Usafiri wa Dar - Mtwara umenikosha roho

Usafiri wa Dar - Mtwara umenikosha roho

Mwaka 2007 nilienda Masasi...sehemu kubwa ya barabara ilikuwa inajengwa...yani tulitoka Dar asubuhi tukafika Masasi saa Mbili usiku...nilipanda Akida trans, siti mbovu...nilifika makalio yote hayafanyi kazi...
Ila siku hizi kitu Najma...saa nane mchana nivee kukayaaa ninkutauna ming'oko.....!

hahaaa uvee kukaya unatauna ming'oko
mipa ming'oko iiii
kwa masasi na nachingwea zipo NAJMA NA GAMET
MTWARA ZIPO MANING,BUTI LA ZUNGU,MACHINGA,FIVE ALLIANCE,JM NA MOJA NIMESAHAU HIZO NDO UHAKIKA NA SAFARI
NEWALA kuna IBRA NA LEO
LINDI MJINI kuna SADIA
 
Hii nilisafiri nayo jana, iko poa sana pia...!! Wametisha

2428mex.jpg

veygc6.jpg
 
Hahahaaa tena juzi kaka angu kanikumbusha kuhusu Mv Safari....yani meli ukipanda tu unaanza kutapikia mlangoni...Khaaaa...

Ila me nlikuwa ngangari nakula kila kitu ns sitapikii......tumetoka mbaliii...

Hahahah.... Kim nana, mie nilikuwa natapikia mlangoni kwa kweli.
Aisee ila ile meli acha tu.
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka enzi hizo Mlima Mmongo Lindi, gari ikishindwa kupandisha pale, lazima mlale mtake msitake.....sema kilichokuwa kinasaidia ni kuwa pale pembeni kuna kama kibwawa cha maji, basi tunajiloweka, tunasahau shida.

Ila sasa hivi ukipita hapo Mmongo na ukiambiwa kulikuwa na mlima utakataa.....kuko flattttttt, mambo ya Nkapa hayo.
Now Dar-Mtwara 7 hours wakati enzi hizo bila ya kulala siku 3 au 4 njiani basi hamjafika.
Mie nikishaiona Mikindani tu, moyo kunemenya kufurahi na ming'oko bila kusahau Chikandanga

shoga angu mtwara unaijua wewe?sikuelewi
 
Hahaha Madame B umenikumbusha mbali MsangaMkuu lol..inaonekana unepiga sana kusini
chingas usemayo kweli kabisa japo sijayaoanda bado hayo mabasi ila nayaona barabarani ni mazuri

Ila pamoja na yote maisha Mtwara ni ghali sana...kila kitu ghali lodge ghali msosi ghali...muda mwingi lodge zimejaa nadhani shauri ya wachimba gesi..ni kama mji umevamiwa haukuwa umejiandaa kwa maingilio makubwa ya watu..

Lingine huduma kwa wateja bado sana kwa watu wa Mtwara..ni sheeder...

Ila kwenye viwanja kweli sasa ivi ghali sana vimepanda bei

Sasa hivi maisha ghali sana hasa kutokana na huu mradi wa gesi.
Sio kama enzi zileeeee
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha Umeniwahi alma gemela kuuliza hilo swali. yaani haya mimi kanikumbusha mbali sana - enzi hizo nipo Mtwara girls

Kumbeeee, basi tulikuwa wote kwa mama Mshana, mama wa kichaga aliyekosa miguu lakini hodari kwa kuvaa vimini.
CC: MMAHE
 
Last edited by a moderator:
Kikwete ameingia ameingia madarakani amekuta km. 60 hazijakamilika

na mpk sasa haijakamilika

ndo kwanza anamwaga lami bagamoyo....

Bandari ya mtwara hakuna hela za kuboresha

ila kuna hela ya kujenga bandari mpya bagamoyo tehhhh

umeona eeeh!!
kikwete hana mchango wowote akalale mbele 60kms for 9 yrs?
msifieni barabara ya kwenda kanda ya ziwa ila kusini big nooooook
 
hivi viwanja kule msangamkuu vinapatikana?una connection yoyote kule?

wamebeba wazungu vingii sana asa hv viko juu
mi nilikua mtwara kikazi nimehama ila naweza nikakuulizia maana hua naendaga
 
umeona eeeh!!
kikwete hana mchango wowote akalale mbele 60kms for 9 yrs?
msifieni barabara ya kwenda kanda ya ziwa ila kusini big nooooook

Ila kile kipande, soon kitaisha maana mwezi Juni walikuwa wanamwaga mkeka rafu
 
wanakera kweli halafu barabara ile kila siku inajingwa hasa kutoka somanga kuelekea nangurukuru

Yaani kile kipande nyoko kweli, mie nikifika pale lazima nisimame maana naogopa kupasuka makalio yangu....kipande hakiishi tu.
 
  • Thanks
Reactions: awp
Barabara yote imekamilika kwa lami?

Bado sehemu ndogo toka Mohoro hadi Somanga kwa taarifa nilizonazo. Siku hizi kuna Bus za Mtwara na Lindi zinafanya zinaenda na kurudi siku hiyo hiyo!
 
Ni kwa mara kwanza kusafiri na basi ambalo ni luxury kutokea Dar kwenda mkoa ule ambao miaka ya nyuma inasemekana ni mkoa uliosahaulika na ni sehemu ya adhabu kwa wafanyakazi wa serikali hii ya bongo.

Kichonikosha roho ni kuona basi hili likitoa huduma ambayo tulizoea kuziona kwenye njia za mikoa ile ya ukanda wa kaskazini, mwanzo kabisa wa safari wahudumu hujitambulisha kwa abiria wao, then kuwahabarisha utaratibu wa safari abiria wote kuhusu kufunga mkanda kwa usalama wetu, kutoa mifuko ya kuweka uchafu,utaratibu wa kuongea na muhudumu bila kubugudhi abiria mwezako, utaratibu wa kushuka kwenye gari,vinywaji baridi vya Azam. mwisho kumtanguliza Mungu kwenye safari.

Sasa kutokana hali hiyo nikakumbuka safari yangu ya 1995 kutoka huko Kusini kuja Dar ambao tulisafiri na lory kwa siku sita, usafiri mwingine ilikuwa meli siku mbili majini, duh Kusini tumetoka mbali.

Hahaha mkuu bhana hilo basi linaitwaje?umenikumbusha safari yangu ya kutoka Mwanza-Dar nilipanda basi liko kama an aeroplane,huwa sina mazoea ya kulala safarini lakini muda huu sehemu kubwa ya safari nilikuwa fofofo.
 
Kumbeeee, basi tulikuwa wote kwa mama Mshana, mama wa kichaga aliyekosa miguu lakini hodari kwa kuvaa vimini.
CC: MMAHE
mmm Madame B, alikuwa mshana au mgana.... mwalimu lyuki, Aloyce na somebodey kaganda. na yule wa kifaransa aliyeshuka midomo alikuwa nani? Aloyce sasa yupo Morogoro.....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom