Thamani ya pesa kuwa chini ndiyo ina promote exports.
Watu wengi hawaelewi somo hili la uchumi.
Mfano, watu wengi wanahusisha moja kwa moja thamani ya pesa kuwa chini na uchumi dhaifu.
Ukweli ni kwamba, nchi inaweza kuwa na uchumi mzuri na thamani ya pesa ikawa chini, zaidi, nchi inaweza kuwa na uchumi mzuri kwa sababu thamani ya pesa iko chini.
Angalia hili suala kihivi.
Nchi ikiwa na pesa yenye thamani kubwa sana, halafu inafanya manufacturing inataka kufanya exports nyingi, itapata tabu kufanya exports kwa sababu bidhaa zake zitakuwa ghali sana kuuza nje. USA ina tatizo hili sasa, US dollar ina thamani kubwa sana, hii ni moja ya sababu USA inashindwa manufacturing kwa ajili ya export. Ndiyo maana ni vigumu kuona vitu vya "Made in USA" Tanzania lakini ni rahisi kuona vya "Made in China".
Nchi ikiwa na pesa yenye thamani ndogo sana, halafu inafanya manufacturing inataka kufanya exports nyingi, itakuwa na urahisi kufanya exports nyingi, itapata urahisi kufanya exports kwa sababu bidhaa zake hazitakuwa ghali sana kuuza nje. China ina advantage hii. Yuan ya China iko relatively weak, kwa mfani, compared to US dollar.
Wachina wamefanya hesabu na ku calibrate makusudi pesa yao Yuan isipande sana thamani, wanajua wenyewe wata zi address disadvantages za weak currency vipi kwa kutumia increased exports. Mfano kwa ku produce sana ndani kiasi wasihitaji sana imports, moja ya vitu vinavyowapa disadvantages watu wenye weak currencies ni kwamba imports zinakuwa ghali sana. Mchina hana tatizo hiki sana kwa sababu anatengeneza vitu vingi hahitaji ku import sana.
Wachina wameiweka pesa yao isizidi thamani sana ili kuongeza exports kiasi kwamba advantages zinazotokana na kuongeza exports ziwe nyingi zaidi ya disadvantages za weak currency.
Somo kubwa hapa ni hipi.
Pesa yenye thamani kubwa si nzuri au mbaya kwa uchumi, pesa yenye thamani ndogo si nzuri au mbaya kwa uchumi.
Inategemea na uchumi wako ukoje, na unaitymiaje hiyo pesa.
Mfano sisi Tanzania tuna pesa yenye thamani ndogo hivyo tunapata hasara zote za kuwa na pesa yenye thamani ndogo, mfano imports nyingi ni expensive sana (tatizo ambalo China hawana sana kwa sababu wanatengeneza vitu vingi ndani). Lakini pia, licha ya sisi kuwa na disadvantages za kuwa na pesa yenye thamani ndogo, hata advantages za juwa na oesa yenye thamani ndogo (ku promote exports) hatuzitumii vizuri kwa sababu tuna export vitu katika level ya chini sana kulinganisha na tunavyoweza ku export optimally.
Watu wengi wanafikiri pesa kuqa na thamani ndogo inamaanisha uchumi ni mbaya, wakati kiukweli thamani yoyote ya pesa inaweza kuleta uchumi mzuri, tatizo ni jinsi unavyoitumia hiyo thamani, si thamani yenyewe.