Kabisa hajakuwa, lakini ni kweli usafiri wa daladala una shida nyingi sana, na shida ni kubwa zaidi kwa wanafunzi, wajawazito, wagonjwa, walemavu na mama wenye watoto wachanga migongoni. Daladala zinajaza kiasi cha kukosa pahala pa kukanyaga, na foleni ndefu zinasababisha ile wahehe wanaita suffocation. Wakinadada wanajikuta wamelowana nyuma ya sketi na magauni yao pale inapotokea wamebanana na vijana barobaro wenye hisia kali.
Kama wakuu wangekuwa wanaifahamu hali hii huwenda wangeruhusu magari yooote ya abiria yapite kwenye barabara hizi za DART ambazo hazina magari ya kutosha ili kupunguza adha hii ya aibu kwa taifa.