USA PROTESTERS: We don't need more Lockdowns its better to be contracted with SARS-CoV-2 than Lockdown

USA PROTESTERS: We don't need more Lockdowns its better to be contracted with SARS-CoV-2 than Lockdown

Hili limeripotiwa kutokea huko nchini marekani, inadaiwa Waandamanaji wamejitokeza kupinga vikali hatua ya serikali kupiga marufuku raia wake kutoka nje ya nyumba zao katika kipindi hiki ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya Covid-19.

Waandamanaji hao wanadai kuwa kufungiwa ndani (Lockdown) ni tishio kwa Uchumi wao Imara na kwamba inaweza kuwa sababu ya kupelekea anguko lingine la Uchumi, hivyo wanaitaka serikali kuachana na mpango huo haraka na kutengua uamuzi huo ili kunusuru Uchumi wa taifa hilo.

Ni nini maoni yako kwa hatua hii inayo chukuliwa na wamarekani?Je nchi zetu za kiafrica zipo tayari kupambana na madhara ya kiuchumi yatakayo tokea baada ya Total Lockdown?

Chanzo; BBC Swahili.
 
Leta picha tujionee wenyewe acha mambo ya oral traditions wakati huu wa advanced technology
 
Ni nini maoni yako kwa hatua hii inayo chukuliwa na wamarekani?Je nchi zetu za kiafrica zipo tayari kupambana na madhara ya kiuchumi yatakayo tokea baada ya Total Lockdown?
Fuatilia uone ni Wamarekani wa aina gani, na baada ya muda mfupi utagundua ni Wamarekani ambao kwa Tanzania ni kama misukule ya Lumumba ambayo ipo tayari kuunga mkono kila kitu kutoka Lumumba na Magogoni!!
 
Fuatilia uone ni Wamarekani wa aina gani, na baada ya muda mfupi utagundua ni Wamarekani ambao kwa Tanzania ni kama misukule ya Lumumba ambayo ipo tayari kuunga mkono kila kitu kutoka Lumumba na Magogoni!!
Mkuu samahani, naona umeathiliwa sana na huo Ulumumba na Ubavicha mkuu.
 
Mkuu samahani, naona umeathiliwa sana na huo Ulumumba na Ubavicha mkuu.
Look at you... nimekuambia fuatilia uone ni nani wanaotaka iondolewe hiyo lockdown!!

Kwa mfano, jana tu hapa Wall Street Journal na NBC wametoa matokeo ya polls ambayo heading inasema:-

More Americans Fear Lifting Coronavirus Restrictions Too Soon, WSJ/NBC Poll Says

Nearly 60% of respondents worry that lifting stay-at-home orders quickly will fuel the pandemic

Worries.png


Na hapo juu unaona mwenyewe... wakati karibu 60% ya Dems na Independent wana hofu restrictions kuondolewa mapema, ni less than 50% ya Reps ndio wenye hiyo hofu!!!

The question is: Hawana hofu au kwa sababu Trump ndie anapigia chapuo suala la stay at home kuondolewa?!
 
Sijui wanataka nini hawa watu[emoji1313][emoji1313]

Wamarekani waandamana baada ya kuchoshwa na kukaa majumbani
Apr 19, 2020 07:47 UTC
Mamia ya wananchi wa Marekani wamefanya maandamano katika miji na majimbo kadhaa kushinikiza kuondolewa kwa agizo la kuwataka wasalie majumbani mwao, kama njia ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Mamia ya wananchi wa Marekani waliochoshwa na agizo hilo la kutotoka nje wameandamana katika mji wa Concord jimbo la New Hampshire, Annapolis, na Texas.
Maandamano kama haya ya kutaka kuondolewa vikwazo vya kutoka nje kwa ajili ya kuzuia maambukizo ya virusi vya Corona nchini Marekani yalishuhudiwa siku chache zilizopita pia katika majimbo ya Minnesota, Michigan na Virginia.
Duru za habari zinaarifu kuwa, akthari ya walioshiriki maandamano hayo baadhi yao wakiwa wamebeba silaha za moto ni wafuasi wa chama tawala cha Republican. Rais Donald Trump amekuwa akivutana na magavana wa majimbo ya Marekani kuhusu suala la kufungua uchumi na shughuli za kila siku za nchi hiyo.
Magavana na watalaamu wa afya wa Marekani wamekuwa wakipiga azma ya Trump ya kuondolewa haraka iwezekanavyo vizingiti vya kiuchumi na kijamii, akiwa na lengo la kufanya kampeni za kutaka kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka huu.
Hii ni katika hali ambayo, idadi ya watu waliombukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imepindukia 740,000 huku zaidi ya 38,000 wakiaga dunia kwa ugonjwa huo na kuifanya nchi hiyo kuwa ndio iliyoathiriwa zaidi na virusi hivyo duniani.
Maandamano mengine yameshuhudiwa mjini New York, ambapo waandamanaji wamemwaga mifuko ya plastiki ya kufunga maiti nje ya Hoteli ya Trump, kulalamikia namna serikali yake imeshughulikia vibaya janga la Corona.

My take:Hilo bango lina ujumbe fulani hivi ambao kama nimeulewa hivi[emoji1313]View attachment 1423717

Sent using Jamii Forums mobile app

Hawa watu wakati mwingine akili zao matope kabisa, wengi wana adamana wameshikilia mitutu ya bunduki eansdahau kabida kuvaa face masks ambazo zina uwezo mkubwa wa kunusuru/linda maisha yao - kazi kuwaza vita masaa yote - we unafikiri siku hiyo ni Wamerika wangapi wali hambukizwa corona kwenye maadamano kama hayo pichani
 
Waandamanaji nchini Marekani wameingia mitaani katika majimbo kadhaa wakishinikiza magavana kufungua uchumi wa majimbo yao kwa kuondosha amri ya kutokutoka nje ama 'lockdown'.

Marufuku hiyo ya kutokutoka nje imewekwa katika majombo yote ya Marekani ili kudhibiti kusambaa kwa janga la virusi vya corona, hali iliyotikisa uchumi wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi duniani.

Maaandamano yameripotiwa jana Jumapili katika majimbo ya Arizona, Colorado, Montana na Washington, huku mwendelezo wa maandamano hayo ukitarajiwa leo Jumatatu.

Hasira juu ya marufuku hizo imeongezeka nchini humo huku waandamanaji wakitaka masharti yalegezwe licha ya hatari ambayo ingalipo ya maambukizi ya virusi vya corona.

Kwa sasa, Marekani ndiyo kitovu cha janga la ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19), kukiwa na wagonjwa zaidi ya 735,000 na vifo zaidi ya 40,000.

Hata hivyo kuna dalili kuwa maambukizi yanafikia kileleni nchini humo na kasi ya maambukizi kuanza kushuka katika baadhi ya majimbo.

Magavana katika majimbo mbalimbali wameanza majadiliano ya kufungua uchumi baada ya kushuhudiwa kupungua kwa maambukizi, lakini maeneo mengine bado yangali kwenye marufuku kali .

Gavana wa jimbo la California Gavin Newsom alikuwa wa kwanza kutoa amri ya watu kusalia nyumbani katika jimbo lenye watu wengi zaidi nchini humo toka Machi 19.

Majimbo jirani ya Washington na Oregon yakafuatia siku chache baadae na kufanya jumla ya watu milioni 11.5 wa majimbo hayo mawili kusalia ndani toka Machi 23.

Gavana wa New York Andrew Cuomo ametangaza wiki hii ametangaza kuongeza muda wa marufuku hiyo jimboni mwake mpaka kufikia Mei 15.

Virusi vya Corona: Marufuku ya kutotoka nje ndio suluhu ya corona

Akizungumza jana Jumapili Cuomo aliwataka wakazi wa jimbo hilo ambalo imeathirika zaidi kwa Marekani kujitenga na shauku ya jimbo lao kufunguliwa tena.

"Bado tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunakidhibiti kirusi hiki," amesema Cuomo. "Wakati ambao wote tukiwa na shauku na tukijiandaa kurejea katika maisha ya kawaida."

"Kwa sasa tupo tu mapumziko (baada ya kuisha kipindi cha kwanza) katika janga hili."

RaisTrump, ameonekana kuridhia maandamano hayo dhidi ya hatua kali za marufuku, akisema siku ya Ijumaa kuwa hatua zinazotekelezwa katika majimbo ya Minnesota, Michigan na Virginia "ni ngumu sana".

Hatua hizo hata hivyo zinahitajika ili kuzuia kusambaa kwa virusi.


==============

Chanzo cha habari:
Anti-lockdown crowd in Texas chants 'fire Fauci' and rally organizer in New Jersey is ARRESTED for violating stay-at-home orders as thousands ignore social distancing to protest stay-at-home orders
  • Protestors chanted 'fire Fauci' at a coronavirus lockdown rally in Austin, Texas, on Saturday
  • They were referring to Dr. Anthony Fauci, the country's top immunologist and infectious disease expert
  • Kim Pagan, of Toms River, New Jersey, was arrested for organizing the anti-lockdown rally in Trenton
  • Gov. Phil Murphy first implemented the coronavirus emergency orders last month
  • Several COVID-19 anti-lockdown protests were held by upset citizens around the United States on Friday
  • Protests happened in places like New Hampshire, Maryland, Oregon and New Jersey
  • President Trump doubled down on his tweets to 'LIBERATE' Minnesota, Michigan and Virginia
  • He told reporters at Friday's White House briefing that the Democratic governors in those three states could have gotten the same result with less restrictions
  • Trump also said the protesters, many of whom were Trump supporters, were 'treated a little bit rou
View attachment 1423053
Protestors in Austin, Texas, screamed 'fire Fauci' in a targeted chant against Dr. Anthony Fauci, the country's top immunologist and infectious disease expert.

Chanzo: Daily Mail
SI MLIKUWA MKIWASIFIA WADHUNGU KWAMBA NI WATU WAELEWA SANA? ANGALIENI HIYO NYOMI BILA KUJALI SOSHO SISTENSI HAHAHAHAHAHA. NA NDIO UNAAMBIWA HAO NDIO BINADABU WALIOTESWA SAID NA VIFO VYA KORONA LAKN BADO WANAKUSANYIKA NA KILA MTU KUTOA KELELE WAKAT UNAAMBIA KUONGEA KWA SAUT KUBWA TU KUNATOKA KURUSHA HEWANI VIJIDUDU VYA BWANA KOVID !!
 
Aisee... Hivi akili zenu mmepeleka wapi?

Yani ili tu lengo lako la hoja ya lock down kwa tz lionekane lina maana?
Fuatilia uone ni Wamarekani wa aina gani, na baada ya muda mfupi utagundua ni Wamarekani ambao kwa Tanzania ni kama misukule ya Lumumba ambayo ipo tayari kuunga mkono kila kitu kutoka Lumumba na Magogoni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni magazeti mengi tu yameripoti kuhusu hayo maandamano. Usijifanye mjuaji sana. Kwa kifupi huna lolote ulijualo.

Nimeishi UK miaka mingi na ni mwenyeji sana wa siasa zake na media zake. US vile vile. Mimi sio kijana btw. Sio kila unayempayukia hapa ni mwenzako.
 
Nimeishi UK miaka mingi na ni mwenyeji sana wa siasa zake na media zake. US vile vile. Mimi sio kijana btw. Sio kila unayempayukia hapa ni mwenzako.
Sasa yaani wewe limbukeni kuishi UK ndio nini. Unataka kumtambia nani?
 
Back
Top Bottom