Usafiri unakwamisha vijana wengi kujinasua kiuchumi.

Usafiri unakwamisha vijana wengi kujinasua kiuchumi.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nikiuliza bei ya kiroba cha mihogo sokoni niliambiwa ni 70,000-80,000. Inamaana ukiwa na heka tano za mihogo Kisarawe, na una van ndogo inayoweza kubeba viroba vinne kwa siku. Una uwezo wa kuingiza laki tatu kila siku ukipelela mihogo soko la ndizi asubuhi.

Jioni unawapa vijana viroba wakachimbe mihogo, anaekuletea kiroba kimejaa unampa 4,000. Unako ng’oa unasafisha na kupanda mingine.

Kinachokwamisha hapa ni jinsi ya kupata van. Kilimo kinahitaji uwekezaji. Ukiwa na mtaji wa kutosha ni rahisi kufanikiwa kwa kilimo.

1641920938765.png
 
Kuweza kufikisha bidhaa yako sokoni, kwa wakati na kwa Gharama nafuu ni hitaji la msingi la Kila biashara

Lazima kila uwekezaji uupime kwa vigezo mbali mbali ikiwemo return on investment

Lakini pia uangalie Kila option iliyopo, kwa mfano uliopo je ni lazima uwe na van ya kwako ili usafirishe mihogo ? Kama Kuna njia nyingine una opt hiyo
 
Huo muhogo umelimwa kwa miaka mingap?? Kilimo cha kwenye papers n rahis
Ulaji wa mihogo mjini unaongezeka kwa kasi kubwa sana kuanzia mihogo mibichi, ya kuchoma na kukaanga. Kutokana na dynamic ya wanaoishi mjini, wanaotumia mihogo kwa chakula wameongezeka sana. Mihogo imekua zao la chakula na biashara na ongezeko limejitokeza hivi karibuni.
 
Kuweza kufikisha bidhaa yako sokoni, kwa wakati na kwa Gharama nafuu ni hitaji la msingi la Kila biashara

Lazima kila uwekezaji uupime kwa vigezo mbali mbali ikiwemo return on investment

Lakini pia uangalie Kila option iliyopo, kwa mfano uliopo je ni lazima uwe na van ya kwako ili usafirishe mihogo ? Kama Kuna njia nyingine una opt hiyo
Kutumia usafiri wa mabasi kuna poteza fursa sana. Ni mara chache kupata public transport itakayokufikisha sokoni na kukodi kuna usumbufu. Kwanza unaona ni kheri niwe na viroba 10+ wakati usafiri ukiwa wako binafsi unaweza kupeleka viroba vinne na ukaridisha hela yako ya mafuta.
 
Huo muhogo umelimwa kwa miaka mingap?? Kilimo cha kwenye papers n rahis
Kawaida si razima kuwe na muda wa kukomaa? Kwani hio inazui nini kwenye kupeleka sokoni? Na pia mtu anaweza kugawa shamba kwa potion na akavuna mwaka mzima
 
Solution, nafkr ni muhimu tuwe na 'uber' ya kudeliver mizigo (especially) agri crops. Km ambavyo Uber inavyo 'deliver' abiria kila siku. Imagine uwe na uwezo wa ku request a van to come to ur farm and transport ur produce. Ni bonge la mchongo sema liko kinadharia bado. Kwasabab tukisema kila mkulima awe na van yake that's I'll be costfull wnye magar yao wa chip in kwny ecosystem ili kurahisisha kazi!.
 
Kilimo ni ajira nzuri ukiwa umewekeza mtaji wa kutosha. Si wote wangependa kuwa wakulima, kuna wengine wanaweza kuwa middle men.

Fikiria unaamua kuwa mkulima wa mboga na matunda kibaha au mlandizi. Unalima heka ya mchicha, nyingine bamia, nyingine nyanya.

Unaweka kisima na unakuwa na miundo mbinu ya umwagiliaji. Unaajiri vijana wachache wa kukusaidia. Unaweza kupeleka tenga au kiroba viroba vya mchicha, bamia na nyanya kila siku sokoni.

Middle men wenye usafiri wanaweza kununua kwa wakulima mashambani.
 
Back
Top Bottom