Usafiri DAR mgumu, tunalipa nauli ya kugeuka na kusafiri kwa wakati mmoja, mamlaka Zinajua?

Usafiri DAR mgumu, tunalipa nauli ya kugeuka na kusafiri kwa wakati mmoja, mamlaka Zinajua?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Usafiri Kijiji la dsm ni mbaya sana. Ukitaka kupata nafasi kwenye daladala utalazimika kupanda daladala linalokwenda mwisho wa gari kisha ugeuze nalo kwenda safari Yako unakotaka kwenda. Kote huko lazima ulipe nauli ya kwenda kugeuka nalo na ile ya unakokwenda. Hii ni kadhia kubwa sana mbali na kadhia ya kubanana na kuibiana.

Sikuyajua haya hadi pale magari yangu yalipopata hitilafu na kuamua kutumia usafiri wa umma.

Kama viongozi wa serikali wangekuwa wanatumia usafiri wa umma huenda hali na mwenendo wa usafiri wa mabasi ya haraka UDART isingekuwa hivi ilivyo sasa.

Watu wanapoteza muda wa kufika kazini na majumbani, na hata wakifika wamechoka sana kwa kusimama na kubanana. Na hali ni mbaya sana kama watakutana na misafara ya viongozi, watasimama hapo masaa 2 hadi 4 kusubiri logistics za traffic.

Viongozi wetu Hawa jamani angalieni huku chini pia.
 
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Usafiri Kijiji la dsm ni mbaya sana. Ukitaka kupata nafasi kwenye daladala utalazimika kupanda daladala linalokwenda mwisho wa gari kiisha ugeuze nalo kwenda safari Yako unakotaka kwenda. Kote huko lazima ulipe nauli ya kwenda kugeuka nalobna ile ya unakokwenda. Hii ni kadhia kubwa sana mbali na kadhia ya kubanana na kuibiana.

Sikuyajua haya hadi pale magari yangu yalipopata hitilafu na kuamua kutumia usafiri wa umma.

Kama viongozi wa serikali wangekuwa wanaitumia usafiri wa umma hali na mwenendo wa usafiri wa mabasi ya haraka UDART isingekuwa hivi ilivyo sasa.

Watu wanapoteza muda wa kufika kazini na majumbani, na hata wakifika wamechoka sana kwa kusimama na kubanana. Na hali ni mbaya sana kama watakutana na misafara ya viongozi, watasimama hapo masaa 2 hadi 4 kusubiri logistics za traffic.

Viongozi wetu Hawa jamani angalieni huku chini pia.
Una magari mangapi hayo ambayo yalioata hitilafu kwa pamoja?

Haukuwa na haja ya kuweka hiyo statement hapo kwasababu kutomiliki gari sio ugonjwa
 
Una magari mangapi hayo ambayo yalioata hitilafu kwa pamoja?

Haukuwa na haja ya kuweka hiyo statement hapo kwasababu kutomiliki gari sio ugonjwa
Nilisafiri muda kidogo nikayaacha kwenye yard unattended, yanahitaji service, bima na battery mpya. Upo? Muda tu nitafix, ila nimeona jamii inapata tabu kiasi Gani kwenye upande huo. Bosi unapoona mfanyakazi amechelewa kufika kazini fikiria mara mbili, do not be judgemental kuhusu sababu ya kuchelewa kwake. Posho na mishahara mnayowapa izingatie nauli za kugeuka. Tunajua kuwa waajiri hawataki kujua mfanyakazi anaishi wapi, analala wapi wala anakuja vipi kazini na kurudi kwake.

Barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa kwanini hazina magari? Misafara ya viongozi inafahamu shida hizi za usafiri wa umma? Unaposimamisha magari yooooyoooote kwa muda mrefu yakupishe wewe unajua shida wanayoipata walioko kwenye madaladala?
 
Kote huko lazima ulipe nauli ya kwenda kugeuka nalobna ile ya unakokwenda.
Sio lazima, kugeuza na gari ni uamuzi binafsi wa abiria ili aweze kupata siti, option ipo ya kusimama, watu wanalipa pia wapiga debe kuwawahia siti. Bado hoja yako ya kadhia za usafiri wa umma ziko sawa.
 
Back
Top Bottom