USA wako serious sana. Uchumi wao ni mkubwa sana 30 trillion USD

Kweli uchumi wao unaonekana mkubwa, ila ukiangalia kwa karibu, unapata maswali yanayoweza kufikirisha. Kwa mfano, Marekani inasema uchumi wake ni $30 trilioni, lakini deni lake ni $33 trilioni. Hii ni kama mtu anayesema ana pesa nyingi, lakini ukweli ni kwamba pesa zake zote ni za mkopo—si zake halisi. Je, unadhani mtu wa aina hii anaweza kusema ni tajiri kweli?

Pia, pesa nyingi za Marekani zinahesabiwa kwenye huduma kama benki na masoko ya hisa, sio kwenye uzalishaji wa vitu halisi kama viwanda au kilimo. Hii ni kama mtu anayependa kuuza ndoto badala ya bidhaa halisi. Uchumi wa aina hii unategemea sana imani ya watu badala ya vitu vya kweli.

Zaidi ya hayo, pesa hizo $30 trilioni hazigawiwi sawa kwa watu wote. Matajiri wachache sana ndio wanamiliki karibu pesa zote, huku watu wa kawaida wakipambana kuishi. Hii ni kama familia inayojigamba kuwa na pesa nyingi, lakini baba peke yake ndiye anayeishi maisha ya kifahari huku watoto wake wakihangaika kupata chakula.

Na usisahau, serikali ya Marekani hutumia pesa nyingi sana kwenye mambo kama jeshi, na pesa hizo nyingi zinatoka kwa mikopo. Hii ni kama mtu anayejenga nyumba kubwa kwa mikopo, lakini hajui atairudishaje pesa hiyo baadaye.

Kwa hiyo, ingawa uchumi wao unaonekana mkubwa, ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya ukuaji huo ni wa bandia. Kama ungekuwa na mwenzako anayejisifu kwa mali alizonazo, lakini mali hiyo ni ya kukopa, ungemshauri ajijenge vizuri zaidi. Ndivyo tunavyoweza kujifunza kutoka Marekani.
 
Uchumi wakati watu kibao ni homeless kwenye Hilo Taifa
Homelessness ndio ubepari wenyewe, ni namna ya kucontrol uvivu kibepari. Amka ukafanye kazi, ishi kwenye mifumo ili upate one, two and three. Usipofanya kazi au ukiishi nje ya mfumo utakosa moja mbili tatu.

Ubepari=uchumi.

USA haishindwi hata mara moja kumpa kila homeless makazi. Ukimpa kila mtu makazi motivation ya maisha kwa watu wako itatoka wapi? What about labour? Watu hawatafanya kazi, No wonder huku kwetu watu wanaamua tu kupiga uvivu sababu wanajua nitakula kwa mjomba nitalala kwa shangazi ndio maana kijana wa 30’s si ajabu hana maisha yupo tu anaranda vijiweni.

Mifumo=Akili:
 
Demokrasia ni ungese mkubwa kinyama,we need Hitler kadhaaa afrika mbona tunawapita hao jamaa Kama wamesimama
Toka uhuru hadi leo Afrika ndio bara ambalo limetawaliwa sana na madikteta kuliko karibu mabara yote lakini leo hii ndio bara maskini kuliko mabara yote duniani.

Maendeleo sio kwamba uwe na utawala wa kiimla kwani ingekuwa hivyo basi leo hii Russia au Korea Kaskazini ndizo zingekuwa mataifa tajiri sana duniani.
 
Hakuna uhusiano wa maendeleo ya nchi fulani na mfumo unao iongoza.
 
huwa nashangazwa sana na waafrika wanapoicheka uchina kuwa na uchumi mdogo vs USA, vp khs afrika yenu vs USA? kwa nini mnaiponda China? au wewe ni USA au EU labda? au unajisahau na kufikiri wewe ni mzungu labda? mnasahahu miaka ya 60’ china ilikuwa masikini kama au klk hata afrika yetu, miaka 60 baadaye wameondoa njaa, wameboresha maisha ya watu wao, leo hii ni one of important countries duniani, wakati afrika yenu imerudi nyuma, per capital income ya afrika yetu ilikuwa higher wakati wa ukoloni klk leo hii, bado tunahangaika na chakula tu milo 3 kwa siku shida, sijaongelea mambo ya afya au hata makazi lkn bado unacheka Uchina?
Tanzania bado changa kaka.
 
Kweli uchumi wao unaonekana mkubwa, ila ukiangalia kwa karibu, unapata maswali yanayoweza kufikirisha. Kwa mfano, Marekani inasema uchumi wake ni $30 trilioni, lakini deni lake ni $33 trilioni. Hii ni kama mtu anayesema ana pesa nyingi, lakini ukweli ni kwamba pesa zake zote ni za mkopo—si zake halisi. Je, unadhani mtu wa aina hii anaweza kusema ni tajiri kweli?

Pia, pesa nyingi za Marekani zinahesabiwa kwenye huduma kama benki na masoko ya hisa, sio kwenye uzalishaji wa vitu halisi kama viwanda au kilimo. Hii ni kama mtu anayependa kuuza ndoto badala ya bidhaa halisi. Uchumi wa aina hii unategemea sana imani ya watu badala ya vitu vya kweli.

Zaidi ya hayo, pesa hizo $30 trilioni hazigawiwi sawa kwa watu wote. Matajiri wachache sana ndio wanamiliki karibu pesa zote, huku watu wa kawaida wakipambana kuishi. Hii ni kama familia inayojigamba kuwa na pesa nyingi, lakini baba peke yake ndiye anayeishi maisha ya kifahari huku watoto wake wakihangaika kupata chakula.

Na usisahau, serikali ya Marekani hutumia pesa nyingi sana kwenye mambo kama jeshi, na pesa hizo nyingi zinatoka kwa mikopo. Hii ni kama mtu anayejenga nyumba kubwa kwa mikopo, lakini hajui atairudishaje pesa hiyo baadaye.

Kwa hiyo, ingawa uchumi wao unaonekana mkubwa, ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya ukuaji huo ni wa bandia. Kama ungekuwa na mwenzako anayejisifu kwa mali alizonazo, lakini mali hiyo ni ya kukopa, ungemshauri ajijenge vizuri zaidi. Ndivyo tunavyoweza kujifunza kutoka Marekani.
So true, very few can see this

Umesema vyema, kwa mtu anayejua uchumi kwa uchambuzi huu atakubaliana nawe

Pia kwa kuongezea GDP ya Marekani inapandishwa sana na inflation kwenye spending mfano healthcare costs, kupanda kwa gharama za rents, matumizi ya kijeshi n.k
 
Lakini wakati huo deni lake ni kubwa kuliko GDP yake.

Ukomo wake wa kukopa bado sana sana infact debt cap ni asilimia 199% ya GDP na hapo GDP bado inatanuka kwa hadi asilimia 3 per annum
 
Kweli uchumi wao unaonekana mkubwa, ila ukiangalia kwa karibu, unapata maswali yanayoweza kufikirisha. Kwa mfano, Marekani inasema uchumi wake ni $30 trilioni, lakini deni lake ni $33 trilioni. Hii ni kama mtu anayesema ana pesa nyingi, lakini ukweli ni kwamba pesa zake zote ni za mkopo—si zake halisi. Je, unadhani mtu wa aina hii anaweza kusema ni tajiri kweli?

Pia, pesa nyingi za Marekani zinahesabiwa kwenye huduma kama benki na masoko ya hisa, sio kwenye uzalishaji wa vitu halisi kama viwanda au kilimo. Hii ni kama mtu anayependa kuuza ndoto badala ya bidhaa halisi. Uchumi wa aina hii unategemea sana imani ya watu badala ya vitu vya kweli.

Zaidi ya hayo, pesa hizo $30 trilioni hazigawiwi sawa kwa watu wote. Matajiri wachache sana ndio wanamiliki karibu pesa zote, huku watu wa kawaida wakipambana kuishi. Hii ni kama familia inayojigamba kuwa na pesa nyingi, lakini baba peke yake ndiye anayeishi maisha ya kifahari huku watoto wake wakihangaika kupata chakula.

Na usisahau, serikali ya Marekani hutumia pesa nyingi sana kwenye mambo kama jeshi, na pesa hizo nyingi zinatoka kwa mikopo. Hii ni kama mtu anayejenga nyumba kubwa kwa mikopo, lakini hajui atairudishaje pesa hiyo baadaye.

Kwa hiyo, ingawa uchumi wao unaonekana mkubwa, ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya ukuaji huo ni wa bandia. Kama ungekuwa na mwenzako anayejisifu kwa mali alizonazo, lakini mali hiyo ni ya kukopa, ungemshauri ajijenge vizuri zaidi. Ndivyo tunavyoweza kujifunza kutoka Marekani.
Uongo mkubwa. Marekani haizalishi??
 
Upo uhusiano mkubwa kati ya mfumo wa kiutawala na maendeleo, exceptions zipo pia kama za uarabuni
Ingekuwa hivyo basi nchi zinazo ongozwa kwa democracy yote yangekuwa tajiri na yale yanayo itwa ya kidkiteta yote yangekuwa masikini lakini ni tofauti.
 
Sijasema demokrasia inaleta utajiri wala udikteta unaleta umaskini, nimeongelea pia exceptions
 
Usilete ubishi GDP ya Marekani ukuaji wake kwa kiasi kikubwa unategemea hisa na masoko ya kifedha na sio viwanda kama China , Ujerumani au Japan
Hisa za nini? Za hewa? Sio za za makampuni na viwanda??
Coca-Cola, adidas, iPhone, dell, Pfizer n.k wakiuza hisa sio viwanda vimeuza hisa??
 
Sijasema demokrasia inaleta utajiri wala udikteta unaleta umaskini, nimeongelea pia exceptions
Ndio maana nimesema kuwa hakuna uhusiano wa maendeleo ya nchi na mfumo unao tumika kuongoza nchi.

Mfano kuna nchi nyingi tu ambazo mifumo ya uongozi wake ni kama wa nchi yetu lakini zina maendeleo wakati sisi ni masikini wa kutupwa.
 
Back
Top Bottom