Usafiri wa ndege Dar es Salaam - Mwanza kwa Tsh 120,000, unaanza Machi 13, 2023

Usafiri wa ndege Dar es Salaam - Mwanza kwa Tsh 120,000, unaanza Machi 13, 2023

Kivipi mkuu sijakuelewa maana wiki nne zilizopita nimeenda Jhb mpaka Durban kwa rand 800 nadhani sawa na Tsh 112,000 na Tiketi ya Kuja Tanzania na Kurudi SA Kenya Airways kwa USD 300...pana muda bei ya ndege kwenda Cape Town kutokea JHB inakua chini kuliko Bus na bado bus zinajaa tuu...
Unalinganisha usafiri wa bus SA na bongo?
 
Mhh sio haina faida ila ni vigumu kupata faida ingawa neno linalotumika ni kuwa ina faida kidogo sana yaani very low margin!
Yaani ingekua haina faida hao Emarates na Qatar wangenunua ndege kubwa na kuwa na route karibu maeneo mengi ya Dunia hii huwezi kufanya biashara ya usafirishaji wakati Viongozi wanataka kupanda bure na kukatisha safari...
 
Yaani ingekua haina faida hao Emarates na Qatar wangenunua ndege kubwa na kuwa na route karibu maeneo mengi ya Dunia hii huwezi kufanya biashara ya usafirishaji wakati Viongozi wanataka kupanda bure na kukatisha safari...
Lengo la uwekezaji siyo lazima faida ya moja kwa moja bali uwezeshaji wa shughuli nyingine zenye faida na impact kubwa kwa nchi zao (Dubai na UAE) yaani multiplying effect! Mkuu Isanga Family kuna hako ka sentensi ka mwisho "viongozi wanataka kupanda bure na kukatisha safari" ebu kafafanue ili tujadiliane.
 
Ally's anawapiga sana huwezi mlipisha abiria 120k kwa Bus Coach, hiyo nauli ilitakiwa ichajiwe kwa Sleep Line Bus ambazo ni full luxury. Hata watu wa Latra hizo nauli wamepitisha kwa kufumba macho
Haulazimishwi mkuu wao wana gari za aina tatu kuna ambazo nauli 65k kuna 85k na 120k ni ww na pesa yako tu
 
Hii hapa gari dar mwanza ni 120,000 na zinapishana na zinajaa kila siku
IMG-20230303-WA0019.jpg
 
Basi hii kuiita vip na watu wanajaa , ni kutokana na uelewa mdogo wa abiria .
Ukienda hapo Zambia tu basi hii hupakii mtu labda kama wanaenda msibani.
Tunaongelea U tanzania ila unalazimisha Uzambia kwa kila mtu!! Ww jamaa vp!!
 
Tunaongelea U tanzania ila unalazimisha Uzambia kwa kila mtu!! Ww jamaa vp!!
Kwa hiyo ukiwa mtanzania ndo utumie low class?
Zambia ni masikini wenzetu tu ila wanajua products gani anapata kwa bei anayolipa
 
Hapana bro bado.mnaibiwa
Siti nyembamba
Inclinaation angle ya seat ni ndogo
Dirisha sio sealed kwa hiyo lina kelele
Suslension ni steel, bado mnaruka ruka kwemye matuta na rasta barabarani

Greyhound's 150 degree seat inclination, hii ni advert ya miaka 11 iliyopita , unaona kioo ni sealed na hiyo basi ni full air suspension
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    46.9 KB · Views: 6
  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    42.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom