Usafiri DAR mgumu, tunalipa nauli ya kugeuka na kusafiri kwa wakati mmoja, mamlaka Zinajua?

Usafiri DAR mgumu, tunalipa nauli ya kugeuka na kusafiri kwa wakati mmoja, mamlaka Zinajua?

🤣🤣🤣🤣 Mtoa thread elewa na tambua kwamba watz wenzako wamekwazika kusikia tu kwamba iwe kweli au sio kweli "Sikuyajua haya hadi pale magari yangu yalipopata hitilafu na kuamua kutumia usafiri wa umma.

Hawataki usemee unamagari🤣
 
Sio lazima, kugeuza na gari ni uamuzi binafsi wa abiria ili aweze kupata siti, option ipo ya kusimama, watu wanalipa pia wapiga debe kuwawahia siti. Bado hoja yako ya kadhia za usafiri wa umma ziko sawa.
Mpiga debe anawahi siti kisha unamlipa yeye kwanza kwa kazi hiyo halaf unamlipa konda nauli.
 
Nilisafiri muda kidogo nikayaacha kwenye yard unattended, yanahitaji service, bima na battery mpya. Upo? Muda tu nitafix, ila nimeona jamii inapata tabu kiasi Gani kwenye upande huo. Bosi unapoona mfanyakazi amechelewa kufika kazini fikiria mara mbili, do not be judgemental kuhusu sababu ya kuchelewa kwake. Posho na mishahara mnayowapa izingatie nauli za kugeuka.

Barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa kwanini hazina magari? Misafara ya viongozi inafahamu shida hizi za usafiri wa umma? Unaposimamisha magari yooooyoooote kwa muda mrefu yakupishe wewe unajua shida wanayoipata walioko kwenye madaladala?
Mkuu hama mbagara
 
Nunua gari, acha kulaumu wakati ni akili yako ndio imekufikisha hapo.
Hapana,umekosea kujibu hivi.

Dar Kuna watu zaidi ya milioni saba na hii kero anayoisema haimuhusu yeye as individual,ila kwa wakazi wote wa Dar ambao hawana uwezo wa kununua magari binafsi.

Mtu kuliongelea tatizo ambalo kiuhalisia lipo kweli alafu anakuja mtu mwingine kama wewe kujibu hivi ulivyojibu unaonyesha wewe ndiye una matatizo. Umemshambulia mleta hoja badala ya kuishambulia hoja.

Ad hominem fallacy.
 
Defensive mechanism "magari yangu mabovu"

Kama kweli unayo magari ya kutembelea, na kweli yamepata hitilafu ungeshindwa kutumia bolt kwenye mizunguko yako ? Kwann unabanana na vikwapa ?

Tafuta hela kwa wivu sana ndg yangu !
 
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Usafiri Kijiji la dsm ni mbaya sana. Ukitaka kupata nafasi kwenye daladala utalazimika kupanda daladala linalokwenda mwisho wa gari kiisha ugeuze nalo kwenda safari Yako unakotaka kwenda. Kote huko lazima ulipe nauli ya kwenda kugeuka nalobna ile ya unakokwenda. Hii ni kadhia kubwa sana mbali na kadhia ya kubanana na kuibiana.

Sikuyajua haya hadi pale magari yangu yalipopata hitilafu na kuamua kutumia usafiri wa umma.

Kama viongozi wa serikali wangekuwa wanaitumia usafiri wa umma hali na mwenendo wa usafiri wa mabasi ya haraka UDART isingekuwa hivi ilivyo sasa.

Watu wanapoteza muda wa kufika kazini na majumbani, na hata wakifika wamechoka sana kwa kusimama na kubanana. Na hali ni mbaya sana kama watakutana na misafara ya viongozi, watasimama hapo masaa 2 hadi 4 kusubiri logistics za traffic.

Viongozi wetu Hawa jamani angalieni huku chini pia.
Afu bado mna tick
 
😁😁😁😁😁 ukakosa pesa ya uber ama bolt?
Ningefanya hivyo haya ninayo advocate ningeyaona wapi?;Hii ni sauti ya wasiokuwa na sauti. Kwakuwa wamesafiri hivyo tangu utotoni wanadhani inatakiwa kuwa hivyo, kumbe ni upuuzi wa watu tu wasiotaka ku regulate usafiri wa umma.
 
Tatizo ni la kiuongozi - barabara zipo magari ya mwendo kasi hamna.

Yaani ni project pekee ambayo ina miundombinu tayari, wateja kibao ila inagfeli.
 
Hapana,umekosea kujibu hivi.

Dar Kuna watu zaidi ya milioni dsbana hii kero anayoisema haimihusu yeye as individual,ila kwa wakazi wote wa Dar ambao hawana uwezo wa kununua magari binafsi

Mtu kuliongelea tatizo ambalo kiuhalisia lipo kweli alafu anakuja mtu mwingine kama wewe kujibu hivi ulivyojibu unaonyesha wewe ndiye una matatizo. Umemshambulia mleta hoja badala ya kuishambulia hoja.

Ad hominem fallacy.
Barabara ya knara kariako, kariakoo Morocco, mbagala gerezani zimeisha tangu lini?;Zina magari mangapi?
 
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Usafiri Kijiji la dsm ni mbaya sana. Ukitaka kupata nafasi kwenye daladala utalazimika kupanda daladala linalokwenda mwisho wa gari kiisha ugeuze nalo kwenda safari Yako unakotaka kwenda. Kote huko lazima ulipe nauli ya kwenda kugeuka nalobna ile ya unakokwenda. Hii ni kadhia kubwa sana mbali na kadhia ya kubanana na kuibiana.

Sikuyajua haya hadi pale magari yangu yalipopata hitilafu na kuamua kutumia usafiri wa umma.

Kama viongozi wa serikali wangekuwa wanaitumia usafiri wa umma hali na mwenendo wa usafiri wa mabasi ya haraka UDART isingekuwa hivi ilivyo sasa.

Watu wanapoteza muda wa kufika kazini na majumbani, na hata wakifika wamechoka sana kwa kusimama na kubanana. Na hali ni mbaya sana kama watakutana na misafara ya viongozi, watasimama hapo masaa 2 hadi 4 kusubiri logistics za traffic.

Viongozi wetu Hawa jamani angalieni huku chini pia.
Mkuu usafiri wa UDART ni janga ni bora u-request bolt/Uber juzi Nilikuwa nataka kwenda Kivukoni Nilikuwa Magomeni Kagera nikakata Tiketi ya Mwendokasi mbona niliichana kwa hasira nikaenda kupanda daladala tu.

DK 50 hakuna basi linalosimama Kituoni yote yamejaza kama yamebeba magunia ya mahindi
 
Una magari mangapi hayo ambayo yalioata hitilafu kwa pamoja?

Haukuwa na haja ya kuweka hiyo statement hapo kwasababu kutomiliki gari sio ugonjwa
Kwakuwa situmii usafiri wa umma kwa muda mrefu mm niliiona ile hali sio sawa . Wewe unanishangaa kwakuwa umefanya tangu ukiwa primary school.
 
CHURA a.k.a Dalali YY hajui na wala hajali kuhusu watanganyika. Yy n zenji tu. Watanganyika tujipambanie.
Leo yy kakaa kwenye treni VVIP peke yake atajua haya. Na kurudi atapanda ndege.
Mkuu wa mkoa wake YY kapewa B 6 z kujengewa ofisi yake. Uko wakazi w DAR mki Haha tu.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Mpiga debe anawahi siti kisha unamlipa yeye kwanza kwa kazi hiyo halaf unamlipa konda nauli.
Yes, biashara binafsi kati ya bairia na mpiga debe, hutaki kubali kusimama ukikosa siti.
 
Mada yako ina mantiki umeharibu kwenye hoja ya magari yako, haikua na ulazima..

Tuko kwenye kizazi cha ovyo kabisa, nchi inarndeshwa kihunihuni, miradi inakufa, mikopo ya hali ya juu, huduma zote za umma ni bure kabisaa, je unaona ni mabasi tu, ujawahi kuwa na uhitaji wa huduma ya umma ukaona mambo yanakwendaje?
hospitali za umma ni ovyo ovyo bure kabisa bila kitu kidogo na kibima chako cha bei rahisi, utaoza bila kitu kidogo huko maofisini ni kujuana, mahakamani ndio usiseme.
Kizazi cha insta ni uchawa tu, kusifiasifia, wanatosheka na mlo wa siku moja wanasahau njaa ya miaka mitano
 
Back
Top Bottom