alma gemela
JF-Expert Member
- Feb 22, 2013
- 842
- 280
Mwaka 2007 nilienda Masasi...sehemu kubwa ya barabara ilikuwa inajengwa...yani tulitoka Dar asubuhi tukafika Masasi saa Mbili usiku...nilipanda Akida trans, siti mbovu...nilifika makalio yote hayafanyi kazi...
Ila siku hizi kitu Najma...saa nane mchana nivee kukayaaa ninkutauna ming'oko.....!
Nakumbuka enzi hizo Mlima Mmongo Lindi, gari ikishindwa kupandisha pale, lazima mlale mtake msitake.....sema kilichokuwa kinasaidia ni kuwa pale pembeni kuna kama kibwawa cha maji, basi tunajiloweka, tunasahau shida.
Ila sasa hivi ukipita hapo Mmongo na ukiambiwa kulikuwa na mlima utakataa.....kuko flattttttt, mambo ya Nkapa hayo.
Now Dar-Mtwara 7 hours wakati enzi hizo bila ya kulala siku 3 au 4 njiani basi hamjafika.
Mie nikishaiona Mikindani tu, moyo kunemenya kufurahi na ming'oko bila kusahau Chikandanga
Ulipanda bus bovu 2007 mbona tulikuwa tunafika saa kumi au tisa
Yote tisa, kumi Mr.Mkapa alipotuletea MV. SANTORINI
hahahaha, mpaka ikaitwa meli ya wanafunzi.
Maana yake likizo ikifika wanafunzi wooooote wa kusini haoooo melini, sema tu wale mabaharia wao walikuwa malaya sana, wanafunzi wametolewa sana bikira kule chini na hawa mabaharia wa Kigiriki.
Wanawavizia mkishuka ngazi, mnakuta wamejipanga huku wanakunywa bia, na walivyo wazuri basi wanafunzi wakiitwa tu, hao wanawafuata.
Wanaingizwa vyumbani mwao, wanakandamiziwa ukuni.
Aiseeee...tumetoka mbali saaaaaana.
Ila MV. SAFARI, sina hamu nayo!!!, umepanda meli kama umepanda mtumbwi unaoelekea MsangaMkuu!!
Linaitwa WIFIBachi gani hilo nkienda kuchamilia ntu yangu niyipande?
Ni kwa mara kwanza kusafiri na basi ambalo ni luxury kutokea Dar kwenda mkoa ule ambao miaka ya nyuma inasemekana ni mkoa uliosahaulika na ni sehemu ya adhabu kwa wafanyakazi wa serikali hii ya bongo.
Kichonikosha roho ni kuona basi hili likitoa huduma ambayo tulizoea kuziona kwenye njia za mikoa ile ya ukanda wa kaskazini, mwanzo kabisa wa safari wahudumu hujitambulisha kwa abiria wao, then kuwahabarisha utaratibu wa safari abiria wote kuhusu kufunga mkanda kwa usalama wetu, kutoa mifuko ya kuweka uchafu,utaratibu wa kuongea na muhudumu bila kubugudhi abiria mwezako, utaratibu wa kushuka kwenye gari,vinywaji baridi vya Azam. mwisho kumtanguliza Mungu kwenye safari.
Sasa kutokana hali hiyo nikakumbuka safari yangu ya 1995 kutoka huko Kusini kuja Dar ambao tulisafiri na lory kwa siku sita, usafiri mwingine ilikuwa meli siku mbili majini, duh Kusini tumetoka mbali.
Kikwete hoyeeeeeeeeeeee
Swadakta, hiyo like niliyokupa kwenye kitufe haitoshi ongeza na hiyo. huwa nashangaa hongera wanampa kiwete kwa lipi coz muhusika ni che benjaHivi huo ugonjwa Wa kusahau sahau mbona unakukabili kwa kasi namna hiyo? Hiyo ni kazi ya Mkapa na Magufuri (Rais mpendekezwa).
2007 barabara ilikuwa nzuri mbona labda somanga maana miaka hiyo nilikuwa nasoma Moshi na sikuwahi kufika usiku ni jioni. Miaka hiyo bus zilikuwa wahida, najma ni wakali wa rough road wakaja. Maana wahida inatoka tunduru inafika dar saa kumi na moja
kuna lingine la kwenda Newala limeanza safari kama mwezi sasa lina hadi huduma ya internet ndani...
LEO LUXURY...
ha ha ha Umeniwahi alma gemela kuuliza hilo swali. yaani haya mimi kanikumbusha mbali sana - enzi hizo nipo Mtwara girlsHahahaha madame B umesoma mtwara girls au masasi girls
ila nna ushauri wa bule kwa wale ndugu zangu waliozamia mikoa wezetu, nimeona kesi nyingi za viwanja apa mkoani vlvle viwanja vinapanda bei kila siku, so km ulikua na shamba la urithi ulilitelekeza njoo araka ulidhibiti la sivyo utakuta wazungu wameshajenga magorofa
maana zile sehemu ambazo awali wa2 walikuwa awazitaki ata bure leo hii wakina dangote wanazinunua kwa garama yoyote.
yaani yule dingi ake Riz angekubali gas izalishwe na kufanyiwa kazi apaapa baa soma mbona mikorosho yote tungeika
hivi viwanja kule msangamkuu vinapatikana?una connection yoyote kule?
msangamkuu bado kumepoa nafikiri unaweza pata kiwanja kirahisi kule, sijafika uko muda sasa tatizo kubwa kule ni inflastructure ya maji na umeme lkn km una nguvu kule sehemu kuwekeza kwa biashara kitalii, pia ukumbuke kuwa wakazi wa kule wamaraba wana maisha ya uswahili swahili
Mkuu Chingas wale wenyeji kuwa na maisha ya kiswahili hakutazuia maendelea kuingia msangamkuu,kununua kiwanja kule inawezekana?wale wenyeji wote watahamishwa na wenye pesa zao
mkapa na magufuli pongezi kwenu. huyu kikwete kwenye utawala wake wa miaka 9 sasa ameshindwa kumalizia zile km 60