Mwaka 2007 nilienda Masasi...sehemu kubwa ya barabara ilikuwa inajengwa...yani tulitoka Dar asubuhi tukafika Masasi saa Mbili usiku...nilipanda Akida trans, siti mbovu...nilifika makalio yote hayafanyi kazi...
Ila siku hizi kitu Najma...saa nane mchana nivee kukayaaa ninkutauna ming'oko.....!
Lol, umenikoshaje!!! Ming'oko, chikandanga, enzi zileee twaenda Mtwara girls (Red skirts) samaki wa Nangurukuru! I mis kusini daaah
Hahahaaa tena juzi kaka angu kanikumbusha kuhusu Mv Safari....yani meli ukipanda tu unaanza kutapikia mlangoni...Khaaaa...
Ila me nlikuwa ngangari nakula kila kitu ns sitapikii......tumetoka mbaliii...
Nakumbuka enzi hizo Mlima Mmongo Lindi, gari ikishindwa kupandisha pale, lazima mlale mtake msitake.....sema kilichokuwa kinasaidia ni kuwa pale pembeni kuna kama kibwawa cha maji, basi tunajiloweka, tunasahau shida.
Ila sasa hivi ukipita hapo Mmongo na ukiambiwa kulikuwa na mlima utakataa.....kuko flattttttt, mambo ya Nkapa hayo.
Now Dar-Mtwara 7 hours wakati enzi hizo bila ya kulala siku 3 au 4 njiani basi hamjafika.
Mie nikishaiona Mikindani tu, moyo kunemenya kufurahi na ming'oko bila kusahau Chikandanga
Hahaha Madame B umenikumbusha mbali MsangaMkuu lol..inaonekana unepiga sana kusini
chingas usemayo kweli kabisa japo sijayaoanda bado hayo mabasi ila nayaona barabarani ni mazuri
Ila pamoja na yote maisha Mtwara ni ghali sana...kila kitu ghali lodge ghali msosi ghali...muda mwingi lodge zimejaa nadhani shauri ya wachimba gesi..ni kama mji umevamiwa haukuwa umejiandaa kwa maingilio makubwa ya watu..
Lingine huduma kwa wateja bado sana kwa watu wa Mtwara..ni sheeder...
Ila kwenye viwanja kweli sasa ivi ghali sana vimepanda bei
Hahahaha madame B umesoma mtwara girls au masasi girls
ha ha ha Umeniwahi alma gemela kuuliza hilo swali. yaani haya mimi kanikumbusha mbali sana - enzi hizo nipo Mtwara girls
shoga angu mtwara unaijua wewe?sikuelewi
Kikwete ameingia ameingia madarakani amekuta km. 60 hazijakamilika
na mpk sasa haijakamilika
ndo kwanza anamwaga lami bagamoyo....
Bandari ya mtwara hakuna hela za kuboresha
ila kuna hela ya kujenga bandari mpya bagamoyo tehhhh
hivi viwanja kule msangamkuu vinapatikana?una connection yoyote kule?
umeona eeeh!!
kikwete hana mchango wowote akalale mbele 60kms for 9 yrs?
msifieni barabara ya kwenda kanda ya ziwa ila kusini big nooooook
Mie shost, Mtwara naijua....
Mie nacheza kotekote
Ila kile kipande, soon kitaisha maana mwezi Juni walikuwa wanamwaga mkeka rafu
wacha wee mtwara girls kumbee!!
naipata sana karibu na airport
wanakera kweli halafu barabara ile kila siku inajingwa hasa kutoka somanga kuelekea nangurukuru
Barabara yote imekamilika kwa lami?
Ni kwa mara kwanza kusafiri na basi ambalo ni luxury kutokea Dar kwenda mkoa ule ambao miaka ya nyuma inasemekana ni mkoa uliosahaulika na ni sehemu ya adhabu kwa wafanyakazi wa serikali hii ya bongo.
Kichonikosha roho ni kuona basi hili likitoa huduma ambayo tulizoea kuziona kwenye njia za mikoa ile ya ukanda wa kaskazini, mwanzo kabisa wa safari wahudumu hujitambulisha kwa abiria wao, then kuwahabarisha utaratibu wa safari abiria wote kuhusu kufunga mkanda kwa usalama wetu, kutoa mifuko ya kuweka uchafu,utaratibu wa kuongea na muhudumu bila kubugudhi abiria mwezako, utaratibu wa kushuka kwenye gari,vinywaji baridi vya Azam. mwisho kumtanguliza Mungu kwenye safari.
Sasa kutokana hali hiyo nikakumbuka safari yangu ya 1995 kutoka huko Kusini kuja Dar ambao tulisafiri na lory kwa siku sita, usafiri mwingine ilikuwa meli siku mbili majini, duh Kusini tumetoka mbali.
Yap pale pale.
Ila nilihama kwa mtutu nikahamia Dar si unajua utukutu wa form 2?