaida USA na WEST pamoja wana tabia ya kujizima data na kutegemea upande mwingine watumie busara.
 
Kwani ina maajabu gani hiyo cuba missiles crisis? Hivi unajuwa kwamba baada ya ile crisis ikaja kugundulika kwamba USA alishaweka kitambo makombora poland yakielekea moscow? Na moja ya makubaliano ilikuwa naye ayaondoe hayo makombora
Tatizo wewe unaamini taarifa za BBC na CNN bil kuchuja.Kisa cha USSR kuweka missile CUBA ni baada ya NATO kuweka hizo missile ITALY na TURKEY.Nikita Khrushchev ndio alikuwa anawaforce NATO watoe Makombora yao yanayoelekea kwake ili dunia irudi kwenye usalama kwa wote.ALieanza choko choko ni NATO.Hata hii vita ya Ukraine imetengenezwa na USA lengo lao waifunje vunje Russia iwe vitaifa vidogo vingi.Moja ya makubaliano ya kuunganisha EAST na WEST German ilikuwa ni kuwa NATO haitaexpand hata yard moja kuelekea EAST.Lakini mabeberu hawaachi fikra zao za kikoloni wameexpand mno kuelekea EAST kinyume na makubaliano.
PUTIN aliweka mstari wake mwekundu kuwa UKRAINE isiingizwe NATO na kwenye makubaliano ya MINSK 2004 walisaini NATO na RUSSIA lakini washenzi ni washenzi tu wamekuwa wakipush sana UKRAINE iingie NATO na kibaya zaidi wakapindua serikali yake na kumuingiza kibaraka wao LEWINSKY pamoja na kuwaua maelfiu ya raia wa UKRAINE wanaozungumza kirusi.UKRAINE as nation is gone forever.Hii ndio upumbavu wa kukubali kutumika kama toilet paper.
 
Oy umewahi kuifuatilia vita ya Vietnam kweli?
Huko Vietnam huyo Marekani alitumia Kila mbinu kujihakikishia ushindi. Ndegezidi ya 5500 zilidondoshwa Kwa Manpads, vijana zaidiya 38000 elfu waliangamia huku maelfu wakiwa missing in action.
Wamarekani hao hao wamepelekea askari wao karibu laki 5 kuwa vilema na magonjwa kama kansa na mapafu nabaadae kifo Kwa kumwaga agent orange kemikali hatari iliyoteketeza karibu robo asilimia ya taifa la Vietnam.
Ni huko Vietnam ambapo Kwa mara y kwanza nuclear bomber B52 ilidondoshwa Kwa mara ya mwanzo.
Lakini wWavietnam walisimama kidete Mvamizi akakimbia vibaya
 
Oy umewahi kuifuatilia vita ya Vietnam kweli?
Huko Vietnam huyo Marekani alitumia Kila mbinu kujihakikishia ushindi. Ndegezidi ya 5500 zilidondoshwa Kwa Manpads, vijana zaidiya 38000 elfu waliangamia huku maelfu wakiwa missing in action.
Wamarekani hao hao wamepelekea askari wao karibu laki 5 kuwa vilema na magonjwa kama kansa na mapafu na baadae kufa Kwa kumwaga agent orange kemikali hatari iliyoteketeza karibu robo asilimia ya taifa la Vietnam.
Ni huko Vietnam ambapo Kwa mara y kwanza nuclear bomber B52 ilidondoshwa Kwa mara ya mwanzo.
Lakini wWavietnam walisimama kidete Mvamizi akakimbia vibaya
 
Biashara unamaanisha nini? Nchi inayoongoza kwa biashara duniani ni China. Biashara ya China duniani imeipita USA kwa zaidi ya USD 1.4trilion sasa unaposema biashara sijui unamaanisha biashara gani

Angali takwimu hapa chini toka Statista ambayo ni kammpuni ya USA

 
Puppet talk.Hana uwezo huo.Marekani na washirika wake wa NATO walikuwa na operation ya kuubadilisha utawala wa SYRIA kijeshi wamefikia wapi? Walibakiza 20KM wafike Damascus ndipo PUTIN akaamua kujoin kumsaidia ASSAD kilichobakia ni historia.Kama uwezo huo wanao mbona walishindwa kwenye lengo lao.
 
technology
China ndiyo nchi inaongoza duniani kwa ku file patent nyingi duniani ikiwa inaziacha mbali USA na nchi nyingine. Kwa hiyo haga upande wa technology kwa sasa USA hamuwezi China. Marekani ambaki kuongozi sehemu chache kwa patent ambazo ni pharmacetical na biotech japo nako soon ataachwa. Angalia tena Statista ambao ni USA wenyewe wanasemaje



Unaweza pia ukaangalia hapa shirika la kimataifa la patent WIPO nao wanaonesha nani mbabe wa kupatent duniani



 
Usipambe kushindwa ukakupa jina jingine.Ni kushindwa tu.Mission ya Afghanistan ilikuwa kuwaondoa TALEBAN madarakani sasa unapoondoka ukiwaacha wao madarakani ni kushindwa tu.
 
Na Ufaransa Amesha mpima Putin ubavu wake AKAONA size yake muda wowote Putin ajichangaje ndio atajua kumbe yeye ni tango pori
Ufaransa anajua ugomvi wake ni ugomvi wa NATO ndio maana anajitia vimaneno.Level ya RUSSIA ni NATO na washirika wake.Mzee haugopi nchi 54 zimeungana kumsapoti UKRAINE na bado anapoteza maeneo kwa kasi kubwa sembuse kijiufaransa kilichoshindwa mpaka na waasi wa MALI.
 
Marekani huyuhuyu aliyewashindwa Taleb huko Afghanistan kwa muda wa miaka 20 na kaishia kukimbia kama ngiri pori. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Haraka ya nini,fanya utafiti kabla ya kuandika.Nchi yenye makombora mengi zaidi ya Nuklia ni Russia na hata yeye anakisiwa kuwa na makombora 6000 na kidogo,USA 5000 na kidogo .Jumla duniani kunakisiwa kuwa na makombora ya nuklia 13000 tu.Sasa sijui hayo 100 million ya USA umetoa wapi.Kwa taarifa yako bomu la TSAR la urusi ndio kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa na kujaribiwa hapa duniani.Pamoja na yote hayo hakuna mshindi kwenye vita vya kinuklia, kwani hata mabomu machache tu yanatosha kuangamiza dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…