Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Usafiri wa anga nchini Tanzania ni usafiri ghali na wa gharama ya juu hadi kufikirisha ukilinganisha na mataifa mengine yakihusisha na safari kutoka bara moja hadi bara jingine.

Usafiri wa anga chini ya Air Tanzania kwa kiasi kikubwa ukisaidiana na Precision Air unaonekana kama umewalenga wanasiasa na wafanyabishara wakubwa.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Caracas, Venezuela hadi Madrid, Uhispania ni takriban $290 sawa na TZS 864,311 - hiyo ni nchi hadi nchi kwenye mabara mawili tofauti.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Bukoba, Tanzania hadi Dar es Salaam, Tanzania ni takriban TZS 631,000 sawa na €212 - hiyo ni mji hadi mji ndani ya nchi.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Fort Lauderdale, USA hadi Cartagena au Barranquilla, Colombia ni takriban $69 sawa na TZS 189,000 - hiyo ni nchi hadi nchi.

Safari ya ndege ya unganisho kutoka Mbeya, Tanzania hadi Mwanza, Tanzania ni takriban 1,100,000 sawa na $403 - hiyo ni jiji hadi jiji ndani ya nchi.

Hii ni mifano midogo sana maana kuna safari za kutoka Seoul, Korea Kusini hadi Barcelona kwa TZS 1,023,000.

Swali langu ni kwanini ATCL na washirika wake ndani ya nchi wana gharama kubwa katika usafirishaji! Je wanatumia teknolojia na mifumo tofauti na ghali ukilinganisha na mataifa mengine?

Ni sababu zipi za msingi zinazofanya flights za ndani ya nchi kuwa ghali maradufu kiuhalisia na hata ukilinganisha na mataifa mengine?

Ni maelekezo kutoka juu kuendelea kuwafinya watanzania wazidi kuishi kijamaa?

JamiiForums naomba msaada wa kuwatafuta ATCL, Mamlaka ya Anga na Wizara ya Uchukuzi watupatie ufafanuzi na statistics zinazohalalisha gharama za usafiri wa anga.
Mkuu unaumiza kichwa bure. Hakuna huduma yoyote iliyo chini ya serikali yenye kuleta ahueni na manufaa kwa wananchi zaidi ya kuwakamua na kuwamasikinisha zaidi. Tazama jinsi nauli za treni ya SGR zilivyokuwa inflated na serikali ya CCM kisa tu kupata hela za kugawana lwenye uchaguzi. Hii nchi ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
 
Wengi wetu bado katika nchi hii ni washamba, viongozi walio wengi tena ngazi za juu na baadhi ya watanzania wenzetu kwa kukosa kwao exposure wanawafanya watanzania waishi maisha magumu sana sana.
Leo hata hii electric train tunaanza kuifanya big deal sana.

Usafiri wa ndege kwasasa duniani ni usafiri tu wa kawaida sana na wala sio issue tena, sio ndege tu hata baadhi ya vitu kama magari, yatches na boats, washing machines majumbani, cooking gas, electricity nk. Huhitaji kuwa Tajiri kuvimiliki kwenye maisha ya Kila siku.

Hii biashara ya ndege tuache sasa kuimonopolize kwa ATCL pekee, tujenge viwanja tutangaze duniani huko tunataka wawekezaji kwenye Airline business na ATCL iwe mmoja wa washindani na wakishindwa kushindana tuibinafsishe kwa mtu binafsi na hao wafanyakazi timua woote.

Kenya wana KQ lakini bado ndani ya nchi yao yapo mashirika yanaruka kutoka Nairobi, Kisumu, Mombasa nk.

Tunapaswa kuwazoesha watu wetu hivi vitu wavione vya kawaida na sio big deal sana ili hata wakiwa viongozi wasiishi na akili za kijima.
Either tufanye maisha yawe mepesi mitaani ili watanzania waenjoy matunda ya uhuru au tuwafanya watanzania wawe na uchumi mzuri ili waweze kukimbizana na kasi ya gharama za maisha.
 
Kwanza unatakiwa ujue hakuna bei ya moja kwa moja ya ndege.

Kwa mfano; kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba ambapo wewe umeweka 631,000/- mtu anaweza kwenda kwa 335,100/- kama atapata lowest fare.

Mbeya kwenda Mwanza kupitia Dar es Salaam ambapo wewe umeweka 1,100,000/- mtu anaweza kwenda kwa 546,700/- kama atapata lowest fare.

Muhimu unapaswa kujua bei za ndege zipo determined na laws of demand and supply. Jitahidi kukata ticket mapema ambapo demand inakuwa chini kwa ndege husika na hivyo bei inakuwa chini.

Tuweni fair. Haya hufanyika duniani kote kwa airlines zote.
 
Almost fixed price kwa habari ya ATC, hizo fair price labda minus 50k, some wanayasema haya kama frequent flyers,
huwezi kuanza kuwafundisha hili leo.

Watu wote kwenye hii thread wanakifahamu wanachokiongea, hawajakurupuka!

Tunajaribu kusema kuwa kwanini usafiri wa ndege umegeuzwa kuwa anasa kubwa sana after 2015? Toeni majibu acheni janja janja.

Labda kama nyie wenzetu before 2015 hamjawahi fanya safari za ndani. (huu ndio mzizi wa hii thread)
 
Mkuu ni Kama naelewa unachozungumza ijapokuwa natamani kupata clarification vizuri zaidi .
Naomba tafadhali dadavua kinagaubaga
 
I am also a frequent flyer. Nimeshasafiri na AFN, ATC, APW, AKQ, AEK na AAA. Ninakijua nilichokiandika.
 
Ndege haina bei moja kama bus. Kwamba kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni 50,000/-.

Kwenye ndege kuna nauli nyingi. Kwa mfano; wewe unaweza kulipa 300,000/-, mwenzako akalipa 400,000/- na mwingine akalipa 600,000/- kwa safari hiyohiyo moja ya Dar es Salaam to Dodoma, na kwenye ndege hiyohiyo.

Tofauti ya bei ni kuwa mwenye bei ndogo alikata mapema wakati demand ilikuwa ndogo na mwenye bei kubwa amekata wakati demand ikiwa kubwa.
 
Kwanza unatakiwa ujue hakuna bei ya moja kwa moja ya ndege.

Kwa mfano; kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba ambapo wewe umeweka 631,000/- mtu anaweza kwenda kwa 335,100/- kama atapata lowest fare.

Mbeya kwenda Mwanza kupitia Dar es Salaam ambapo wewe umeweka 1,100,000/- mtu anaweza kwenda kwa 546,700/- kama atapata lowest fare.

Muhimu unapaswa kujua bei za ndege zipo determined na laws of demand and supply. Jitahidi kukata ticket mapema ambapo demand inakuwa chini kwa ndege husika na hivyo bei inakuwa chini.

Tuweni fair. Haya hufanyika duniani kote kwa airlines zote.
Hajui hata maana ya low season na high season kwenye ticket za ndrge

Na route zenye high demand bei huwa juu kuliko route zenye low demand

Pia hajui kuna low cost airlines za walala hoi Tanzania hatuna kuna moja ilikuwepo fast jet na Community airlines hazipo .Binafsi nilishawahi safari na fast Jet hadi Harare low season kws elfu 70 tu hadi Harare Zimbabwe nikapanda basi toka Harare hadi South Africa sababu kulipa ticket ya ndege za hadhi ya juu kama KQ na South African Airways,ATCL nk nilikuwa sina pesa hiyo nikaona nichukue cheap airline hadi Harare na from Harare nichukue basi

Mleta mada mshamba fulani sio airlines zote zinafanana kwa bei , status ,nk zingine ni kama daladala tu na bei zake ziko.chini

Kuja kutuletea ushamba wake wa ndege na kujitia kuponda ATCL ni mjinga sana
 
I am also a frequent flyer. Nimeshasafiri na AFN, ATC, APW, AKQ, AEK na AAA. Ninakijua nilichokiandika.
Unadhani hatukielewi unachokiandika!

Tunaelewa ila sio mzizi wa hii thread. Nani asiyejua unachokisema hapa?

Acha kupindisha mambo thread inazungumzia kitu tofauti, unatuhubiria ambacho tayari tunakifahamu.
 
Almost fixed price kwa habari ya ATC, hizo fair price labda minus 50k, some wanayasema haya kama frequent flyers,
huwezi kuanza kuwafundisha hili leo.

Watu wote kwenye hii thread wanakifahamu wanachokiongea, hawajakurupuka!

Tunajaribu kusema kuwa kwanini usafiri wa ndege umegeuzwa kuwa anasa kubwa sana after 2015? Toeni majibu acheni janja janja.

Labda kama nyie wenzetu before 2015 hamjawahi fanya safari za ndani. (huu ndio mzizi wa hii thread)
Hata tukimkubalia hili la Dar - Bukoba kwa 335,000k bado tutauliza why Miami hadi Barranquilla au Cartagena ni wastani wa 270,000?!

Gharama ni kubwa mno na zinaonekana wazi kuwa engineered makusudi kabisa.

A continent flight!
 
Hajui hata maana ya low season na high season kwenye ticket za ndrge

Na route zenye high demand bei huwa juu kuliko route zenye low demand

Pia hajui kuna low cost airlines za walala hoi Tanzania hatuna kuna moja ilikuwepo fast jet na Community airlines hazipo .Binafsi nilishawahi safari na fast Jet hadi Harare low season kws elfu 70 tu hadi Harare Zimbabwe nikapanda basi toka Harare hadi South Africa sababu kulipa ticket ya ndege za hadhi ya juu kama KQ na South African Airways,ATCL nilikuwa sina pesa hiyo

Mleta mada mshamba fulani sio airlines zote zinafanana kwa bei , status ,nk zingine ni kama daladala tu na bei zake ziko.chini

Kuja kutuletea ushamba wake wa ndege na kujitia kuponda ATCL ni mjinga sana
Kwanini umeassume hajui? Ukimsoma vizuri unaona ni mtu asiyejua?

Punguza kuwa sensitive, ATC si ya ukoo wa mtu.
 
Usafiri wa anga nchini Tanzania ni usafiri ghali na wa gharama ya juu hadi kufikirisha ukilinganisha na mataifa mengine yakihusisha na safari kutoka bara moja hadi bara jingine.

Usafiri wa anga chini ya Air Tanzania kwa kiasi kikubwa ukisaidiana na Precision Air unaonekana kama umewalenga wanasiasa na wafanyabishara wakubwa.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Caracas, Venezuela hadi Madrid, Uhispania ni takriban $290 sawa na TZS 864,311 - hiyo ni nchi hadi nchi kwenye mabara mawili tofauti.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Bukoba, Tanzania hadi Dar es Salaam, Tanzania ni takriban TZS 631,000 sawa na €212 - hiyo ni mji hadi mji ndani ya nchi.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Fort Lauderdale, USA hadi Cartagena au Barranquilla, Colombia ni takriban $69 sawa na TZS 189,000 - hiyo ni nchi hadi nchi.

Safari ya ndege ya unganisho kutoka Mbeya, Tanzania hadi Mwanza, Tanzania ni takriban 1,100,000 sawa na $403 - hiyo ni jiji hadi jiji ndani ya nchi.

Hii ni mifano midogo sana maana kuna safari za kutoka Seoul, Korea Kusini hadi Barcelona kwa TZS 1,023,000.

Swali langu ni kwanini ATCL na washirika wake ndani ya nchi wana gharama kubwa katika usafirishaji! Je wanatumia teknolojia na mifumo tofauti na ghali ukilinganisha na mataifa mengine?

Ni sababu zipi za msingi zinazofanya flights za ndani ya nchi kuwa ghali maradufu kiuhalisia na hata ukilinganisha na mataifa mengine?

Ni maelekezo kutoka juu kuendelea kuwafinya watanzania wazidi kuishi kijamaa?

JamiiForums naomba msaada wa kuwatafuta ATCL, Mamlaka ya Anga na Wizara ya Uchukuzi watupatie ufafanuzi na statistics zinazohalalisha gharama za usafiri wa anga.
Tozo za viwanja vya ndege vya hapo nyumbani, kwa kiasi fulani hutingisha nauli za ndege.

Ova
 
Flight ya mkoa mmoja kwenda mwingine ni sawa na kutoka Miami, US hadi Barranquilla, Colombia, au kutoka Singapore hadi Athens, Ugiriki au Bangkok, Thailand hadi Oslo, Finland.
Usisahau Ukitaka kwenda Libya au Algeria mara nyingine unapaswa kwanza kwenda Ulaya ndiyo urudi Africa, ni ngumu kulinganisha nchi za wenzetu na Africa kimiundombinu....mfano hakuna flight ya Mbeya- Mwanza inakuradhimu uje Kwanza Dsm ndiyo uende Mwanza.
 
Hajui hata maana ya low season na high season kwenye ticket za ndrge

Na route zenye high demand bei huwa juu kuliko route zenye low demand

Pia hajui kuna low cost airlines za walala hoi Tanzania hatuna kuna moja ilikuwepo fast jet na Community airlines hazipo .Binafsi nilishawahi safari na fast Jet hadi Harare low season kws elfu 70 tu hadi Harare Zimbabwe nikapanda basi toka Harare hadi South Africa sababu kulipa ticket ya ndege za hadhi ya juu kama KQ na South African Airways,ATCL nk nilikuwa sina pesa hiyo nikaona nichukue cheap airline hadi Harare na from Harare nichukue basi

Mleta mada mshamba fulani sio airlines zote zinafanana kwa bei , status ,nk zingine ni kama daladala tu na bei zake ziko.chini

Kuja kutuletea ushamba wake wa ndege na kujitia kuponda ATCL ni mjinga sana
Nitakujibu kwenye mlengo wa mada hii na kupuuza dhihaka au kejeli zisizokuwa na uthibitisho.

Tanzania imewahi kuona uwepo wa hizo unazozitanabaisha kama low budget airlines, ni nini kilipekea kusitisha huduma zake ilhali zilikuwa zinatengeneza faida?

Maswali yangu yanagusa pande zote kufahamu sababu zinazopelekea gharama kubwa ya usafiri wa anga nchini, na moja wapo inaweza kuwa hiyo ya ATCL kutotaka ushindani katika soko la ndani.
 
Back
Top Bottom